Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,063
- 735
Huwezi kuona correlation sasa hivi maana mliharibu baada ya 1985...positive correlation zilikuwepo RDA...JKT...N.K...
Kama sio juhudi zake Nyerere, Zakumi angekuwa wapi...Madilu angekuwa wapi...Mkulu angekuwa wapi...
1961 nchi inapata Uhuru, Baba yangu alikuwa tayari yuko kazini baada ya kuhitimu elimu yake ambayo iligharimiwa 100% na babu na bibi yangu ambao waliishia std4. Kazi hiyo aloanza kuifanya 1961 amedumu nayo mpaka alipostaafu.
Sasa ukiniambia bila Nyerere Madela angekuwa wapi jibu ni kwamba angekuwa hapa Tanzania kwa sababu kusoma kwangu hakukutegemea neema kutoka kwa Nyerere.Pengine kuja kwangu hapa USA kumetokana na after effect za siasa ya mwalimu Nyerere( Vurumai za kiuchumi).
Kusoma kwangu kulitegemea jinsi Bibi(ambaye yuko hai mpaka leo) na Babu yangu walivyopiga mzigo kwa juhudi zote na kupitisha uamuzi wa kumpeleka baba yangu shuleni mwaka 1948 wakati watu wengi au hawakuona faida au hawakuwa informed about education chini ya utawala wa mkoloni.
Maamuzi ya Nyerere yalisaidia watu wengi kusoma mpaka level ya shule ya msingi, lakini yalidumaza ukuaji wa elimu ya juu. Sasa hivi kuna juhudi kubwa sana kukuza elimu ya juu baada ya mfumo wa elimu wa mwalimu kufa kifo cha asili.
Binafsi Nyerere hakunipa nafasi yeyote kwenda shule na sioni mkono wake wala maamuzi yake yanipeleka shule, kwa sababu nchi ingepata uhuru mwaka 1981 shule ningekwenda tu, Nyerere asingetaifisha shule za misheni, shule ningekwenda tu. Upe isningeanzishwa shule ningekwenda tu.
Sioni ni vipi ningeshindwa kwenda shule kwa sababu kwa upande wetu mwamko wa kwenda shule hakuuleta Nyerere uliletwa na Babu na Bibi yangu.
Nisingekwenda shule tu kama baba yangu asingesoma enzi za mkoloni.