kwanini wasichana wako hivi?

kwanini wasichana wako hivi?

nestory

Member
Joined
Jul 21, 2008
Posts
22
Reaction score
0
utakuta wakati mahitaji yake yote anayatoa kwako,anakua mpole mkarim na pia mwenye busara.lakini akishapata chanzo chochote cha kumpatia fedha anabadirika.au hiyo ni dalili kua hakua anakupenda? lakini mbona asilimia kubwa about 98%, yani almost wote wako hivyo.naomba mnisaidie wana JF kwenye hili,kwamba ukweli uko wapi?
 
Ni mtizamo tu wajameni.
Mtu akiwa hana kitu hata confidence humwishia.Huwa kama mtumwa. Akijiweza, confidence huongezeka, huwa na uthubutu wa kuchangia mazungumzo, huweza kuelezea msimamo wake hata kama uko tofauti na wako.Hilo kwa vyovyote litakushtua utaanza kuona ana kiburi kumbe ni mabadiliko tu ya kawaida ya mwanadamu.Ushasikia mbinu za kumjengea mtu uwezo wa kujiamini? Unadhani step ya kwanza ni ipi? Ni uwezo wa kujimudu.
Fundisho: Kama unataka kumsaidia mtu na unataka abakie mtumwa milele basi usimsaidie maana kubakia mtumwa milele haitawezekana.
 
women are like that bana....
zoea tu....
ni swala la muda hilo
 
Naomba nikusahihishe kidogo si wote wako hivyo labda hao wachache uliokutana nao wako hivyo. Unajua fedha ni kitu kibaya sana na ni kizuri pia. Fedha yaweza kusababisha mtu akabadilika vibaya mno ukashindwa kuelewa. ukweli kila mtu anao moyoni mwake.
 
Ni mtizamo tu wajameni.
Mtu akiwa hana kitu hata confidence humwishia.Huwa kama mtumwa. Akijiweza, confidence huongezeka, huwa na uthubutu wa kuchangia mazungumzo, huweza kuelezea msimamo wake hata kama uko tofauti na wako.Hilo kwa vyovyote litakushtua utaanza kuona ana kiburi kumbe ni mabadiliko tu ya kawaida ya mwanadamu.Ushasikia mbinu za kumjengea mtu uwezo wa kujiamini? Unadhani step ya kwanza ni ipi? Ni uwezo wa kujimudu.
Fundisho: Kama unataka kumsaidia mtu na unataka abakie mtumwa milele basi usimsaidie maana kubakia mtumwa milele haitawezekana.

"Mtumikie Karifi Upate Mradi Wako".... Hii iko kwa wanawake tu au hata Wanaume??
 
hata wanaume wanapokua na shida na inabd kumtegemea mwanamke wanakua wapole sana, wasikivu na hujua kuonyesha upendo. lakini ikimchangamkia tu anakua mwingine
 
Kwa hiyo hili suala liko pande zote... Kwa wanawake na wanaume...
 
Nina gf wangu, tangu anaingia advance level,anafanya mtihani mpaka mda wa

kusubiri matokeo alikua ni mtu mwenye nyodo sana, (offcourse mi nafanya kazi

lakini si yenye kipato kikubwa saaaaaaaaaaaaaaaaaana) ,sasa baada ya

matokeo akawa ameferi,yaani amepata matokeo ambayo ayawezi kumfikisha

chuo, sasa naona upendo umezidi kupita kiasi mpaka naona kero,maana kira saa

atataka muwasiliane na vitu vingine vingi tu. mi nafkiri huu unaweza ukawa

mfano wa utata ambao mkuu wangu anawasilisha KWA WANA JF, sasa mnasemaje kwa kesi kama hii?
 
Women ni opportunist wazuri sana....normally wanamheshimu mtu anayewafanya maisha yao yawe rahisi. Ikiwa vinginevyo lazima aonyeshe true colors zake.
 
Bana wee tukumbuke hawa waliumbwa kutokana na ubavu wetu kwahiyo usishangae wakiwa namna hiyo,ndio inavyotakiwa wawe vizazi na vizazi vumilia tu majukumu.
 
Women ni opportunist wazuri sana....normally wanamheshimu mtu anayewafanya maisha yao yawe rahisi. Ikiwa vinginevyo lazima aonyeshe true colors zake.
unfortunately this applies both to men and women!!

wanaume watawaongelea wanawake kwa kuwa wanauzoefu nao na wanawake tutawaongelea wanaume kwa kuwa pia tuna experience na nyie!!!
 
Ni tabia watu wanazo; wake kwa waume! labda hapa ingekuwa kwa nini mpenzi wako yuko hivyo; ume generalise na kwa kufanya hivyo hukuwatendea haki Mama zetu (ebo walikuwa wasichana hapo kabla!)
 
Ni mtizamo tu wajameni.
Mtu akiwa hana kitu hata confidence humwishia.Huwa kama mtumwa. Akijiweza, confidence huongezeka, huwa na uthubutu wa kuchangia mazungumzo, huweza kuelezea msimamo wake hata kama uko tofauti na wako.Hilo kwa vyovyote litakushtua utaanza kuona ana kiburi kumbe ni mabadiliko tu ya kawaida ya mwanadamu.Ushasikia mbinu za kumjengea mtu uwezo wa kujiamini? Unadhani step ya kwanza ni ipi? Ni uwezo wa kujimudu.
Fundisho: Kama unataka kumsaidia mtu na unataka abakie mtumwa milele basi usimsaidie maana kubakia mtumwa milele haitawezekana.

Shoga hilo fundisho kama mtu hajakuelewa basi ana ubishi wa kuzaliwa nao.
 
Ni tabia watu wanazo; wake kwa waume! labda hapa ingekuwa kwa nini mpenzi wako yuko hivyo; ume generalise na kwa kufanya hivyo hukuwatendea haki Mama zetu (ebo walikuwa wasichana hapo kabla!)

Wewe kaka umeongea points. Ungekuwa karibu! we acha tu.
 
Sio wote Nestrory wapo wengi na wapole ,wavumilivu na wenye moyo wa subira ukikuta wa hivyo huyo alikuwa anatafuta kivuli cha kupumzika jua lipungue kisha aendelee na safari yake
 
Back
Top Bottom