Paschal qamara
JF-Expert Member
- Aug 17, 2022
- 2,218
- 3,958
October 7 Hamas waliua wanajeshi pekee?Kuua watu kwa kuvunja miiko ya kivita (Rules & Customs of War) ni jambo la kishenzi kuwahi kufanywa na nchi ambayo inajiita imestaarabika kama Israel. Kiuhalisia Israeli walitegewa mtego na wakaingia mazima huku dunia ikishuhudia ukatili wao. Huwezi kuua watoto na wanawake kikatili vile.
October 7 Hamas waliua wanajeshi pekee?
Mimi huwa naona ni sababu za kimaslahi na udini.
Maslahi
Tuanze na Libya.
PLO ilikuwa inapewa sana msaada wa kifedha na Libya, pia Libya ilikuwa inatoa pressure kwa jumuiya ya kimataifa na umoja wa nchi za Kiarabu kuhusu agenda ya Palestina.
Hivyo Libya ilikuwa na uzito kwa PLO kuliko Tanzania ambayo ilikuwa inapiga kelele zaidi kwenye OAU lakini kelele zake kimataifa hazikuchukuliwa kwa uzito sawa na wa Libya. Heshima ya Tanzania kwenye UN ilikuwa ndogo kuliko heshima ya Libya, na bado Libya ilikuwa inasikika vizuri kwa Waarabu.
Kwa kuwa Libya ilikuwa upande wa Iddi Amin, PLO ililazimika kuwa upande wake vilevile. Leo hii Iran haiwezi pigana na Uturuki, alafu utarajie Hamas au Hezbollah wawe upande wa Uturuki wapigane na mfadhili wao na trainer.
Tukija kwa Uganda yenyewe.
Wakati Wapalestina wanateka ndege ya Israel mwaka 1976 waliileta Entebbe airport. Hapo Iddi Amin alijitoa mhanga kimataifa kuwaonyesha ushirikiano wa waziwazi Wapalestina. PLO walikuja kwa mshirika wao kwenye vita ya Kagera.
Naamini PLO walizingatia maslahi sababu hata kwenye uvamizi wa Iraq kwa Kuwait mwaka 1991, PLO walikuwa upande wa Iraq. Iraq ndio ilikuwa inawanufaisha kifedha na kupaza sauti UN na Arab League kuliko Kuwait wasiotaka shida.
Dini
Iddi Amin alisaidiwa na Gaddafi sababu ya dini yake.
Gaddafi alianzia Chad kwenye kusaidia upande wenye Waislamu, kwenye Chadian civil war alikuwa anasaidia kundi la Kiislamu, baadae akafanya annexation ya eneo la Chad. Baadae Chad ikapigana naye kwa ufanisi kwenye Toyota war ikashangaza dunia kuyatimua majeshi ya Libya.
Gaddafi pia aliwasaidia magaidi waliolipua disco mjini Berlin, hakuwa na sababu, dini tu.
Vilevile Gaddafi alimfanya Rais Albert Bernard Bongo kubadili dini na kuwa Omar Bongo ndio ampe misaada. Na kwenye hekaheka hizo, Bongo akaifanya Gabon iwe mwanachama wa Organization of Islamic Countries wakati Waislamu nchini humo hawakuwa hata 10%.
Ukija kwa PLO, hawajawahi kuwa involved kijeshi na upande usio wa dini yao.
Huwa nina hisia kwamba bila Gaddafi kuwataka PLO waje vitani Uganda, basi wao wasingekuja. Aliyewaita waje na aliyewasafirisha na kuwapa silaha ni Gaddafi. Kwa kifupi PLO kwao Mwalimu Nyerere ni 'kafiri mwenye kiherehere na kelele zisizo na nguvu'.
Mkuu nchi zote tatu namaanisha Egypt na Syria na Isrel zilisaidiwa na Marekani na Urusi na China kwa vifaa na washauri wa kijeshi na vipuri.Umemeza propaganda, Yom Kippur bila msaada wa Marekani Israel walishikwa pabaya na General Assad. Japo nakubaliana na wewe kuhusu suala la unafiki wa viongozi wa Afrika kwenye hili.
Mkuu hv zile body camera za wapiganaji wa hamas zilikua zinadanganya?????October 7 Hamas waliua wanajeshi pekee?
Mkuu ni kweli kabisa nakubaliana na ww kua mwanzo wa vita waarabu wa Syria walikua wanashinda na waliwateka na kuua wayahudi wengi.Na unajua kabisa hata General Assad....alikua anasaidiwa na Warusi....vile vifaru na vifaa vya kuona usiku gizani..ile kombainia ya vifaru ikiongozwa na ndugu yake aliyekufa vitani siku chache mbeleUmemeza propaganda, Yom Kippur bila msaada wa Marekani Israel walishikwa pabaya na General Assad. Japo nakubaliana na wewe kuhusu suala la unafiki wa viongozi wa Afrika kwenye hili.
Katika vita vya kagera au????Kama hoja ni dini, mbona ALGERIA taifa la kiislamu liliiunga mkono Tanzania na kutoa msaada muhimu kabisa ?
Nimeshalijibu hapo juu mkuuMbona hili swali alijibiwi hamna anaye jua jamani?
Mshikamo kweli nauona SUDAN na Somalia na Chad na Darfur na Libya na Syria na Iraqi na Mindiano state na Nigeria kaskazini kwa uchache tu...hawana tofauti na wakrsto wa Ireland kaskazini na Bosnia na mabudha wa Mynamar 😂🤣🤣🤣.Hakuna Dini, chama, ideology chenye mshikamamo kama Waislamu.
Waislam ushirikiana katika jambo lolote lile liwe Jema ama Ovu.
Uislam wa Amin Dada ulikuwa na nguvu kuliko uhusino wa Tanzania na Palestine.
Mkuu nchi zote tatu namaanisha Egypt na Syria na Isrel zilisaidiwa na Marekani na Urusi na China kwa vifaa na washauri wa kijeshi na vipuri.
Na hata Urusi ilitishia kuingilia vita kama IDF wataendelea kukaa mbele ya mji wa Isimailia na kukataa cease fire maana range zao za mizinga zilikua within Cairo city.
Mwanzo wa vita Egypt na Syria zilikua zinaelekea kuishinda Israel.....ila kibao kiligeuka.......nadhani unakumbuka siege za Sinai desert pale IDF walipowazunguka wale wanajeshi wa Egypt na kuwafanya mateka na kusababisha makamanda wa msiri wakubali mpango wa cease fire na kubadilishana mateka wa kivita!!!
Na nadhani unakumbuka pia makomandoo wa Egpyt jinsi walivyofanikiwa kuwaua wanajeshi wa IDF kama 700 hv na kuteka wengine mamia na kujipenyeza ndani kabisa ya jangwa la sahara lililokua chini ya IDF kasoro kule El sheikh....chini ya ulinzi wa mfumo wa kuzuia makombora na ndege za kijeshi wa urusi sikumbuki unaitwa SARS,s au la......na walifanikiwa kuangusha ndege 28 au 37 hv za IDF.....siku za mwanzo za vita..!!
Na nadhani unakumbuka pale mwanzo makomandoo smart wa vikosi vya parachuti wa jeshi la Syria walipofanikiwa kuteka vilima vya Golan....kabla ya kuzidiwa na kurudishwa nyuma mpaka bonde la mto Jordan upande wa kaskazini.
Kama kusingekua na cease fire basi IDF wangefika near Damascus na near Ismailia.....maana range za mzinga yao zilikua within Damascus town na Ismailia town na Cairo.
Japo nje ya Ismailia walipata upinzani mkali wa makomandoo wa jeshi la Egypt.
Propaganda ipo wapi mzeee???
Kama msaada wa kijeshi.......USA na France ziliisaidia Israeli silaha na vipuri......na Egypt na Syria walipewa silaha na vipuri walipewa na USSR na PRC.
SOMA VIZURI ANDIKO LANGU AFU UNIAMBIE PROPAGANDA NI IPI ???
NA NANI ALIUA ADUI WENGI???
NA NANI ALIKUA NA MATEKA WENGI????
KATI YA ISRAEL NA EGYPT NA SYRIA 1973
Mkuu ni kweli kabisa nakubaliana na ww kua mwanzo wa vita waarabu wa Syria walikua wanashinda na waliwateka na kuua wayahudi wengi.Na unajua kabisa hata General Assad....alikua anasaidiwa na Warusi....vile vifaru na vifaa vya kuona usiku gizani..ile kombainia ya vifaru ikiongozwa na ndugu yake aliyekufa vitani siku chache mbele
Na Usisahau hata pale makomando wa vikosi vya parachuti vya Syria walipoteka kwa mara ya kwanza zile stations za kijeshi juu ya vilima vya Golan....train walipewa na Warusi kabla ya vita...na hata walipozidiwa na wengine kuuawa na kushikwa mateka bado silaha za kirusi walikutwa nazo.
Usisahau kwamba IDF walipenetrate mpaka within Damascus range.!!
NB: TUNAWAPA CREDIT IDF SABABU WALIPIGANA NA NCHI MBILI NA KUSURVIVE NA BILA CEASE FIRE ZILIZOLAZIMISHWA NA USSR NA USA BASI IDF WANGETEKA MAENEO MENGINE YA SYRIA NA EGYPT.........KUMBUKA WAKATI WA CEASE FIRE ILIPOANZA KILA JESHI LILISIMAMA LILIPOISHIA NA HAPO NDIPO MSHINDI ALIONEKANA WAZI
PROPAGANDA NI IPI MKUU????
Katika vita vya kagera au????
Kama ni vita vya kagera....
Kumbuka walikua na uhasama na waarabu wenzao wa libya.....ilo lipo wazi.....na libya walikua wanawaunga mkono wanajeshi wa Amin.
Alitoka ahadi ya Watanzania kufunga mkanda kwa miezi 18,lakini mpaka sasa haijulikani mikanda ilifunguliwa lini.Vita ya Kagera chanzo ni urafik wa Nyerere na Obote,
Kitendo cha Amin kumpindua Obote kilimkwaza Sana Nyerere. Tangu hapo Nyerere na Obote wakawa na mipango ya Chini Chini ili kufanikisha Obote kurudi Madarakani.
Amin kuivamia Kagera ilikuwa Kama jibu Kwa Nyerere na onyo kumuonya aache kushirikiana na Obote kumhujum , Amin hakuwa na Nia ya kupora Kagera iwe Uganda maana alikuwa anatambua kuwa uwezo huo hana, yeye alikuwa amechoshwa na uswahiba wa Nyerere na Obote.
Kama unavyojua mtu anayekuchokoza hata kama unajua humuwez kimapigano bado huwezi kukaa kimya bali Kwa hasira utaokota hata jiwe.
Nyerere alikuwa akisubir Kwa ham Amin aingie kwenye 18 zake ili apate sababu za kumtoa Madarakani.
Ubinafsi wa Nyerere na hasira za Kizanaki ulichangia pakubwa vita hii ,, vita ambayo makovu yake bado yanaonekana nchini.
Baada ya Vita Nyerere alipambana awezavyo kuirudisha nchi kwenye mstari ikashindikana akaamua kubwaga manyanga miaka 6 au 5 na nusu baada ya Vita.
Vita ya Kagera chanzo ni urafik wa Nyerere na Obote,
Kitendo cha Amin kumpindua Obote kilimkwaza Sana Nyerere. Tangu hapo Nyerere na Obote wakawa na mipango ya Chini Chini ili kufanikisha Obote kurudi Madarakani.
Amin kuivamia Kagera ilikuwa Kama jibu Kwa Nyerere na onyo kumuonya aache kushirikiana na Obote kumhujum , Amin hakuwa na Nia ya kupora Kagera iwe Uganda maana alikuwa anatambua kuwa uwezo huo hana, yeye alikuwa amechoshwa na uswahiba wa Nyerere na Obote.
Kama unavyojua mtu anayekuchokoza hata kama unajua humuwez kimapigano bado huwezi kukaa kimya bali Kwa hasira utaokota hata jiwe.
Nyerere alikuwa akisubir Kwa ham Amin aingie kwenye 18 zake ili apate sababu za kumtoa Madarakani.
Ubinafsi wa Nyerere na hasira za Kizanaki ulichangia pakubwa vita hii ,, vita ambayo makovu yake bado yanaonekana nchini.
Baada ya Vita Nyerere alipambana awezavyo kuirudisha nchi kwenye mstari ikashindikana akaamua kubwaga manyanga miaka 6 au 5 na nusu baada ya Vita.
*kichwa kuleHaya mambo mnafundishwa Sunday school. Mnatiwa sumu dhidi ya waislam na uislam. Mkija humu mnaandika utumbo usiokichwa waala miguu
kwa sababu,IDDI AMIN alikuwa MWISLAM na NYERERE alikuwa MKRISTOTanzania ilikuwa moja ya nchi kinara barani Afrika kutetea haki za Wapalestina. Nchi hii ilienda mbali na kuamua hata kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na nchi ya Israel mwaka 1973 baada ya shinikizo la nchi za kiarabu zilizokuwepo ndani ya O.A.U kuwa kubwa.
Ikumbukwe Israel walikuwa na mchango mkubwa kwa Tanzania kuliko hata Palestine, kwasababu wao ndiyo walisaidia katika kufundisha maafisa wengi wa jeshi la Tanzania, akiwemo Marehemu Generali Muhiddin Kimario, pamoja na kusuka JKT.
Mwaka 1973, baada ya vita vya Yom Kippur nchi nyingi za Afrika zilivunja mahusiano ya kidiplomasia na Israel, na kuanza kutetea haki za Wapalestina. Ukisoma nyaraka za OAU, moja katika falsafa inazozipinga ni UZAYUNI (ZIONISM) na UBAGUZI WA RANGI (APARTHEID).
Tanzania ilikwenda mbali na kuanza kutetea haki za wapalestina kule UN. Kinachoshangaza ni kwamba Palestine Liberation Organization (PLO), mbali na kuwa marafiki wa Tanzania, walijiunga na vikosi vya Libya katika kumsaidia Idd Amin ambaye alikuwa anapambana na Tanzania.
Ikumbukwe tu, mwaka 1973 Tanzania ndiyo ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuitambua PLO na kuruhusu kundi hilo kujenga makao yake jijini Dar es salaam. Ofisi za PLO jijini , Dar es salaam ndiyo yalikuwa makao makuu ya PLO barani Afrika. Katika moja ya nukuu ambayo Mzee Nyerere aliwahi kuitoa kuhusu Palestina ni hii:
"Kizazi chetu kilikuwa kizazi cha mapambano ya utaifa kwa ajili ya uhuru wa nchi zetu … lakini hali ya Wapalestina ni tofauti sana na mbaya zaidi, Wamenyang’anywa nchi yao wenyewe, Kwa hiyo wanastahili kuungwa mkono na Tanzania na dunia nzima"
Najiuliza tu, chanzo kikubwa cha PLO kuisaliti nchi ambayo ilikuwa inawatetea hivi ni nini ?
View attachment 2857800