I wonder kama umenielewa
RnB kuna vitu artists wanaigana
same as hip hop na singeli na bongo fleva...
Na kuna standards zikiwekwa na msanii mmoja the rest wanafuata..
na ku add glamour kwa msanii ni kitu chenye nguvu...
Ulichoandika si rocket science wala si total solar eclipse kiasi nishindwe kuelewa.
Wewe unazungumzia standards au unazungumzia 'niche' ya msanii individually?
Mimi naona hapo unachanganya madesa.
Hata huko Marekani unapopenda kupatolea mfano kuna wasanii kibao tu waliofanikiwa kwa kujitofautisha na wengine.
Hakuna 'universal' industry standard inayofuatwa kama unavodai.
Labda cha muhimu zaidi ni kulenga kazi zako kwa walengwa walio mahsusi na kujua hao vionjo vyao.
Umemtolea mfano Chris Brown...kwa taarifa yako Chris Brown si msanii pekee mwenye mafanikio Marekani.
Wapo na wengine wengi tu walofanikiwa kwa kujifanyia mambo kivyao bila kuiga iga kwa wasanii wengine.
Na kwa vile tu jambo fulani limefanikiwa kwa mtu A hiyo haina maana kuwa litafanikiwa kwa mtu B.
Kwa ufupi, sanaa ni tasnia iliyo changamani ambayo mafanikio yake hutokana na mambo na sababu nyingi, na si kuigana igana tu.
Hakuna playbook ya sanaa.