Kwanini Watanganyika wanafunguliwa mashtaka mabaya mabaya awamu ya sita?

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,490
Reaction score
38,302
Heshima sana wanajamvi.

Nijikite katika mada moja kwa moja.

Tangu awamu ya sita ianze kuitawala Tanganyika timeshuhudia Watanganyika wakipewa kesi kubwa kubwa.

Awamu ya sita inaongozwa na Mzanzibar hatujawahi kusikia au kuona akiwabambikia Wazanzibari wenzake kesi za uhaini au kesi za ugaidi.

Imekuwa ni rahisi sana kumbambikia Mbowe kesi ya ugaidi kwakuwa ni Mtanganyika.

Imekuwa ni jambo la kawaida kabisa kumbambikia Lissu kesi ya uhaini kwasababu ni Mtanganyika.

Kuwa Mtanganyika awamu hii ni hasara kubwa na laana kuu.
 
Nchi inaongozwa na mtu mwenye akili ndogo na wafuasi wake nao wamekuwa na akili ndogo na hayo ndio matokeo yake , kiti cha Rais sio kiti ambacho hata barmaid anaweza kukikalia , tumekidhalilisha sana kiti cha rais
 
Sheria inafuata mkondo wake.Mlikuwa mnafurahi mkisikia mashekhe wako ndani kwa kesi za ugaidi.Na masheikh hao wakiwa ni watanganyika.
 
Kwa sababu watanganyika nyie wenyewe mmemtengenezea mazingira huyo mzanzibar kuitawala Tanganyika jinsi anavyotaka huku akiwalipa fadhila kwa kuwapeni uhuru wa nyie kufanya upigaji/ufisadi.

Miaka miwili ya mwanzo Samia aliliongoza hili taifa kwa nidhamu ya hali ya juu sana mpaka pale alipoona uchawa na kujipendekeza ni hulka ya watanganyika na wala hamna uzalendo wowote, ndio akaamua kuanza kuwaburuza tu na yeyote anayemletea disturbance anapewa kesi nzito ya kumpoteza.
 
Mh Lisuu akirudi jukwaani atumie hii silaha/hoja ya Tanganyika, aseme kabisa watanganyika wanateswa na mzanzibari.

Aulize wananchi je wapo tayari kutetea Tanganyika yao au waendelee kuburuzwa na Mzanzibari.
 
Makamanda uchwara mmna hasira kwa sababu limwenyekiti lenu limeswekwa lupango ha ha ha😁
Hapana ebu tuwe na roho ya kibinadamu kidogo.

Kati ya watu wanampinga Lissu mimi nimo kila mmoja anajua misimamo yangu.

Pamoja na kumpinga sipendi kuona akionewa,akibambikiwa kesi za uongo,sipendi kuona rasilimali zetu zikichezewa kwasababu ambazo hazina mashiko.
 
Hakuna mwanaccm mwenye roho ya kibinadamu
 
Hakuna mwanaccm mwenye roho ya kibinadamu
Kabisa hakuna...!!

Mimi huwa naamini ccm ndio adui wa kwanza wa taifa hili yaani kwa maana nyingine wana ccm ndio wahaini wenyewe na sio vinginevyo.

Angalia kwanza wanavyojipendekeza kwa huyu mzanzibar sio kwamba eti wanampenda kwa uzalendo/uchapakazi wake, bali ni kwa udhaifu wake ambao umepelekea wao kuwa na uhuru wa kuliibia hili taifa na hawaogopi kuua mtu ambaye yuko kinyume na wao, sasa hao ni binadamu wa kawaida kweli? Si ni zaidi ya wanyama?
 
Ni katika awamu hii ya 6 tumeona na kushuhudia Wazanzibari wakitengewa 21% ya ajira katika taasisi zote za muungano.

Ukweli mchungu nimeamua kuukana uraia wa Tanzania (Mtanganyika) sasa mimi Ngongo ni Mzanzibar.
Wajinga sana na kamkoa kao hako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…