Kwanini Watanzania hawazichangamkii Toyota Mark X Vio

Kwanini Watanzania hawazichangamkii Toyota Mark X Vio

Nduka

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2008
Posts
8,553
Reaction score
2,380
Hii gari nimeipenda sana ilivyo na nafasi ndani, siti zake za nyuma zinaweza kulala kuongeza nafasi ya mizigo. Bei zake ni za kizalendo sana, nadhani kwa class yake ni gari ya bei nafuu kuliko zote. Injini ni 2.4 na inakuhakikishia power na durability. Kwanini wabongo hawajazichangamkia sana?

toyota_mark-x-zio_2007_photos_1_b.jpeg

SO FAR

1/ Watu hawapendi muonekano wake - imekaa kama zile gari za kubebea maiti
2/ Ukubwa wa injini
3/ Bei - haina uhakika
4/ Ni gari ya chini ; barabara zetu ni mtihani

Bado napenda kujifunza kwanini wabongo hawajaipokea kivile? Nikiiona naona ni kama NADIA ambayo ilipapatikiwa sana hadi leo sokoni zinaenda tu.
 
Ina range kuanzia 11M (2007) hadi 14 (2009). Bei za kizalendo mno.
Hapo ukiwa unanunulia kwenye yard za hapa mjini?

Kama sio, jumlisha na gharama za kuileta kutoka ughaibuni pamoja na kodi za TRA
 
Hapo ukiwa unanunulia kwenye yard za hapa mjini?

Kama sio, jumlisha na gharama za kuileta kutoka ughaibuni pamoja na kodi za TRA
Hiyo ni kala kitu, unaweza kupata chini ya hapo ukiagiza plus kodi za TRA.
 
2.4 maana yake ni cc 2400 .wabongo wanataka gari ya cc 2000 iwe juu juu kama rav 4 na sio ndege ya ardhini.

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
Nadhani kwa mazingira ya barabara zetu ni sababu valid. Ila sasa huoni bei hapo ni nusu ya RAV4 na unapata nafasi kubwa ndani na engine power karibia sawa?
 
Ina range kuanzia 11M (2007) hadi 14 (2009). Bei za kizalendo mno.
Yaani wewe siyo mtu wa magari kabisa,unatamani tu wala hujui...hiyo gari inauzwaga M22 ktk showroom za hapa TZ na ukiagiza mwenyewe yamkini ukaikomboa kwa 17-18M
 
Yaani wewe siyo mtu wa magari kabisa,unatamani tu wala hujui...hiyo gari inauzwaga M22 ktk showroom za hapa TZ na ukiagiza mwenyewe yamkini ukaikomboa kwa 17-18M
Ndio tatizo la kuwa mtu wa magari, hapa mjini mnapigwa/mnapiga sana. Kuuza au kununua gari hiyo milioni 22 ni wizi wa mchana kweupe. Kama unataka ya 2007, nikupeleke sehemu wakuuzie kwa milioni 11 leo hii.
 
Back
Top Bottom