Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?

Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?

Huwezi kuona correlation sasa hivi maana mliharibu baada ya 1985...positive correlation zilikuwepo RDA...JKT...N.K...

Kama sio juhudi zake Nyerere, Zakumi angekuwa wapi...Madilu angekuwa wapi...Mkulu angekuwa wapi...

1961 nchi inapata Uhuru, Baba yangu alikuwa tayari yuko kazini baada ya kuhitimu elimu yake ambayo iligharimiwa 100% na babu na bibi yangu ambao waliishia std4. Kazi hiyo aloanza kuifanya 1961 amedumu nayo mpaka alipostaafu.

Sasa ukiniambia bila Nyerere Madela angekuwa wapi jibu ni kwamba angekuwa hapa Tanzania kwa sababu kusoma kwangu hakukutegemea neema kutoka kwa Nyerere.Pengine kuja kwangu hapa USA kumetokana na after effect za siasa ya mwalimu Nyerere( Vurumai za kiuchumi).

Kusoma kwangu kulitegemea jinsi Bibi(ambaye yuko hai mpaka leo) na Babu yangu walivyopiga mzigo kwa juhudi zote na kupitisha uamuzi wa kumpeleka baba yangu shuleni mwaka 1948 wakati watu wengi au hawakuona faida au hawakuwa informed about education chini ya utawala wa mkoloni.

Maamuzi ya Nyerere yalisaidia watu wengi kusoma mpaka level ya shule ya msingi, lakini yalidumaza ukuaji wa elimu ya juu. Sasa hivi kuna juhudi kubwa sana kukuza elimu ya juu baada ya mfumo wa elimu wa mwalimu kufa kifo cha asili.

Binafsi Nyerere hakunipa nafasi yeyote kwenda shule na sioni mkono wake wala maamuzi yake yanipeleka shule, kwa sababu nchi ingepata uhuru mwaka 1981 shule ningekwenda tu, Nyerere asingetaifisha shule za misheni, shule ningekwenda tu. Upe isningeanzishwa shule ningekwenda tu.
Sioni ni vipi ningeshindwa kwenda shule kwa sababu kwa upande wetu mwamko wa kwenda shule hakuuleta Nyerere uliletwa na Babu na Bibi yangu.

Nisingekwenda shule tu kama baba yangu asingesoma enzi za mkoloni.
 
...........shule za missionary au watu binafsi,najua mnatetea eti ilikuwa lazima ili maskini wasome,lakini kumbukeni waliokuwa wanasoma hizo shule nao walikuwa maskini tuu tena wengi wao bure kabisa,kama jasusi alivyosema ukiona watu binafsi au missionary wanajenga na kuendesha shule ni msaada mkubwa sana kwa society na watu wake,...........!

Point taken Mkuu Koba, however wakti huo kulikuwa na ubaguzi (Dini, rangi nk) kwenye hizo shule...unakumbuka hilo?
 
Madela -Wa-Madilu,
Mkuu lugha unayotumia ni ya kibinafsi sana..yaani upana wake ni mdogo sana kiasi kwamba unaweza kudai kwamba hakuna kitu wala mtu yeyote duniani aliyesaidia maisha yako zaidi ya baba na mama yako..
Huko USA, hata kama ndege zisingekuwepo ungefika tu kwani umeshafika sasa nini kingekuzuia..Na bila shaka huwa unashangaa sana kuona watu wakimpongeza rubani kwa kuwafikisha salama..unawaona wajinga sana kwani hawakuona zile turbulence!..Haa haaa haa!..
 
Zakumi,
Babu yangu alinisimulia jinsi Wajerumani walivyokuwa wanawachapa viboko ili walime pamba. Na hiyo unaweza kuiita "incentives?"

Jasusi:

I know what you are talking about, but there is one thing to consider here. The Germans used slave labor while Nyerere used freed-slave labor.
Slave labor=Viboko
freed-slave labor=Incentives

Enlight me if I am wrong.

Z10
 
Inasikitisha sana kuwa mpaka sasa watu hawajaelewa somo. Ndugu zangu, Tanzania ya leo haikuwa ya Jana. Hali iliyokuwepo wakati ule ilikuwa ni ngumu kupita kiasi. Nyerere alijitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha watanzania wanapata Elimu kulingana na mahitaji ya nchi.

Can you look at these statistics and the state of education in Tanganyika/ Tanzania?
In 1961 there was racial and religion descrimination in education system, Nyerere's Government abolished it soon after independence.
"Complete integration of the separate racial systems was introduced very soon after independence, and discrimination on grounds of religion was also brought to an end. A child in Tanzania can now secure admittance to any Government or Government-aided school in this country without regard to his race or religion and without fear that he will be subject to religious indoctrination as the price of learning" (The Africa Global Village: News / Comments / Education for Self-Reliance- Tanzania, 2009)

-By 1961, 490,000 students were attending primary education and most of them ending up in STD IV but by 1967, 825,000 children were attending such schools up to STD VII.
-In 1961, there were 11,832 children in secondary schools, only 176 of whom were in Form IV. By 1967 there were 25,000 and 880 were in form IV

-in 1973 about 106,000 pupils completed primary education,whereby 18,5OO or 8% were selected for entry to secondary schools (TANU, 1974) (http://archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti/vol2no1/aejp002001010.pdf.)

In the 1970s the government introduced the Two year course in Technical education for standard seven leavers who were not able to join secondary education or other training institutions.

Bado baada ya kumaliza O-level au A-level wanafunzi walikuwa na uamuzi wa kwenda kuajiriwa au kujiunga kwenye vyuo mbalimbali

Jitihada zote hizo alizofanya bado watu hawa hawamkubali?

Kumbukeni mambo ya kufanya kwa ajili ya kujenga nchi yalikuwa mengi. Na pia ajira zilikuwa nje nje wakati ule, watu walikuwa wanachaguwa shule au kufanya kazi.

Madela -Wa-Madilu,
Mkuu lugha unayotumia ni ya kibinafsi sana..yaani upana wake ni mdogo sana kiasi kwamba unaweza kudai kwamba hakuna kitu wala mtu yeyote duniani aliyesaidia maisha yako zaidi ya baba na mama yako..
Huko USA, hata kama ndege zisingekuwepo ungefika tu kwani umeshafika sasa nini kingekuzuia..Na bila shaka huwa unashangaa sana kuona watu wakimpongeza rubani kwa kuwafikisha salama..unawaona wajinga sana kwani hawakuona zile turbulence!..Haa haaa haa!..

Mkandara:

Madela anazungumza kitu cha maana sana. Baada ya kuanza shule za bure. Watanzania wamesahau kabisa na wengi wana-take education for granted.

Na sio ubinafsi. Wakati tunapata uhuru, mwamko wa kusomesha tayari ulikuwepo.

Haiwezekani kabisa malalamiko ya mwanzo yalikuwa ni kuongeza idadi ya wanafunzi wanaotoka Tanganyika kwenda Makerere.

Mwamko ulikuwepo, ingawaje si kwa nchi nzima lakini tayari watu walikuwa wana-sacrify mapato yao kusomesha watoto wao.

Baba yangu kalima vibarua, wazazi wake wamekoboa magunia ya mpunga kwa mkono kumpeleka shule. Hivyo leo mtu akiniambia kuwa nilitegemea UPE, nitamwambia you must be kidding.
 
Inasikitisha sana kuwa mpaka sasa watu hawajaelewa somo. Ndugu zangu, Tanzania ya leo haikuwa ya Jana. Hali iliyokuwepo wakati ule ilikuwa ni ngumu kupita kiasi. Nyerere alijitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha watanzania wanapata Elimu kulingana na mahitaji ya nchi.

Can you look at these statistics and the state of education in Tanganyika/ Tanzania?
In 1961 there was racial and religion descrimination in education system, Nyerere's Government abolished it soon after independence.
"Complete integration of the separate racial systems was introduced very soon after independence, and discrimination on grounds of religion was also brought to an end. A child in Tanzania can now secure admittance to any Government or Government-aided school in this country without regard to his race or religion and without fear that he will be subject to religious indoctrination as the price of learning" (The Africa Global Village: News / Comments / Education for Self-Reliance- Tanzania, 2009)

-By 1961, 490,000 students were attending primary education and most of them ending up in STD IV but by 1967, 825,000 children were attending such schools up to STD VII.
-In 1961, there were 11,832 children in secondary schools, only 176 of whom were in Form IV. By 1967 there were 25,000 and 880 were in form IV

-in 1973 about 106,000 pupils completed primary education,whereby 18,5OO or 8% were selected for entry to secondary schools (TANU, 1974) (http://archive.lib.msu.edu/DMC/African Journals/pdfs/Utafiti/vol2no1/aejp002001010.pdf.)

In the 1970s the government introduced the Two year course in Technical education for standard seven leavers who were not able to join secondary education or other training institutions.

Bado baada ya kumaliza O-level au A-level wanafunzi walikuwa na uamuzi wa kwenda kuajiriwa au kujiunga kwenye vyuo mbalimbali

Jitihada zote hizo alizofanya bado watu hawa hawamkubali?

Kumbukeni mambo ya kufanya kwa ajili ya kujenga nchi yalikuwa mengi. Na pia ajira zilikuwa nje nje wakati ule, watu walikuwa wanachaguwa shule au kufanya kazi.

Mimi ni mwalimu by training na nimesoma historia ya elimu Tanzania. Katika mfumo wa elimu ya Tanzania, elimu ya jadi ilikuwa ni elimu complete ingawaje ilikuwa haina kusoma na kuandika.

obsession yenu ya kusoma na kuandika, ilifanya kufikiri kuwa watu wakielimika elimu ya darasani basi nchi itakuwa-mswanu. Watu wamesoma hakuna kinachooneka.

Na kama shule za kujua kusoma na kuandika ni muhimu sana basi Waghana wangefanya vizuri sana. Wakati Karl Peter anapitisha mikataba ya ulaghai tayari waGhana walikuwa na shule.
 
Mwaka 1974 vijana waliomaliza kidato cha sita Tanzania yote walikuwa ni 1,800 (elfu moja na mia nane) tu. Hawa walikuwa ni pamoja na mtoto mmoja wa Mwalimu, ambaye alimaliza Form 6 Mkwawa mwaka huo. Idadi ya vijana waliomaliza kidato cha sita Kenya na Uganda mwaka huo ilikuwa mara 5 au zaidi ya hao.

Kati ya Uhuru na 1985, Mwalimu alijenga chini ya shule 50 za sekondari! Yaani kwa wastani Mwalimu alikuwa anaridhika kujenga sekondari mpya mbili kwa mwaka!

Naona wakubwa wanapeleka watoto wao English Medium Schools. Kwa nini wasirudishe mfumo wa zamani (uliobadilishwa na Mwalimu) wa shule zote kufundisha kwa Kiingereza kuanzia darasa la tatu? Kama ni vizuri kusoma kwa Kiswahili, iweje wahakikishe waoto wao wanasoma kwa Kiingereza?

Siasa ya Elimu Ya Ujamaa na Kujitegemea ilikuwa ndio msingi wa Elimu chini ya Mwalimu. Ni siasa iliyowalimisha watoto nusu siku badala ya kusoma! Ilitokana na kuiga China bila kufikiria.

Mwalimu was a good man. He would have despised people who agreed with things just because they were done by him.
 
Mkulu
What are you insinuating here.
Jifunue.
 
mimi pia nabisha kwa kishindo kuwa mwalimu hakutaka tusome, mwl. Alitangaza vita dhidi ya maadui watatu;ujinga, maradhi na umaskini. hiyo ilitosha sana kwa kila mwenye ufahamu kubaini siraha kamili za kushinnda ama wote maadui au mojawapo ya hao.
 
pia ikumbukwe kwamba TEACHER ALIKUWA ANAHUDUMU KATIKA NGAZI YA TAIFA NA SIO KATIKA NGAZI YA FAMILIA, HIVYO KITAIFA ALIFANYA LILILO KUWA LAKE KWANI SHULE ZILIKUWEPO NA WAALIMU WALIKUWEPO PIA. KILICHOKOSEKANA NI JITIHADA BINAFSI, NI HAYO TU
 
Unaweza kutoa hoja kwamba uchumi wakati wa Nyerere uliyumba (kama quote hapa chini inavyosema) kwa hivyo basi investment kwenye Elimu ulipwaya wakati huo. Sera kama za UPE, au kuchukua vijana wa darasa la 7, form 4 au 6 kwenda kufundisha bila maandalizi mazuri kusomea ualimu.... ni matokea ya mafanikio / mapungufu ya Elimu wakati wa Nyerere.

Tanzania
Tanzania's love affair with industrialization is equally instructive because after the nation gained independence in 1961, President Julius Nyerere made impassioned speeches about reducing
urban-rural income disparities by giving priority to farmers and rural communities. Under Nyerere's leadership, however, the government abolished the Ministry of Local Government and the
Ministry of Cooperatives and forced farmers to give up their private farms and move into ujamaa villages that were modeled after Chinese communal farms. The government used cotton and coffee
tax revenues to help finance the establishment of some 400 state owned companies, including textile and bicycle factories18 and an illfated pulp and paper factory that was built with technical expertise from Finland (Lipumba 1984). When the government paid small scale coffee farmers 23% of the world price of coffee (Tweeten 1989), farmers responded to this economic extortion by smuggling coffee and other crops across Tanzania's porous national borders. Although Nyerere is praised for his honesty, his leadership in fostering ethnic harmony, and his voluntary decision to step down from the presidency, one cannot overlook the grim reality that after receiving billions of dollars of foreign aid, Tanzania is the sixth poorest country in the world (World Bank 1999). Tanzania's economic stagnation is a textbook case of the failure of state-led industrialization and communal farming, and it illustrates how draconian rates of taxation on farmers can spawn a massive smuggling operation across national borders.

extract from http://www.cimmyt.org/english/docs/special_publ/del/3rd_EcoLec99.pdf
 
VERY TRUE

Deadly WRONG

Naomba unipe maelezo kwa nini unadhani ukuaji wa elimu ya juu haukudumazwa na mfumo wa elimu wa Mwalimu Nyerere; hasa ukizingatia kwamba hakukuwa na mkakati wa kupanua chuo kikuu cha UDSM hata ilipofika siku Nyerere alipoachia madaraka, na pengine hadi leo hii idadi ya wanafunzi imeongezwa lakini si Wahadhiri wala vyumba vya madarasa?

Je huoni kwamba Mpaka sasa ni makundi yaleyale yalonyang'anywa shule miak ya 70 ndo yako mstari wa mbele kujenga vyuo vikuu? Na serikali ilo jaa Mafisadi wa kukata kwa mundu ikifuatia nyuma huku ikiwa hoi?
 
Ukuaji wa elimu ya juu na mfumo wa elimu wa Mwl Nyerere......i would not want to go into much details and into specifics......as you may want me to pursue that route......however, in a nutshell, apart from developing UDSM tokea pale Mtaa wa Lumumba mpaka kufikia kuwa SUA and other higher learning technical institutes........and looking on the Budget he JKN spent on Education (you may check on lengthy previous discussions we had here at JF about budget ya education)......labda mtu uwe Kipofu (not to offend vipofu though) ndio utakuwa na maswali kama yako......eti Mwl alidumaza elimu ya juu........again im sorry one must be a joker........

Mfumo tulionao sasa ni VURUGU TUPU....product tunazopata toka ma-vyuoni ndio kama hivo tena.......mediocre kind of output....hata hiyo mediocre nitakuwa nimependela....tuseme below average.....sihitaji kulizungumzia sana hili......na kama hulitambui hili basi...i will be wasting my time..........

Walimu na Vyumba vya madarasa...........sikuwahi kusoma UDSM lakini kipindi cha Mwl sikuwahi kushuhudia...higher learning institutions zikiwa na hali mbaya kama ilivyo sasa....on many aspects........sasa....akina sie ndio tunakuja na excuse.....eti baba alijenga nyumba ndogo...kwa sababu haku-count watoto tutakao zaa akina sie sasa hivi........thats unthinkable from one who knows what is talking about.........

Kuhus Walimu elimu ya juu....ni kweli hili lilimshinda na hasa kutokana na kuzorota vibaya kwa uchumi.....walimu wengi kama akina Mwl Moshi and the like walizamia Nchi jirani za Afrika wengine Marekani na Asia........yes.....now how do we rectify this situation.......kwa Kukaa na kulaumu eti JKN hivi na vile.?!!........shuut
 
Mwl. Augustine Moshi,
Mwaka 1974 vijana waliomaliza kidato cha sita Tanzania yote walikuwa ni 1,800 (elfu moja na mia nane) tu. Hawa walikuwa ni pamoja na mtoto mmoja wa Mwalimu, ambaye alimaliza Form 6 Mkwawa mwaka huo. Idadi ya vijana waliomaliza kidato cha sita Kenya na Uganda mwaka huo ilikuwa mara 5 au zaidi ya hao.

Kati ya Uhuru na 1985, Mwalimu alijenga chini ya shule 50 za sekondari! Yaani kwa wastani Mwalimu alikuwa anaridhika kujenga sekondari mpya mbili kwa mwaka!

Naona wakubwa wanapeleka watoto wao English Medium Schools. Kwa nini wasirudishe mfumo wa zamani (uliobadilishwa na Mwalimu) wa shule zote kufundisha kwa Kiingereza kuanzia darasa la tatu? Kama ni vizuri kusoma kwa Kiswahili, iweje wahakikishe waoto wao wanasoma kwa Kiingereza?

Siasa ya Elimu Ya Ujamaa na Kujitegemea ilikuwa ndio msingi wa Elimu chini ya Mwalimu. Ni siasa iliyowalimisha watoto nusu siku badala ya kusoma! Ilitokana na kuiga China bila kufikiria.
Mwalimu was a good man. He would have despised people who agreed with things just because they were done by him.
Mkuu wangu unajua huwa unanisikitisha sana jinsi unavyoangalia vitu hasa ktk elimu wakati wewe ni mwalimu..
sasa mkuu wangu unapojaribu kuhoji mwaka 1974 kuwa na wanafunzi 1,800 form six una maana gani haswa?.. hapo nyuma tumeambiwa kwa mwaka 1961 kulikuwa na wananfunzi 176 tu form Four..sasa sijui kulikuwa na wangapi hiyo Form six. Licha ya hapo nimesema sana kuwa hao unaowasema 1,800 form six mwaka 1974 walianza lini darasa la kwanza?..
Je, hupati kujiuliza Nyerere aliweza vipi kuwa na wanafunzi wengi kiasi hicho form six within very short time frame maanake kwangu mimi nashindwa hata kuelewa alifanya nini! tofauti ya wanafunzi mwaka 1961 kuja 1967 hadi 1974 ni kubwa sana.. hata sielewi mnachojaribu kusema hapa..

Kisha swala la kufundisha masomo kwa kiingereza toka darasa la tatu naomba unipe kwanza faida zake kutokana na vipindi vya masomo ya darasa la tatu!..
 
Ogah na Mkandara,

Si sahihi kusema Mwalimu hakudumaza elimu ya juu eti kwa vile haikuwa na vurugu. Kitu kikiwa kidogo sana hakiwezi kuwa na vurugu.

Nimechukua mfano wa 1974 as a base line. Thirteen years after independence Tanzania was producing only 1,800 form six leavers per year. Mwalimu aliona hao ni wengi. Mwaka uliofuatia, 1975, akatangaza Azimio la Musoma ili kuwazuia wasiende chuo kikuu moja kwa moja.

Kama unatawala nchi changa, na idadi ya wanafunzi vyuo vikuu haiongezeki kiasi cha kuridhisha basi wewe unadumaza elimu ya juu. That applies squarely to Mwalimu.

Mimi nilikuwa mwaka wa pili UDSM wakati Mwalimu alipotangazia taifa kwamba wanafunzi wa chuo kikuu wamegoma kwenda vijijini. That was a shocking lie! As an idealistic youth niligundua, kwa mara ya kwanza, kwamba Mwalimu anasema uongo! With maturity, niligundua kwamba hata aliposema hakuna sabuni, hakuna dawa kwa sababu ya maendeleo ilikuwa ni uongo, na alijua anasema uongo.

Mwalimu paid lip service to education. He did not put his money where his mouth was. At independence Tangangika was spending 20% of its budget on education. Mwalimu proceeded to cut this down to a mere 4.9% at his departure. Kama angeendelea sijui ingekuwaje.
 
Mkandara,

Kiongozi serious anaweza kuongeza idadi ya wanafunzi wa nchi nzima toka 100 hadi 10,000 katika kipindi cha miaka 10. Hukuona Mkapa alivyoongeza idadi ya wanafunzi haraka? Hata watu wa aina ya Lowasa wameweza kujali Elimu zaidi ya Mwalimu!

Mwalimu alitutawala miaka 25. Nitajie shule za sekondari 25 ambazo alijenga. Huwezi! Hakujenga hata hizo. Badala yake alijishughulisha zaidi na kuhakikisha wanafunzi wanalima, wanakimbia mchakamchaka na kukariri hotuba zake tu!
 
Mwl. Augustine,
Nimechukua mfano wa 1974 as a base line. Thirteen years after independence Tanzania was producing only 1,800 form six leavers per year. Mwalimu aliona hao ni wengi. Mwaka uliofuatia, 1975, akatangaza Azimio la Musoma ili kuwazuia wasiende chuo kikuu moja kwa moja.
Mkuu hapa bado unachemsha...
Mimi sijapitia takwimu hizo ulizotoa lakini nadiriki kusema sio kweli kwa sababu haiwezekani Tanzania ku produce wanafunzi 1,800 wa form six kila mwaka wakati takwimu hizo hizo zinaonyesha ongezeko la wanafunzi kuingia Form five kila mwaka.. Sasa hii idadi yako ya kusema kila mwaka (1,800 per Year) imetoka wapi?..

Yes, tunakubali kwamba pamoja na maongezeko yote alofanya mwalimu bado hesabu haikutosheleza mahitaji ya elimu nchini, na kweli tunakubali kulikuwepo na mapungufu mengi tu lakini mimi nachoweza kusema strategically Mwalimu ali fail pale aliposhindwa kutenganisha Ujamaa kama society anayotaka kuijenga na Ujamaa kama siasa inayo control maslahi ya Taifa..Kila alipokutanisha vitu hivi viwili tulishindwa kwenda mbele kwa sababu huwezi kufanya biashara ukajiuzia wewe mwenyewe..Ujamaa kama society kwa mtazamo wangu hugawana walichouza na sio kugawana walichovuna..Huu ni usemi unaotaka muda mrefu kuuelezea on why we failed..

Sasa tofauti ya mwalimu na leo ni kwamba tuligawana mavuno wakati wa mwalimu na leo hii tunakula mbegu....iwe ktk elimu, afya na hata Uchumi..
Kumlaumu mwalimu wakati hatuna hata mfano bora zaidi ya kuonyesha Kenya ambao kabla hata ya Uhuru walituzidi sisi kwa hesabu kubwa sana ni kufufua chuki nyingine dhidi yake..

Na kama nilivyosema jinsi sisi tunavyotaka maendeleo ndivyo Kenya nao wanakwenda mbele haiwezekani wao wasimame mahala sisi tuje kuwakaribia au kuwakamata ndio iwe mfano bora wa elimu yetu..Hatushindani mkuu wangu - Watu na Mazingira yetu tofauti kabisa!..
 
Mwl. Augustine Moshi,
Ninarudia swali lako la pili unapotaka kuona mwalimu kajenga shule 25 za secondary.. Mkuu wangu mimi nafanya biashara, mtaji wa kwanza ni mgumu sana kuzalisha unaweza kabisa chukua mwaka kabla kuhaona faida.. na siku biashara ikianza kunoga ndipo unapoweza kununua mali zaidi na kulijaza duka.. Hata siku moja huwezi kudandia mali iliyokwisha kuwa na msingi ukasema umezalisha zaidi na kusahau kazi nzito ya mtu aliyeweka msingi huo..
Kuchukulia takwimu za Andindile:-

By 1961, 490,000 students were attending primary education and most of them ending up in STD IV but by 1967, 825,000 children were attending such schools up to STD VII.
-In 1961, there were 11,832 children in secondary schools, only 176 of whom were in Form IV. By 1967 there were 25,000 and 880 were in form IV..
-in 1973 about 106,000 pupils completed primary education,whereby 18,5OO or 8% were selected for entry to secondary schools (TANU, 1974)..

Mkuu binafsi nishafanya uchunguzi na nadhani unakumbuka miaka ya nyuma tumewahi kuzungumzia hili.. Hadi wakati wa Mkapa asilimia ya wanafunzi waliojiunga na shule za sekondary ilikuwa 7 kama ile ya Nyerere hakuna tofauti zaidi ya hesabu ya wanafunzi kuonekana kubwa.
Nikiwa na maana kama Nyerere alipeleka wanafunzi 7 sekondary kwa kila 100, Mkapa alipeleka wanafunzi 70 kwa kila 1,000...Hapo hujajenga kitu mkuu wangu kama tutataka kuitazama elimu kwa kiwango kinachotakiwa...tunashindwa kutazama wali fail kwenda mbele kama kigezo cha uzembe wa mfumo wa elimu..Ndilo tatizo kubwa la takwimu zetu siku zote.

Mwaka 1973 wanafunzi waliomaliza darasa la saba walikuwa 106,000 na akasifiwa ktk kufuta ujinga leo hii tunazungumzia millioni 1 na upupu, mara kumi ya hesabu ya mwalimu sasa hapa unahitaji shule ngapi!.. mkuu wangu tulichobadilika ni ukubwa wa umbo tu hivyo unachoona sasa hivi ni ukubwa wa nguo.. wakati wa mwalimu tukiwa wachanga tulivaa nepi ktk elimu leo hii tunavaa suruali ukubwa wa nguo hiyo usikutishe ni feki - made in China..
 
Back
Top Bottom