Kwanini wasanii wa Bongo hawajui kujieleza?

Kwanini wasanii wa Bongo hawajui kujieleza?

Kujielezea kipaji ..
Hapana kujieleza ni practice.
Kazini boss wangu ametengeneza podium kila siku tuna safety topic ambapo mmoja huwa anajieleza mbele ya audience ya managers ambao wanweza kuwa 8
Mpaka managers nao wanajieleza Na kuna uhuru wa kupongezana Na kukosoana. Mimi sikuwa mpenzi wa kuongea mbele za watu but now am getting there.
 
Tatizo si kujieleza tu. Hata ng'ombe anajieleza.

Tatizo ni kujieleza vizuri, kwa mpangilio, ukaeleweka.
Lakin mkuu si mmesema HAWAJUI KUJIELEZA, means sio tu kujieleza Vizuri, but Hawajui KUJIELEZA sio?. Halafu umesema kujieleza ni Self expression..hivyo kwa asiye muelewa means hana knowledge ya kinachoelezwa na mzungumzaji , hayo mambo yakuto maliza sentence may be kwa audience lengwa huelewa...kama sio mlengwa wa maelezo ya mzungumzaji utaishia kufanya DISCOURSE ANALYSIS na Pragmatic kumjaji kuwa hajui kujieleza....
 
Unapoandika "mmesema" ushanijumuisha na wengine.

Sipendi kujumuishwa hivyo.

Jikite kwenye nilichoandika mimi.

Usiniletee habari za "mmesema".

Ukijua kuhesabu moja mpaka mbili lakini usijue zaidi unajua kuhesabu au hujui?

Ukijua kusoma a na b usijue zaidi, unajua kusoma au hujui?
 
Kiranga,
Hahahahaha Povu lanin mkuu....labda unatatizo sawa na hao wasanii

Kwanza ujue hii ni thread inayochangiwa maoni na watu wengi. Nimesema "mmesha" kwa sababu kuu Moja umeunga mkono hoja ya mleta topic, hivyo wewe na mleta topic pamoja na wengine wanao unga mkono hoja hii nimewaweka group Moja kwasababu ya wazo lenu Moja. Kama hutaki kujuishwa Fanya kitu hiki, either uhakikishe wazo lako ni lako halijaungwa mkono na mwingine or hujaunga mkono hoja ya mwingine ili uwe peke yako katika kukosolewa hiyo tu haitoshi pia hakikisha topic hiyo ni yako pekee..
FACT KUPANIC HARAKA NI TATIZO LA KISAIKOLOJIA
 
Wewe hata nikipiga chafya kwa reflex action utaona povu.

Kwa sababu huwezi mjadala wa mikikimikiki.

Hujajibu maswali niliyouliza na uliyojibu sijauliza.
 
Mara nyingi matatizo katika kujieleza yanaonesha matatizo katika kufikiri.

Hususan, kukosa uwezo wa kufikiri kwa kina, au kutojali habari za kufikiri kwa kina.

Sifikiri kwamba hatuna uwezo wa kufikiri kwa kina. Hakuna sababu ya kunifanya nikubali hilo. Naona kama tumekubali utamaduni wa kutofikiri kwa kina.

Wengi tunatakiwa kubadilika kwa angalau haya.

1. Kufikiri kabla ya kusema. Ni rahisi kuharibu kujieleza kama tunasema sana bila kufikiri.

2. Kujali wengine sana. Ukijali wengine, utaweza kufikiri sana jinsi ya kujieleza mpaka wakuelewe vizuri. Kwa mfano, ukiongea na mtoto, ukimjali, utataka kuongea kwa njia ambayo mtoto atakuelewa. Ukimuelezea mtoto kwa lugha ambayo imekaa kikubwa utamchanganya. Mara nyingi makosa katika kujieleza yanaonesha mtu anayejieleza kutojali wanaomsikiliza.

3.Kujifunza kujieleza kutoka kwa watu maarufu waliofanikiwa kuweza kujieleza kwa umakini. Kuna watu wana kipaji hiki. Ni muhimu kuwasoma.

4. Kusoma vitabu. Kusoma kunajenga mawazo na kupanua wigo. Kunatupa kanuni za msingi za kufuatilia na jinsi ya kuzihakiki.

5. Kutotaka kutafsiriwa vibaya. Ukiwa hutaki kutafsiriwa vibaya utaweka juhudi zaidi kujieleza vizuri. Kwa mfano, hata ukisema kitu, halafu ukagundua hakijamalizika au kina utata, utarudia ili kufanya masahihisho au maongezo. Hiki ni kitu ambacho wengi wetu hatufanyi.

6. Kumalizia sentensi. Jaribu kumalizia kila sentensi na wazo. Usidhani tu kila mtu anaelewa unachosema na anaweza kumalizia.

7. Kuelezea mambo kutoka mwanzo mpaka mwisho. Tuepuke kuanza kuelezea habari kutoka kati au bila hitimisho.

8. Kuuliza kama umeeleweka au kama kuna maswali. Mara nyingi mawasiliano ni kitu chenye utata, kwa sababu, hujui mwingine unayewasiliana naye ana uwezo gani, kaelewa nini, hajaelewa nini n.k. Hivyo, ni muhimu kumuachia nafasi na yeye ajieleze, kumpa muda wa kuuliza maswali na kuweza kuhakiki kwamba wote mnaelewana. Kuna watu wakianza kuongea wanataka kuongea wao tu bila kuwapa nafasi wengine.

9. Kuangalia "non verbal communication". Mambo mengine hayasemwi, unaweza kuona mtu anaangalia saa yake wakati mna maongezi ukajua labda unamchelewesha. Hapo unaweza kumpa nafasi ya kuaga kwa kumuuliza "Una miadi sehemu nini?"

10. Kusikiliza si tu kinachosemwa, bali hata ya kilichoachwa kusemwa. Ukimuuliza mtu swali moja, halafu asijibu hilo swali na kujibu lingine, unatakiwa kujua ama hajaelewa swali au anataka kuficha na kutojibu. Unaweza kuamua kuuliza swali tena ili kumpa nafasi ajibu, hususan kama unaona hajaelewa, au kuacha kuuliza kwa kuona anakwepa kujibu.
sawa kaka nimeona amri kumi hizo
 
Wewe hata nikipiga chafya kwa reflex action utaona povu.

Kwa sababu huwezi mjadala wa mikikimikiki.

Hujajibu maswali niliyouliza na uliyojibu sijauliza.
Wala Sina shida kujisifu kwako kusiko na logic hapa maana ni udhaifu pia....sijakujibu kwasababu maswali yako yamesha jijibu yenyewe..😂 na sjakatazwa kueleza nisiyo ulizwa
 
Wala Sina shida kujisifu kwako kusiko na logic hapa maana ni udhaifu pia....sijakujibu kwasababu maswali yako yamesha jijibu yenyewe..[emoji23] na sjakatazwa kueleza nisiyo ulizwa
Una shida, ndiyo maana unaninukuu.

Usingekuwa nanshida ungenipotezea tu.
 
Inawezekana upo sahihi kwa upande wako...Ila kwa upande wangu kukupotezea hiyo ndio itakuwa shida..
Kwa sababu huwezi kuacha kunifikiria kama binti asivyomsahau mwanamme aliyemtoa bikira.

Straight to ignore list.
 
Back
Top Bottom