Ushawahi muona DAVIDO au burna anavaa nguo yenye brand asiyo itangaza?
Ila wanaendesha magari ambayo wao sio mabalozi.
Wanaendesha bugatti, bentley na wanazitangaza bila wao kuwa mabalozi wa hizo kampuni.
Wanatumia simu za iphone na samsung na watu wengine wanawaona nazo. Je unataka kusema wao ni mabalozi wa hizo kampuni?
Hizo Nike, Adiddas zimeshakuwa kubwa kiasi kwamba hata bila Diamond, zenyewe zinauzika. Ndo maana wanapenda kuvaa brand kubwa. Watu maarufu huko ulaya wanavaa saa za Rolex bila kuwa mabalozi.
Kuna muda unafika unahitaji kuwa na brand kubwa bila wewe kuwa balozi. Yani kiufupi brand ni kubwa kuliko msanii.
Kwahiyo unataka diamond atumie simu ya itel sababu ni balozi, aache kutumia iphone. Aache kutumia V8, Escalade na Roll Royce kwa sababu sio balozi wa hizo kampuni.
CR7 anamiliki Bugatti, McLaren, Maserati, Audi, BMW, Bentley, Ferrari, Range, Chevrolet, Mercedes, Roll Royce na huwa anapiga nazo picha.
NB: Huwezi kushindana na Ukubwa