Kwanini Wasichana wengi wanaona wana haki ya kupewa Salamu na sio kutoa?

Kwanini Wasichana wengi wanaona wana haki ya kupewa Salamu na sio kutoa?

RoadLofa

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
1,509
Reaction score
3,313
Ivi Kwanini? Wasichana Wengi Uwa Wanajiona Wana Haki ya Kupewa Salamu na Sio Kutoa?

images.jpeg

Habarini wanajamii Forums nimekuwa na kitu kinanishangaza sana tangu utoto hadi sasa kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu , imekuwa kawaida kwa jamii ya kiafrica mvulana kumshobokea mtoto wa kike yaani kuanza kumpa salamu ata kama kakukuta sehemu , maana navyojua mtu anapokukuta sehemu yeye ndo anatakiwa kukupa salamu na sio yeye afike na kukaa kimya kisha wewe ndo umpe salamu

Hii kitu nimeishuhudia mara kwa mara tangu nizaliwe hadi sasa , hii kitu imekuwa ikinikuta mara kwa mara labda nipo kwenye bus naenda mkoa fulani nimekaa zangu kwenye seat anakuja msichana seat ya pembeni yangu anafika na kukaa bila ata salamu aisee uwa nashindwa kumuanza kumsalimia au kwa kumuonea aibu nampa hi halafu nakausha, hii ishu pia kwenye usafiri wa umma uwa inatokea unakuta nimewahi nimekaa zangu ndani ya gari mara anaingia sister duh anakuja anakaa pembeni yangu kimya kimya ata asalimii uwa sijui namuonaje kuna muda uwa napiga kimya hadi safari napoishia maana uwa naona kumshobokea mtu kumsalimia aliyekukuta ni kuuaibisha ukoo wangu na mimi pia.

Sijui kwa wengine kama hii hali wanaishuhudia ila nimekuwa naishuhudia ata mitaani na vyuoni ni ivyo ivyo binti anaweza kuwakuta mmekaa na asiwasalimie au akasalimia kwa majina kadhaa na sio wote 😀😀sijui uwa ni kitu gani kinawasumbua, ila kwa mimi nachoamini iyo ni tabia iliyojengeka kwao kutokana na wavulana tunavyowatreat wasichana tunajishusha sana mbele ya wasichana hadi wanatudharau na wanaona wana haki ya kila kitu kutoka kwetu hadi salamu 😀😀

Ningependa kusikia maoni ya wasichana na wanaume kuhusu ili suala ...
 
sio salamuu tuuu
Vitu vingiii, mfano kupenda kupewa maua, kutolewa outing, zawadi lukuki..genye etc,
Hata mara moja hawezi enda nyumba ya kulala wageni akalipia yeye .... hakyii ys shwetaniii ka nasema uongooo hahaaa
Ndio hivyoo kwa jinsia ya kike, mara nyingi huwa inapokea na kukuza mambo/vitu mbali mbaliii ----its a psychological in-born

ukiona wa tofauti ni wachache sanaa
 
Hata sipo kukosoa uumbaji wa Pungu ila wengi ni tabia zao tu za kipuuzi
 
Kuna siku mke wangu yupo kwao ananilalamikia eti kwanini sjamtafuta siku hiyo ilibidi nimwambie kuwa nyie wanawake muda mwingine muwe mnatuonea huruma sie wanaume kila kitu nikufanyie na simu tu unataka niwe nakupigia kila siku,hata kupiga tu simu huwez toka siku hyo kabadilika akiona sjampigia ananipigia

Mimi demu akinikuta sehemu kama hajanisalimia na mimi napiga kimya haijalishi ni mzuri kiasi gani
 
Sipendi watu wanaopenda penda salamu utadhani chakula khaa hadi kwenye daldala napo unataka usalimiwe,utasalimiwa na wangapi sasa na utasalimia wangapi maana wanaingia na kutoka. Tafuteni pesa wakuu muache kujali vitu vidogo vidogo
 
Huwa sisalimii maslay queen kabisa hasa njiani,,

Leo nimeingia ofisi fulani nimekuta wasichana wengi wanaogopa kuingia Kwenye ofisi ninayoenda mimi nikapita katikati yao nikaingia ofisini nilivotoka wakanisalimia wenyewe kwa heshima na kuomba utaratibu bila hiyana nikaelekeza nikapita zangu.
 
Sipendi watu wanaopenda penda salamu utadhani chakula khaa hadi kwenye daldala napo unataka usalimiwe,utasalimiwa na wangapi sasa na utasalimia wangapi maana wanaingia na kutoka. Tafuteni pesa wakuu muache kujali vitu vidogo vidogo

Sipendi watu wanaopenda penda salamu utadhani chakula khaa hadi kwenye daldala napo unataka usalimiwe,utasalimiwa na wangapi sasa na utasalimia wangapi maana wanaingia na kutoka. Tafuteni pesa wakuu muache kujali vitu vidogo vidogo
Wewe utakuwa mhusika, salimia watu bhana,
 
Wasichana/wanawake wanaofanya kazi taasisi za kifedha, hasa benki wanaweza kuwa wanaongoza kwa kiburi cha kutosalimia.......... Wengi wanajiona wameyapatia maisha..... they are so stupid!
I rest my case! Nimetupa jiwe gizani. Nasubiri atakayegugumia kwa maumivu, ili nimjue niliyemtungua.......
 
Back
Top Bottom