JET SALLI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 2,392
- 1,578
Ndugu zangu nimejiuliza maswali kadha wa kadha kuhusu suala la MWAJIRI kupitia ofisi ya Afisa utumishi kuingiza makato ktk mshahara wa mtumishi kwa vyama viwili tofauti vya wafanyakazi ktk mshahara wa mtumishi,nimefuatilia suala la Sumbawanga ,vilevile bado nafuatilia na mikoa,pamoja na wilaya nyingine ili kujua ukubwa wa tatizo hili,na ninaona suala hili la kutokuheshimu kanuni na sheria linatokea sana kwa upande wa WALIMU,Mwezi uliopita niliandika humu kuhusu suala la Mkurugenzi wa MANISPAA ya Sumbawanga,pamoja na Afisa utumishi wake walivyoingiza makato ya vyama viwili ktk mishahara ya walimu bila ridhaa yao na tunajua waraka ambao ndio sheria yenyewe inakataza kabisa tabia hii.Mtumishi ananya kazi Mwezi mzima na analipwa ujira wake hv mtu wa pili anaetamani pesa ambayo Mwalimu huyu kaitolea jasho Mwezi mzima na hivyo anajisikia kuikwapua bila ridhaa ya mwenye pesa ile ni nani.Na ni kweli kabisa CWT wamekua wakifanya kampeni chafu dhidi ya chama mwenza CHAKUHAWATA,Na hii inaonyesha kwa namna gani uwezo wa kufikiri ni mdogo kwa viongozi wa CWT kwa ngazi zote kuanzia kwenye matawi mpaka taifa.Hv kweli unaweza ukatamani kutokupoteza wanachama halafu ukaendelea na ujinga wa zamani usijirekebishe na hivyo ukaendelea kuwa punguwani tu,hii haiingii akili kama kweli CWT ina viongozi wenye akili timamu kabisa lzm Kuna shida.Itoshe kujifunza yafuatayo,ndani ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania vipo vyama vingi vya wafanyakazi kwa uchache nitaje baadhi na taasisi zake.Kwa mfano
a)wafanyakazi wa Serikali kuu vyama vyao ni THT,TEWUTA,RAAWU,
b)Taasisi za fedha vyama vyao ni TUICO na FIBUCA
c)Wafanyakazi wa migodini vyama vyao ni NUMET na TAMICO.
d)Na ndugu zetu waelimishaji wa Taifa ambao ni walimu vyama vyao ni CWT na CHAKUHAWATA.
Watumishi wote wa Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wanajiunga na chama chenye unafuu kwao na sio chama kinachofikiria kuvuna fedha bila ridhaa ya mtumishi husika.
Naendelea kutoa WITO kwa serikali sikivu ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania chini ya mama shupavu asiyependa watu waonewe na kuteseka SAMIA SULUHU HASSAN Kuhakikisha kwamba kanuni na sheria za kiutumishi zinaeshimika ndani ya nchi hii kwa kuzingatia sheria ya Ajira na mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004 na mm kila nikitafakari sielewi kwanini Kwenye sekta ya UALIMU SHERIA HII HAIHESHIMIKI je wakurugenzi,Maafisa Utumishi na wanasheria ktk MANISPAA na wilaya zetu kama inavyotokea kule SUMBAWANGA MANISPAA je wameshindwa kutafsiri sheria na kama wameshindwa kutafsiri sheria iliyo wazi nn kifanyike kwa watu kama hawa wenye kuonyesha uwezo mdogo,wakati Serikali ina hazina ya Rasilimali watu tena wasomi wabobevu haipaswi kuwa na watendaji mfano wa Mkurugenzi wa MANISPAA ya SUMBAWANGA na Afisa utumishi wake kwa mambo wanyowatendea walimu ndani ya MANISPAA ya Sumbawanga.