Kwanini waraka wa kisheria unaomkataza mwajiri kuingiza makato ya vyama viwili vya wafanyakazi kwa mpigo bila ridhaa ya mtumishi,hauheshimiwi?

Mkuu kwenye huu mjadala usiweke hisia. Weka vifungu kama sajo . Mwenzio anaandika kitachotakiwa kufanyika wewe unaandika kinachofanyika-ambacho ni kosa
Huyo jamaa mwenyewe hiyo Sheria anayoizungumzia haijui.
 

Attachments

  • Screenshot_20221224-140050.png
    59.4 KB · Views: 41
Wewe jamaa una ubishi wa kichoko kinoma. Unajifanya unajua Sheria kuliko Sheria yenyewe na CMA.
Sawa mkuu, mimi ninakuambia kuwa hakuna kifungu cha 72(c) cha sheria ya ajira na uhusiano kazini, unaita hiyo ni ubishi wa kichoko, haya tuma wewe kifungu cha 72(c) cha hiyo sheria.
 
Huyo jamaa mwenyewe hiyo Sheria anayoizungumzia haijui.
Ukishindwa hoja utaanza kurukaruka kama hivi unavyofanya, sasa hapo ulichotuma ni kipi, maana umekomaa na kifungu cha 72(c) ila ulichotuma hapa sioni hicho kifungu, sasa unapelekea uelewa wako juu ya sheria ya ELRA kuwa wa kutia shaka.
 
Ukishindwa hoja utaanza kurukaruka kama hivi unavyofanya, sasa hapo ulichotuma ni kipi, maana umekomaa na kifungu cha 72(c) ila ulichotuma hapa sioni hicho kifungu, sasa unapelekea uelewa wako juu ya sheria ya ELRA kuwa wa kutia shaka.
Una akili ndogo sana. Endelea kubishana Kama JUHA.

Maana uelewa wako ni mdogo sana.
 
Lakini mkuu kwenye hiyo sheria hawajafafanua hiyo ada ya uwakala ilipwe kwa kipindi gani.
 
Lakini mkuu kwenye hiyo sheria hawajafafanua hiyo ada ya uwakala ilipwe kwa kipindi gani.
Sijaelewa unaposema kipindi gani unaongelea muda (duration) au mazingira (circumstance), lakini vyovyote vile, iwe unaongelea muda au mazingira, ni kweli sheria haijaonesha muda wa makato utakuwa ni muda gani lakini tafsiri ni kuwa inatakiwa makato yawe kwa muda tu ambapo majadiliano yatakuwa yakifanyika (kama majadiliano ni ya miezi 4 - basi makato yatakuwa kwa miezi 4) au mara 1 tu ikiwa majadiliano yalichukua muda mfupi ndani ya mwezi 1 tu.
 
Bado ipo too vague
 
Walimu ni malofa
 
Kama kuna walimu wanahama CWT basi kasi inatakiwa iwe kubwa zaidi maana fedha zao zinaliwa kwa kasi kubwa sana.
Vyama vya wafanyakazi wanashirikiana na MWAJIRI Kumuumiza MTUMISHI.

Anayeingiza Makato ya mshahara kwenye Salary slip ni MWAJIRI.

Kwahiyo kulaumu vyama vya wafanyakazi pekee ni kutojua ADUI HALISI NI Nani.
 
Bado ipo too vague
Ni kweli. Lakini hii haitumiki sana, binafsi niliishuhudia ikitumika mwaka 2012 kukata mishahara ya walimu wasio wanachama wa CWT kwa kuwa chama kiliwafanyia majadiliano na serikali kipindi cha mgomo wa walimu usio na kikomo ambapo serikali iliazimia kuwafukuza kazi walimu wote waliogoma na baada ya majadiliano ikaondoa nia hiyo. Sasa hivi sasa (2023) mtumishi ukikatwa ada ya uwakala (agency shop fee) ni lazima upewe maelezo umekatwa kwa sababu ipi, maana hakuna majadiliano rasmi yanayofanywa kati ya chama cha wafanyakazi na serikali ambayo yanawanufaisha wafanyakazi wote.
 
Anayekata pesa za mishahara ni nani?
 
Ni Mwajiri
Mwajiri anakata pesa anawapa vyama vya wafanyakazi.

Mwajiri ndio mtunzi wa na msimamizi wa sheria.

Mwajiri huyo huyo ndio hakimu wa kesi za watumishi.

Mwajiri huyo huyo akitaka kusikiliza changamoto za watumishi anasikiliza kutoka kwenye vyama vya wafanyakazi.

Unaona Hali halisi???
 
Huo ndio uhalisia. Lakini kumbuka nilikuambia kuwa sheria hailazimishi mtumishi kuwa mwanachama wa chama cha wafanyakazi, na hata kama ni mwanachama insmruhusu kujitoa chamani kama akipenda. Sasa watumishi wengi hawajui hili wanaishia kukatwa mshahara pasipo kuhiyari wala kupenda.
 
HAKUNA mtumishi anayelazimishwa kuijunga na chama Cha wafanyakazi.

Na hata Kama ukijiunga utaratibu wa kujitoa uko wazi.

Changamoto ya Makato hasa kwa wasio wanachama iko kwenye ADA YA UWAKALA.

Hiyo ADA YA UWAKALA inatumika, uwe mwanachama au usiwe mwanachama WANAKATA.

Na Hali ni mbaya zaidi ikitokea DHRO/Afisa Utumishi nanDED ni wanufaika wa pesa za hivi vyama.
 
Changamoto ya Makato hasa kwa wasio wanachama iko kwenye ADA YA UWAKALA.

Hiyo ADA YA UWAKALA inatumika, uwe mwanachama
Naam, sasa umeanza kuelewa somo kuwa kujiunga na vyama vya wafanyakazi ni jambo la hiyari, kwamba sio lazima mfanyakazi awe ni mwanachama wa chama cha wafanyakazi.

Tukija kwenye makato ya ada ya uwakala, hukatwi tu pasipo sababu, ni lazima kuwe na justification ya kukatwa kwake. Nimetoa mfano, kama kuna majadiliano yamefanyika mwezi huo na kada yako ikihusika, hapo utakatwa mshahara.

Sasa kama unakatwa bila maelezo, ni haki yako kupinga makato yasiyo halali. Unamshtaki mwajiri wako kwa kukata mshahara bila uhalali, yeye ndiye aeleze ni kwa mujibu wa nini aliamua kukata hiyo ada ya uwakala. Itamlazimu kuonesha barua kutoka hicho chama majority inayomuomba akate ada ya uwakala kwa kuwa chama kimefanya kazi fulani, bila hiyo makato ni batili, anatakiwa kurejesha fedha yako (mwajiri).

Vivyohivyo, hata kama chama majority kikiwa na barua ya kuuomba ada ya uwakala ila ukiwa unaamini hakuna majadiliano kilichoyafanya, napo unaweza kukishtaki chenyewe na mwajiri kwa kukukata pesa yako pasipo halali. Hili suala lipo ndani ya mtumishi na sio kuwa anaonewa pasipo kupewa njia ya kujitetea.

Changamoto iliyopo sasa ni kuwa migogoro ya watumishi wa umma imezuiwa kwenda CMA ila iende Tume ya Utumishi wa Umma (PSC). Huko kusikilizwa inachukua miaka 2 na zaidi
 

Sababu inayotumika siku zote ni moja, na ipo kwenye sheria.

"Ikitokea katika eneo lako la kazi at least Nusu ya wafanyakazi ni wanachama wa chama Cha wafanyakazi, then Chama kinazungumza na Mwajiri kwaajili ya kukata hiyo ADA YA UWAKALA"


Note: Mwajiri=Chama Cha wafanyakazi ni YALE YALE.
Nimetoa mfano, kama kuna majadiliano yamefanyika mwezi huo na kada yako ikihusika, hapo utakatwa mshahara.
Hayo majadiliano anafanya NANI na NANI?
Unamshtaki Mwajiri wapi huko unakohisi utatendewa HAKI ???

Iwe CMA au PSC HAKUNA Cha maana utapata. Nimekuwekea taarifa ya hukumu ya walimu 347 kutoka CMA umeona??

Kitu pekee unachoweza kufanya labda mchongo tu, uongee na Afisa Utumishi binafsi akutoe.

Lakini as long as Sheria ya Ajira itabaki kuwa Kama ilivyo HAKUNA pa kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…