Kwanini wapiga kura wameamua kuifuta CHADEMA?

Chadema kikiwa chini ya katibu mkuu Dr Slaa mtu muadilifu wa kweli mkakati wake kama chama cha upinzani ulikua kupinga rushwa na kutaka uwepo wa utawala bora. Wakati Dr Slaa akiwa Katibu Mkuu nchi ilikua imeoza kwa rushwa kuanzia chama tawala CCM chenyewe na serikali yake hadi maisha uraiani. Hakuna kitu mtu unafanikisha bila kuhonga. Watu wengi walijiandaa kupigia kura upinzani 2015 kuondoa utawala wa wala rushwa.

Wengi walitegemea kuona Dr Slaa akiteuliwa kama mgombea wa Chadema jambo ambalo lilifanyika ila mwenyekiti Mbowe akaweka uteuzi wa Dr Slaa kibindoni badala yake inaaminika akafanya biashara ya kuuza uteuzi kwa mgombea aliyebwagwa huko CCM na kumfanya mgombea wa Chadema.

Mgombea huyo kutoka CCM, Chadema ndio walikua wanamshambulia miaka mingi kama kinara wa rushwa nchini.

Baada ya ushindi wa Magufuli kiongozi thabiti mpinga rushwa na mjenzi wa nchi Chadema badala ya kuja na mkakati na mbinu za upinzani chanya kwa maendeleo ya nchi wakaanguka kwenye mtego wa kutumiwa na nchi za nje zilizotaka kuona Magufuli anashindwa kutokana na kubana maslahi ya makampuni yao ya kinyonyaji.

Chadema wakakubali kupinga kila mradi wa maendeleo kuanzia miundombinu elimu na afya eti ni vitu tu havina maana kwao cha maana ni uhuru haki na maendeleo.

Wakataka kufanya raia wajinga sana hawaoni uhusiano kati ya miradi ya serikali ya CCM na maendeleo yao. Zaidi ya hapo chadema wakawa waongo na wazushi kuhusu haki za binadamu na kusema nchi inahitaji kukombolewa toka utawala eti dhalimu wa CCM.

Kutokana utendaji mzuri na kampeni bora kabisa toka CCM na mgombea urais wake kama wengi walivyotarajia Chadema ni kama imefutika.

Walifanya makosa makubwa ya kimkakati kwa kugeuza lengo lao kuu ni kuingia madarakani tu wakati wangeweza kua tayari kuunga mkono uongozi mzuri unapokuepo. Wamefanya chama cha siasa ni kwa ajili ya maendeleo ya viongozi wa chama badala ya maendeleo ya wananchi.
 
Attachments

  • VID-20201103-WA0000.mp4
    919.5 KB
Wapiga kura wameamua kufuta chadema! Hii si kweli. Sasa ni chama kipi cha upinzani hawajakifuta? Waliotaka kuifuta chadema ni wale waliozuia mikutano ya kisiasa. Walionyima nafasi upinzani kwenye vyombo vya habari vya taifa. Waliofuta bunge live nk.

Mbinu ilifanya kazi vizuri sana vijijini na kwa watu wasio na smart phones. Ilifanya wapinzani wasahaulike kabisa huku kila siku ccm wakionekana nchi nzima miaka 5.
Habari walizopata kuhusu wapinzani ni mbaya tu kama makesi nk.

Haujafa Tanzania nao ni kama maji tu yatafuata kanuni zake. Kuiua chadema sio kuua upinzani.
 
CHADEMA kikiwa chini ya katibu mkuu Dkt. Slaa mtu muadilifu wa kweli mkakati wake kama chama cha upinzani ulikua kupinga rushwa na kutaka uwepo wa utawala bora. Wakati Dr Slaa akiwa Katibu Mkuu nchi ilikua imeoza kwa rushwa kuanzia chama tawala CCM chenyewe na serikali yake hadi maisha uraiani. Hakuna kitu mtu unafanikisha bila kuhonga. Watu wengi walijiandaa kupigia kura upinzani 2015 kuondoa utawala wa wala rushwa.

Wengi walitegemea kuona Dr Slaa akiteuliwa kama mgombea wa Chadema jambo ambalo lilifanyika ila mwenyekiti Mbowe akaweka uteuzi wa Dr Slaa kibindoni badala yake inaaminika akafanya biashara ya kuuza uteuzi kwa mgombea aliyebwagwa huko CCM na kumfanya mgombea wa Chadema.

Mgombea huyo kutoka CCM, Chadema ndio walikua wanamshambulia miaka mingi kama kinara wa rushwa nchini.

Baada ya ushindi wa Magufuli kiongozi thabiti mpinga rushwa na mjenzi wa nchi Chadema badala ya kuja na mkakati na mbinu za upinzani chanya kwa maendeleo ya nchi wakaanguka kwenye mtego wa kutumiwa na nchi za nje zilizotaka kuona Magufuli anashindwa kutokana na kubana maslahi ya makampuni yao ya kinyonyaji.

Chadema wakakubali kupinga kila mradi wa maendeleo kuanzia miundombinu elimu na afya eti ni vitu tu havina maana kwao cha maana ni uhuru haki na maendeleo.

Wakataka kufanya raia wajinga sana hawaoni uhusiano kati ya miradi ya serikali ya CCM na maendeleo yao. Zaidi ya hapo chadema wakawa waongo na wazushi kuhusu haki za binadamu na kusema nchi inahitaji kukombolewa toka utawala eti dhalimu wa CCM.

Kutokana utendaji mzuri na kampeni bora kabisa toka CCM na mgombea urais wake kama wengi walivyotarajia Chadema ni kama imefutika.

Walifanya makosa makubwa ya kimkakati kwa kugeuza lengo lao kuu ni kuingia madarakani tu wakati wangeweza kua tayari kuunga mkono uongozi mzuri unapokuepo. Wamefanya chama cha siasa ni kwa ajili ya maendeleo ya viongozi wa chama badala ya maendeleo ya wananchi.
Ujinga wako mkubwa.
 
CCM mlichokuwa mnakitafuta sasa mnakwenda kukipata!! Ni suala la muda tu.
 
Back
Top Bottom