Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

Mimi baada ya kujifunza Na kuelewa umuhimu wa kusafiri kiafya nimeazimia kuanzia kupanga na kusafiri kwa kuanzia maeneo ambayo naweza kuya -access Kwa urahisi.

Matharani unaweza kuanzia kwa level ya Wilaya , mikoa , nchi jirani , za mbali kisha ng’ambo.

Kwa kadiri ya uwezo wako.

Walau uanze karibu.

Imagine hata mbuga za wanyama watu hawaendi?!
👏👏👏✅
 
Wengine watakuambia hawahitaji kwenda kwenye mbuga za wanyama kwa sababu teknolojia imewarahisishia🤣🤣🤣

Kwamba kwa video vivutio vilivyopo kwenye mbuga za wanyama🤣🤣🤣
 
Mwanamke aitwaye Cassandra de Pecol kutoka Connecticut, alifanikisha ndoto yake ya kutembelea nchi zote duniani, 193,
akiwa na umri wa miaka ishirini na saba.

Mpaka anafikisha miaka 18, Canada ndiyo nchi pekee aliyokuwa amefika, tena, ni kwa vile mama yake anatokea huko. Sababu kubwa iliyomfanya asisafiri akiwa mdogo ni uwezo mdogo wa kifedha.

Kufanikiwa kwake kuzitembelea nchi 193 ni jitihada zake binafsi. Anavyoonekana si tajiri, ila anapenda kusafiri. Lakini kuna Watanzania ambao pengine wana uwezo mkubwa kifedha kumzidi yeye lakini bado hawasafiri.

Ukizilinganisha nchi za Afrika Mashariki, hasa Kenya, Uganda, na Rwanda, Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kutokusafiri kwenda nchi zingine. Kwa nini hivyo?

1. Umaskini?

2. Lugha?

3. Ugumu wa upatikanaji wa passport?

4. Ushamba?

5. Utamaduni?

Sababu ni nini?
1.

Siyo watz tu. Duniani kote ipo hivo
 
Iko hivi ukiangalia wazungu wengi ni watu ambao wanafanya sana saving hata wenye vipato vya kawaida.

Wanaweza saving kwakuwa kwanza kiwango cha utegemezi kwao ni kidogo sana. Yani utakuta baba na mama wana mtoto mmoja au hawana na hamna mtu anaewaomba hela.

Hakuna sijui michango ya ukoo, sijui mtoto wa mjomba ada shule, mara rafiki anaoa, mara bibi anaumwa n.k

Birth control imesaidia wenzetu sana. Sisi huku mtu ana ndugu zaidi ya laki na akipata tu ka ajira ka kulipwa laki saba basi kila mtu anamtolea macho, vizinga visivyoisha.

Huyo mtu ata save sangapi ili aweze kutembelea nchi mbalimbali?

Kingine kwa wenzetu wa nje huko wengi wanakula generational wealth. Yani mtu anazaliwa anakuta familia iko well-off kuanzia vizazi kadhaa vilivyopita. So yeye anaendeleza kutengeneza hela tu na future ya kizazi chake so mambo kama kusafiri ni kawaida tu.

Chamwisho ni nchi yetu hii ina mifumo ya ajabu sana. Mtu kumiliki passport tu inaonekana kama vile ni jambo la ajabu sana. Ukienda uhamiaji kutaka passport inakuwa ni mchakato mgumu utadhani unataka kwenda mbinguni.

Nchi za wenzetu kuwa na passport ni kawaida na kila raia anayo kama document muhimu. Hapa kwetu passport inachukuliwa tofauti sijui kwanini CCM hawataki raia wamiliki passport?
Kumbe ,wazungu hawana hizo Habari za MICHANGO YA UKOO,??

HEBU Tupe SoMo kidogo

Kwa maelezo hayo nimeona, Generational wealth plan ,ni Bora mara maelfu kuliko hizo Habari za MICHANGO YA UKOO
 
watanzania wanapenda sana kusafiri ila uhamiaji passport wanaona kama dhahabu kumpa mtu
 
Tanzania nchi ya amani ambapo ukiweka jitihada kidogo tu maisha yanakunyookea. Sababu kuu ni watu kuridhika na nchi yao na kutokuwa na sababu ya kuhangaika. Hao wakenya, Rwanda na Burundi wana dhiki kali kwenye nchi zao hivyo hawasafiri kwa kupenda.
Hata watalii wanaokuja kutalii Tanzania nao pia ni kwa sababu ya shida kwenye nchi zao?

Mkuu, wewe umeshawahi kutembelea hata hifadhi za Taifa hapa Tanzania?
 
Kwanza nimekulia kwenye kijiji kinachopakana na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro. Hifadhi zote za kaskazini nimezivuruga. Nisingefaulu darasa la saba ningeenda kusomea Tour Guide. Una swali lingine?
 
Swali la nyongeza: kwa kusema kuwa umezivuruga unamaanisha kuwa umezitembelea kama mtalii au ilitokea tu kupita humo kama msafiri?
 
Yote mawili. Kupita na kuzitembelea. Nikiwa mwanafunzi nimetembelea hizo hifadhi mara kadhaa. Huku ukubwani pia nimetembelea kreta Ngorongoro mara 2. Wewe ulishawahi tembelea hifadhi ipi?
 
Tanzania ni nchi bora sana duniani. Ukisafiri mikoani inatosha kupata kile ambacho ungekipata duniani kote.

Pia teknolijia ya sasa unaweza kwenda popote, kuonge na yeyote duniani ukiwa kijijini sitimbi na internet. Hata kuagizs chochote.

Kama huridhiki na nchi yako utakuwa unatamani kusafirisafiri hovyo.
Du na wewe kama Huna cha kuchangia si unasoma tu mkuu!!! Kutembea ni raha sana hata nchi zinazoizunguka bongo sio inatosha...
 
Mwanamke aitwaye Cassandra de Pecol kutoka Connecticut, alifanikisha ndoto yake ya kutembelea nchi zote duniani, 193,
akiwa na umri wa miaka ishirini na saba.

Mpaka anafikisha miaka 18, Canada ndiyo nchi pekee aliyokuwa amefika, tena, ni kwa vile mama yake anatokea huko. Sababu kubwa iliyomfanya asisafiri akiwa mdogo ni uwezo mdogo wa kifedha.

Kufanikiwa kwake kuzitembelea nchi 193 ni jitihada zake binafsi. Anavyoonekana si tajiri, ila anapenda kusafiri. Lakini kuna Watanzania ambao pengine wana uwezo mkubwa kifedha kumzidi yeye lakini bado hawasafiri.

Ukizilinganisha nchi za Afrika Mashariki, hasa Kenya, Uganda, na Rwanda, Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kutokusafiri kwenda nchi zingine. Kwa nini hivyo?

1. Umaskini?

2. Lugha?

3. Ugumu wa upatikanaji wa passport?

4. Ushamba?

5. Utamaduni?

Sababu ni nini?
na hata wakisafiri ukikutana nao usiwaamini kwakweli, wamenitapeli mara mbili
utasikia bro nisaidie dola mia tatu hapo kuna vitu ninunue nikirudi bongo tu nakuwekea kwa akaunti,
akirudi bongo haweki , hata ukimchek anakua haeleweki sio poa
ishu nyingine ni lugha, lugha si English peke yake, hata French, spanish n.k lakini wengi hawajui, hivyo wanaona aibu kusafiri kwa sababu hawana uhakika wa lugha ya kuzungumza
atleast wafanyabiashara wanasafiri sababu pesa inawapa confidence wanaweza kuweka hata translator
Lakini all in all Tanzania sisi bado, tuko wenyewe kwetu hatutaki kutoka lakini hiyo confidence sasa,[emoji38][emoji38], utafikiri tumeyaona yote ya Dunia
 
Kusafiri ni muhimu. Jiwekee mpango wa kusafiri hata kama ni mara moja kwa mwaka.
 
Attachments

  • #Umuhimu_wa_kusafiri(720p).mp4
    39.2 MB
Iko hivi ukiangalia wazungu wengi ni watu ambao wanafanya sana saving hata wenye vipato vya kawaida.

Wanaweza saving kwakuwa kwanza kiwango cha utegemezi kwao ni kidogo sana. Yani utakuta baba na mama wana mtoto mmoja au hawana na hamna mtu anaewaomba hela.

Hakuna sijui michango ya ukoo, sijui mtoto wa mjomba ada shule, mara rafiki anaoa, mara bibi anaumwa n.k

Birth control imesaidia wenzetu sana. Sisi huku mtu ana ndugu zaidi ya laki na akipata tu ka ajira ka kulipwa laki saba basi kila mtu anamtolea macho, vizinga visivyoisha.

Huyo mtu ata save sangapi ili aweze kutembelea nchi mbalimbali?

Kingine kwa wenzetu wa nje huko wengi wanakula generational wealth. Yani mtu anazaliwa anakuta familia iko well-off kuanzia vizazi kadhaa vilivyopita. So yeye anaendeleza kutengeneza hela tu na future ya kizazi chake so mambo kama kusafiri ni kawaida tu.

Chamwisho ni nchi yetu hii ina mifumo ya ajabu sana. Mtu kumiliki passport tu inaonekana kama vile ni jambo la ajabu sana. Ukienda uhamiaji kutaka passport inakuwa ni mchakato mgumu utadhani unataka kwenda mbinguni.

Nchi za wenzetu kuwa na passport ni kawaida na kila raia anayo kama document muhimu. Hapa kwetu passport inachukuliwa tofauti sijui kwanini CCM hawataki raia wamiliki passport?
CCM wameharibu maisha ya vijana wengi sana, ujira wa elfu saba kwa siku umesababisha ongezeko la MACHAWA
 
Sikiliza wasemavyo wataalam kuhusu umuhimu wa kusafiri.
 
Attachments

  • Expert_Advice__The_Health_Benefits_of_Traveling(720p).mp4
    37.4 MB
Back
Top Bottom