Mimi huwa naona ni sababu za kimaslahi na udini.
Maslahi
Tuanze na Libya.
PLO ilikuwa inapewa sana msaada wa kifedha na Libya, pia Libya ilikuwa inatoa pressure kwa jumuiya ya kimataifa na umoja wa nchi za Kiarabu kuhusu agenda ya Palestina.
Hivyo Libya ilikuwa na uzito kwa PLO kuliko Tanzania ambayo ilikuwa inapiga kelele zaidi kwenye OAU lakini kelele zake kimataifa hazikuchukuliwa kwa uzito sawa na wa Libya. Heshima ya Tanzania kwenye UN ilikuwa ndogo kuliko heshima ya Libya, na bado Libya ilikuwa inasikika vizuri kwa Waarabu.
Kwa kuwa Libya ilikuwa upande wa Iddi Amin, PLO ililazimika kuwa upande wake vilevile. Leo hii Iran haiwezi pigana na Uturuki, alafu utarajie Hamas au Hezbollah wawe upande wa Uturuki wapigane na mfadhili wao na trainer.
Tukija kwa Uganda yenyewe.
Wakati Wapalestina wanateka ndege ya Israel mwaka 1976 waliileta Entebbe airport. Hapo Iddi Amin alijitoa mhanga kimataifa kuwaonyesha ushirikiano wa waziwazi Wapalestina. PLO walikuja kwa mshirika wao kwenye vita ya Kagera.
Naamini PLO walizingatia maslahi sababu hata kwenye uvamizi wa Iraq kwa Kuwait mwaka 1991, PLO walikuwa upande wa Iraq. Iraq ndio ilikuwa inawanufaisha kifedha na kupaza sauti UN na Arab League kuliko Kuwait wasiotaka shida.
Dini
Iddi Amin alisaidiwa na Gaddafi sababu ya dini yake.
Gaddafi alianzia Chad kwenye kusaidia upande wenye Waislamu, kwenye Chadian civil war alikuwa anasaidia kundi la Kiislamu, baadae akafanya annexation ya eneo la Chad. Baadae Chad ikapigana naye kwa ufanisi kwenye Toyota war ikashangaza dunia kuyatimua majeshi ya Libya.
Gaddafi pia aliwasaidia magaidi waliolipua disco mjini Berlin, hakuwa na sababu, dini tu.
Vilevile Gaddafi alimfanya Rais Albert Bernard Bongo kubadili dini na kuwa Omar Bongo ndio ampe misaada. Na kwenye hekaheka hizo, Bongo akaifanya Gabon iwe mwanachama wa Organization of Islamic Countries wakati Waislamu nchini humo hawakuwa hata 10%.
Ukija kwa PLO, hawajawahi kuwa involved kijeshi na upande usio wa dini yao.
Huwa nina hisia kwamba bila Gaddafi kuwataka PLO waje vitani Uganda, basi wao wasingekuja. Aliyewaita waje na aliyewasafirisha na kuwapa silaha ni Gaddafi. Kwa kifupi PLO kwao Mwalimu Nyerere ni 'kafiri mwenye kiherehere na kelele zisizo na nguvu'.