Kwanini Watanzania wanahofia kupita Zimbabwe katika safari za Afrika Kusini?

Je, unakwenda kununua gari ambalo ni mpya kabisa (brand new) kutoka kiwandani au gari ambalo tayari limetumika (used) ?
Kama unaenda kununua gari used nakushauri tena kwamba ufanye utafiti wako wa kina kuhusu suala hili la manunuzi ya gari kwa sababu kwa mujibu wa Sheria za nchi ya Afrika ya Kusini, ni kosa kisheria kwa mtu yoyote yule ambaye ni raia wa nchi za kigeni na ambaye Hana Viza halali ya kumruhusu kuishi nchini humo kununua gari lililotumika (mtumba) na kisha kuondoka nalo na kwenda (kulisafirisha) nje ya nchi hiyo. Jambo hili haliruhusiwi kisheria, labda kama Sheria hizo zimebadilishwa miaka hii. Biashara ya kuuza magari ya mtumba nje ya nchi hiyo ya South Africa imepigwa marufuku kabisa kisheria, labda kama utaenda kununua gari mpya kutoka kiwandani, hiyo inaruhusiwa.
 
Msumbiji kukoje kiusalama?
 
La mtumba mkuu! Kuna Shuhuda za wadau wengi wanaodai waliyachukulia huko South Africa.
 
La mtumba mkuu! Kuna Shuhuda za wadau wengi wanaodai waliyachukulia huko South Africa.
Okay sawa.

Lakini unapaswa kuwatafiti kwa undani zaidi hao Watu kuhusiana na suala hili. Usije ukaingia kwenye Mgogoro wa kisheria dhidi ya Serikali za huko uendako. Wenzetu kwenye nchi zao kuna utawala wa Sheria, nobody is above the law.
Uwaulize, Je, wakati waliponunua hayo magari ya mtumba huko South Africa, walikuwa na Viza ya kuishi huko au walienda tu mara Moja Kama wageni wengine wa kimataifa wenye kibali cha muda mfupi tu cha kuwepo huko??
Pia, ufuatilie na ujiridhishe juu ya uhalali wa manunuzi ya magari yao waliyonayo kwani South Africa ndiyo nchi inayoongoza kwa uhalifu hapa barani Afrika, ikiwamo na uhalifu wa kughushi katika biashara ya kuuza au kununua magari.
 
🙏🙏🙏
 
Zimbabwe,
1. Barabara mbovu zaidi,
2. Rushwa, polisi/Trafiki,
3. Utekaji barabarani.
 
Kitu kikubwa hakikisha unaingia kihalali, naamini hili litakuwa maana unaenda kwa ndege.

Cha pili, hakikisha una documents zote za gari na mauziano ya gari na zipatikane kwenye mamlaka husika ulipe ushuru wao wote. Ukicheza hapa inakula kwako.
La mtumba mkuu! Kuna Shuhuda za wadau wengi wanaodai waliyachukulia huko South Africa.
Katika safari yako Ondoa Zimbabwe kabisa.

Pia Msumbiji kwa sasa sidhani kama bi sehemu sahihi kwasababu za vurugu za baada ya uchaguzi.

Itapendeza hii route ya
1. Botsawana Zambia TZ, au
2. BoT Zam Malawi Tz
3. Namibia Zambia, Tz
4. Namibia Zambia Malaw Tz.

NB. Barabara ya Lusaka Tanzania haikuwa nzuri sana, sijui kwa sasa. Ndio maana inakuwa vizuri ukiingia Zambia unachepukia Malawi barabara ni nzuri hadi Kyela
 
Ulishawah kuvuka border toka uzaliwe. Punguza ujuaji kwenye mambo usiyoyafahamu. Unataka Sheria, Sheria bila kutaja kifungu?. Humu kuna kina Isanga family wanakera Magari toka SA kila siku wewe upo kwa shemeji yako Buza kwa Rulenge unaongea habari za SA
 
Sasa hivi kimebaki kipande kidogo tu kutoka Mpika kuitafuta Isoka nadhani ndio bara bara mbovu ila inatengenezwa ukifika Chinsali ni mkeka mkubwa na mpana mpaka Nakonde..
 
Congo labda uende Kasumbalesa then Rudi Ndola-Kapiri Mposhi-Nakonde/Tunduma
 

Nafikiri wewe bado unaishi katika Mazingira ya ulimwengu wa kufikirika.

Kwa mujibu wa Sheria za Afrika Kusini, hairuhusiwi KUFANYA biashara ya kununua magari ambayo tayari yameshatumika nchini humo (used cars) na kisha kuyasafirisha kwenda nje ya nchi hiyo kwa mtindo wa kufanya biashara ya Kimataifa ya magari yaliyokwisha tumika. Biashara ya namna hiyo inaruhusiwa kwa magari mapya tu (brand new cars).
 
Zimbabwe ni shida sana! Sikushauri upite huko.
Mimi nilipita last year January, Nilitoka SA kununua gari, aisee police wa pale mpakani Victoria Falls walinisumbua sana mpaka nilijuta.
Kinachokera zaidi ni kuwa nilikuwa na nyaraka zote halali but walikuwa wanatafuta kila sababu za kunichomoa hela.
nilijiuliza sana hivi hawa Ndo Nyerere alipambana wapate uhuru halafu wanatufanyia hivi watanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…