Unafikiri media za Tz ziko huru?Sasa imekuwa kama imehalalishwa vile kwa viongozi wa upinzani kuvikacha vyombo vya habari vya ndani na kukimbilia media za nje na za washindani wetu wa kiuchumi.
Alianza Zitto na zile fedha za kusaidia elimu ya watoto wa kike lakini kwa bahati nzuri WB wakamshushua na kumpuuza. Zitto aliitumia BBC badala ya media za ndani.
Sasa Tundu Lissu naye anayarudia makosa yaleyale, hivi kwanini mnakwepa media zetu?
Inakera sana.
Maendeleo hayana vyama!
Je wapinzani wakihojiwa na media za nje ulitaka wakimbie?
Je walichoongea kwny hizo media ni kuhusu uchumi?
Kwa hiyo walienda kuwaambia habari za ndege, sgr na stigler's gorge? Kwamba kwenye kutekeleza miradi hiyo kuna siri za kiuchumi?
Mim najua walizungumza habari za watu kutekwa, kuuwawa, kuzushiwa makesi, vyombo husika kushindwa kkufanya uchunguzi na kutoa majibu ya matukio ya kihalifu eg Lissu kupigwa risasi akiwa maeneo rasmi ya serekali yenye ulinzi, kuuwawa kwa kina Mwangosi, Mawazo Akwilina etc. Vilevile media za Tz kuogopeshwa kufanya coverage ya shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani ma tv ya taifa kumilikiwa na ccm.