John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Je, unakwenda kununua gari ambalo ni mpya kabisa (brand new) kutoka kiwandani au gari ambalo tayari limetumika (used) ?1. Lengo kuu la safari ni kununua gari
2. Lengo la ziada ni kutalii, yaani, kuangalia nchi na miji ya wenzetu. Ndiyo maana ninatamani kupita nchi nyingi na maeneo mengi kadiri iwezekanavyo, kama usalama na bajeti itaruhusu. Ikishindikana kwa sababu mojawapo kati ya hizo mbili, nitafanya litakalowezekana.
Safari ya kwenda South Africa itaanzia Mwanza kwa ndege kupitia Dar Es Salaam hadi Johannesburg. Kutoka Johannesburg nitaenda hadi Pretoria kwa gari la abiria ambapo nitalala siku moja au mbili kwa ajili ya "kulichunguza" jiji. Kisha nitarejesha tena Johannesburg.
Gari natarajia kuchukulia Johannesburg au Durban. Itategemeana na nitakachokikuta maeneo tajwa.
Bila kujali kama gari nitachukulia Johannesburg au Durban, kufika Cape Town ni lazima. Safari kama hizo ni kwa wengi wetu, kwa hiyo nafasi ipatikanapo ni vizuri kuitumia vizuri. Safari ya "kuitafiti" South Africa itakahitimishwa Cape Town. Baada ya hapo, nitakuwa tayari kwa safari ya kurejea Mwanza.
Mpaka sasa, uwezekano uliopo ni kupita NAMIBIA na ZAMBIA, kwa kuzingatia ushauri wa wazoefu wengi.
Japo nimepanga kufika PRETORIA, JOHANNESBURG, DURBAN na CAPE TOWN, si SHERIA. Naweza kufanya adjustment kwa kupunguza au kuongeza miji nitakayofika. Lakini natamani zaidi kuongeza.
Ikitokea nitalazmika kupunguza, basi kipaumbele ni kufika DURBAN na CAPE TOWN. Bila kutia miguu yangu hayo majiji mawili, sitahesabu nimefika South Africa.
Kama unaenda kununua gari used nakushauri tena kwamba ufanye utafiti wako wa kina kuhusu suala hili la manunuzi ya gari kwa sababu kwa mujibu wa Sheria za nchi ya Afrika ya Kusini, ni kosa kisheria kwa mtu yoyote yule ambaye ni raia wa nchi za kigeni na ambaye Hana Viza halali ya kumruhusu kuishi nchini humo kununua gari lililotumika (mtumba) na kisha kuondoka nalo na kwenda (kulisafirisha) nje ya nchi hiyo. Jambo hili haliruhusiwi kisheria, labda kama Sheria hizo zimebadilishwa miaka hii. Biashara ya kuuza magari ya mtumba nje ya nchi hiyo ya South Africa imepigwa marufuku kabisa kisheria, labda kama utaenda kununua gari mpya kutoka kiwandani, hiyo inaruhusiwa.