Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

Nilishangaa kukutana na wabongo Mongolia mjini Ulaanbaatar, tulipiga sana stori jioni tuliyopanga tukutane

Yaani mkikutana kwa wenzetu mnakuwa karibu kama ndugu wa familia moja
Miaka fulani tuliendaga tel aviv
Huko tulikutana na watanzania waliyokaa muda mrefu sana huko
Kuna mzee mmoja huko alinikaribisha
Kwake somebody gasper matunda,aliniambia alipokuwa bongo
Alikuwa tanzania elimu supplies
Sema amejikita huko na yuko vzr alikuwa

Ova
 
Tanzania ni nchi bora sana duniani. Ukisafiri mikoani inatosha kupata kile ambacho ungekipata duniani kote.

Pia teknolijia ya sasa unaweza kwenda popote, kuonge na yeyote duniani ukiwa kijijini sitimbi na internet. Hata kuagizs chochote.
Kama huridhiki na nchi yako utakuwa unatamani kusafirisafiri hovyo.
Majibu ya kiongozi wa Chama haya
 
1.Pesa
2.Hobby

Nadhani hizi ndizo sababu za msingi. Wenye pesa hawana hobby, wenye hobby hawana pesa.

Nilimwambia bwana mmoja katika kupiga stori kuwa nikiwa na miaka 27 nilishasafiri nchi 7 za humu humu kwetu Afrika, akaniuliza ulikuwa unasafiri na nani nikamwambia na my-then Boy friend. Akanijibu tu kuwa definitely huyo mtu hakuwa mTz. Na ni kweli.
 
Mwanamke aitwaye Cassandra de Pecol kutoka Connecticut, alifanikisha ndoto yake ya kutembelea nchi zote duniani, 193,
akiwa na umri wa miaka ishirini na saba.

Mpaka anafikisha miaka 18, Canada ndiyo nchi pekee aliyokuwa amefika, tena, ni kwa vile mama yake anatokea huko. Sababu kubwa iliyomfanya asisafiri akiwa mdogo ni uwezo mdogo wa kifedha.

Kufanikiwa kwake kuzitembelea nchi 193 ni jitihada zake binafsi. Anavyoonekana si tajiri, ila anapenda kusafiri. Lakini kuna Watanzania ambao pengine wana uwezo mkubwa kifedha kumzidi yeye lakini bado hawasafiri.

Ukizilinganisha nchi za Afrika Mashariki, hasa Kenya, Uganda, na Rwanda, Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kutokusafiri kwenda nchi zingine. Kwa nini hivyo?

1. Umaskini?

2. Lugha?

3. Ugumu wa upatikanaji wa passport?

4. Ushamba?

5. Utamaduni?

Sababu ni nini?
3.ugumu wa kupata passport hasa ukiwa unatokea kigoma
 
Mimi baada ya kujifunza Na kuelewa umuhimu wa kusafiri kiafya nimeazimia kuanzia kupanga na kusafiri kwa kuanzia maeneo ambayo naweza kuya -access Kwa urahisi.

Matharani unaweza kuanzia kwa level ya Wilaya , mikoa , nchi jirani , za mbali kisha ng’ambo.

Kwa kadiri ya uwezo wako.

Walau uanze karibu.

Imagine hata mbuga za wanyama watu hawaendi?!
 
Kwa miaka mingi sana nilikuwa sipendi kusafiri isipokuwa pale ilipolazimu tu labda kikazi au kijamii.

Lakini kwa neema ya Mwenyezi Mungu nimefunguliwa, nimejifunza nimepata ufahamu sasa hivi sio yule tena.

Ujinga tupa kule.

Nimewekwa huru kweli kweli.
 
Back
Top Bottom