Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?

Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?

..kama mtakumbuka Mwalimu Nyerere alianzisha mpango wa quota system.

..mpango huo ulikuwa na lengo la kuidhibiti mikoa kama Kagera[ziwa magharibi] na Kilimanjaro isi-dominate ktk idadi ya wanafunzi wanaokwenda shule za serikali za sekondari.

..quota system iliweka pass mark ya juu zaidi ktk mikoa kama Kilimanjaro na Kagera, huku mikoa ya pembezoni ikipewa pass mark ndogo.

..maelezo ya Mwalimu yalikuwa ni kuleta usawa ktk upatikanaji wa fursa za elimu kwa kila Mtanzania.

..kuna watoto toka Kagera na Kilimanjaro walilazimika kubadilisha majina na kwenda mikoa yenye pass mark ndogo kurudia mitihani ya darasa la 7. je, akitokea mwananchi wa Kagera au Kilimanjaro akamlaumu Mwalimu kwa kumnyima elimu akiwa kwao atakuwa amekosea?

..kulikuwa na ubaya gani kwa Mwalimu kuboresha mazingira ya upatikanaji elimu ktk mikoa ya 'pembezoni' bila kuwawekea kuwawekea 'spidi gavana' au quota system wanafunzi wa Kagera na Kilimanjaro?

..kuna wataalamu wanadai wanafunzi waliotoka mikoa ya pembezoni na kubebwa kwa quota-system hawakuwa wameandaliwa vizuri hivyo matokeo yake waliishia kufanya vibaya walipofika sekondari.

..je, mwananchi wa mikoa ya pembezoni ana haki ya kumlaumu Mwalimu Nyerere kwa kutoboresha mazingira ya upatikanaji elimu na badala yake kuwapatia quota system ambayo in a long run didnt help them that much?
 
Tuliswagwa kama ng'ombe na kuamuliwa kushika jembe na kulima kwa pamoja katika mashamba ya bega kwa bega.
MWalimu angeamuru wananchi hao hao wafayatue tofari na kujenga shule zao wenyewe, kwanza kwa kuanza na Primary school kisha kuendelea taratibu na Secondary school nani angebisha wakati ule?
Tafsiri ya ujamaa wa Nyerere siku zote imekuwa kugawana kilichopo kwa mtindo wa kimasikini kuliko kuongezea nguvu juu ya kile kilichopo na kugawana kwa mtindo wa kimaendeleo.
Unanyang'anya shamba la Mwamwindi na Mwangubi wanao lima kwa matrekta huko Isimani Iringa na kuzrisha mahindi kibao, na kuwapa wanakijiji wanao lima kwa jembe la mkono na kuacha magugu yatambe kila kona na kuvuna haba.
Unavuna risasi ya kifuani na njaa.
Ni rahisi kuwatawala watu wenye njaa na wasio na elimu.

Hisia zangu na tafakari zinanipeleka kwenye hitimisho moja kwamba MWalimu alipenda wasomi wachache ambao wanajiona wana bahati ya kufika pale walipokuwa na hivyo kuwa Royal kwake milele." Bila MWalimu Nyerere nisingefika hapa"
Watu kama Ben mkapa walikua Royal kwa Mwalimu kwa mtindo wa Fisi katika ngozi ya ndama na pembe za mbuzi(japo yeye si uzao wa mfumo wa elimu wa Nyerere).
Nyerere alikuwa hashauriki na watu waliokuwa wakionyesha kumcriticize wazi wazi.
Nyerere alipenda watu waliokuwa wakitii mara moja bila kuuliza kama Kawawa.
Kilichokuja kumpa ushauri wa maana Nyerere ni kushindwa kwa sera zake mwenyewe na joto la kuanguka kwa mfumo wa kikomunisti Duniani, hapo aliamua kuweka manyanga chini na kuachia mchuma ukiporomoka kwenye mteremko bila break za uhakika.

Leo tunaambiwa yeye apewe sifa lawama tuzivae sisi.
Kuna mambo mengi ya kumpa sifa Nyerere bila mikwaruzo, katika suala la elimu mtapata shida sana kuzuia hoja kama hizi zetu akina Madela ili kumfanya Mwalimu apewe sifa bila mawaa.

Ni kweli watu walikuwa vumbi tupu kwa ujinga na umasikini lakini si kweli kwamba hakuwa na vision ya kujiendeleza.
Makanisa karibu yote huko vijijini by 1961 yalikuwa yamwfungua kitu inaitwa Bush School ambayo ilikuwa ikitoa elimu mpaka darasa la pili. Makanisa mengi yalikuwa tayari kabisa kuziboresha shule hizo ziweze kufikia kiwango cha darasa la nne. Waumini wake walikuwa tayari kufanya hivyo bila msaada wa serikali.
MWalimu alipokuja na dote yake ya kutaifisha shule mipango hii ya kukuza elimu kupitia sehemu zinazo waunganisha wananchi ilikwama kwa takriban miaka 25.
Baada ya Mwalimu kushindwa katika ulingo wa kukuza uchumi Tanzania. Makanisa haya kwa mara nyingine yamejitumbukiza tena kutoa elimu kwa mtindo ule ulio pigwa kibano miaka ya 60..
Leo si Bush Schools tena ni Tumaini Universities.

Huwezi kudai kwamba Elimu ya Chuo kikuu siku hizi ni vurugu tupu wakati unaipa less tha 5% ya bajeti yako na fedha nyingi kuishia kwenye mikutano ya kijinga na safari kwenda kuomba nje ya nchi kila siku.
Serikali inaongozwa na uzao wa watu waliosomeshwa vizuri na kuwa Royal kwa mwalimu lakini wasio na utaifa wala hisia za kujitegemea. Watu wanao amini kwamba wao ni kundi la watu bora kabisa Tanzania kwa kuzingatia kwamba walisoma kwa utii na unyoofu wakati shule zilipokuwa shule kweli kweli,nuri, chache na zenye mtizamo wa kujenga tabaka la wasomi wachache walioandaliwa kuajiriwa kuliko kujiajiri na mbumbu wengi wanaojua kusoma na kuandika na kudai kuwa ni wasomi au wamefuta ujinga.

Mtu akiambiwa mjinga, ni kwamba hajui kusoma na kuandika???
 
Jokakuu,
kama mtakumbuka Mwalimu Nyerere alianzisha mpango wa quota system.

..mpango huo ulikuwa na lengo la kuidhibiti mikoa kama Kagera[ziwa magharibi] na Kilimanjaro isi-dominate ktk idadi ya wanafunzi wanaokwenda shule za serikali za sekondari.

..quota system iliweka pass mark ya juu zaidi ktk mikoa kama Kilimanjaro na Kagera, huku mikoa ya pembezoni ikipewa pass mark ndogo.
Mkuu hii hata haijakaa vizuri kabisa.. ebu soma tena kisha nambie unachojaribu kusema..
 
Mkandara said:
Mkuu hii hata haijakaa vizuri kabisa.. ebu soma tena kisha nambie unachojaribu kusema..

Mkandara,

..hivi hili suala la quota-system kwako ni geni?

..hujui kwamba kuna vijana walikuwa wanatoka Kagera na Kilimanjaro kwenda kurudia mitihani ya std 7 kwenye mikoa yenye pass mark ya chini?

NB:

..idea ya kutoa elimu kwa wote ni nzuri. lakini njia hii ya quota system sidhani kama ilikuwa ni njia nzuri.

..baada ya miaka kadhaa ya utekelezaji wa quota system bado mazingira ya utoaji na upatikanaji elimu ktk mikoa ya pembezoni yaliendelea kuwa mabaya.
 
Madela Wa Madilu,
Mku hakuna mtu anazungmzia Ujamaa hapa.. taabu za kulima hata China walizipata. Msumbiji na Angola walikuwa vitani miaka yote na wajamaa imekuwaje wao wasogee hatua za maendeleo sisi tumebakia pale pale..
Mkuu nitazidi kukufahamisha kwamba Nyerere pamoja na makosa yote, tusitafute sababu.. record inaonyesha wazi tulikuwa na wanafunzi wangapi shule za juu, Wataalam krtk utekelezaji.. Inachukua miaka zaidi ya 14 kumtayarisha mtoto kufikia ngazi yoyote ile ya juu ktk elimu. Mambo mengi yaliyotokea miaka ya 70 na 80 ni watoto walianza shule wakati wa Mkoloni..
Kama alivyosema Augustine Moshi mwaka 1974 walikuwa wanafunzi 1800 form six, hawa wote walianza shule ya msingi miaka 15 nyuma..kwa maana hiyo walianza mwaka 1959 kama sikosei tukitawaliwa bado na mkoloni..
Nina hakika kama sii Nyerere kutengeneza njia bora kwa kina Asugustine ni wachache sana wangefika form six kama madai yake kwani record ya mkoloni inaonyesha wazi..
Hivyo kuongezeka kwa wanafunzi ngazi ya juu kwa aslimia 300 kila mwaka ni record nzuri sana kwa maskini..Tena basi kati yao wote ni wasomi bora zaidi ya kuwa na utitiri wa wahitimu..
Kweli kabisa ilikuwa inauma sana kuona shule nyingi za Primary zikito mwanafunzi mmoja au wawili kwa mwaka kuingia sekondary lakini hesabu yake kwa mikoa yote ni ongezeko ambalo linatia moyo..Hakuwa perfect lakini mwanzo ni mgumu sana kulinganisha na wakati huu kwani nina hakika kama utaondoa Private schools sidhani kama Mwinyi au Mkapa wameweza kuongeza elimu ya juu kwa kiwango cha mara TATU kwa miaka 10 waliyokuwepo madarakani..
Hivyo tutazame pia mfumo wa kisiasa ambao hata China uliwakwaza lakini baada ya mabadiliko ya Kiuchumi, misingi bora ya kuendeleza elimu na kilimo ilifuatwa na harambee likapigwa. Tena basi wao ndio waliswagwa kama mbuzi lakini kwa hiari wakiamini viongozi wao walifahamu wanachokifanya..Hawa walikuwa hawakusoma kama sisi zaidi ya vitabu vya Mao Tse Tung na Mapinduzi ya kifikra..
Tatizo ni wewe na mimi mkuu wangu, sisi wadanganyika wasiotaka maendeleo zaidi ya kutafuta mchawi na uganga wa kurogana.. Nchi yetu imekosa vitu muhimu ktk kutafuta maendeleo - WATU na UONGOZI BORA.
 
Jokakuu,
Mkuu kufahamu kwangu quota system hakuwezi badili maana ya hoja yako..mimi bado sijakuelewa kwa sababu nachoelewa mimi ktk miaka yote ya utawala wa Nyerere mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, Mbeya na Dar-es Salaam ndiyo ilikuwa ikitoa wanafunzi wengi kuingia Sekondary na hata Chuo Kikuu kwa sababu ndiko pekee kulikokuwa na shule nyingi za - A levels..
Pili, Wazazi wengi wasomi kwa makabila yao walisambazwa mikoani Tanzania nzima, hivyo sii rahisi kwa mtoto wa Mchagga au Mhaya kubakia kwao wakati wazazi wake wamepigwa trasnfer Mwanza..akihamia Mwanza bila shaka atarudia darasa..
Sasa nifahamishe unachojua wewe maanake sote tumesoma wakati wa Nyerere ni level gani unayozungumzia..
 
300%??

Hesabu huwa nazipatia kidogo.

300% ina kwenda hivi ukiwa na mtu mmoja chuo kikuu leo mwakani utakuwa na 1 x 300%/100%=3 negleting the first student in the first year.

Mwaka unaofuata 9 mwaka mwingine tena 27

1,3,9,27,81....3^(n-1) where n=(0,1,2,3--n)

Ukibadnika 100 kwenye first term.

100,300.900,2700,8100,24500......

Ukuaji huu haukubaliani na hali halisi.

Labda kama na idadi ya wanafunzi wa shule za msingi imo humo kwenye 300%

Nielewesheni
 
..kama mtakumbuka Mwalimu Nyerere alianzisha mpango wa quota system.

..mpango huo ulikuwa na lengo la kuidhibiti mikoa kama Kagera[ziwa magharibi] na Kilimanjaro isi-dominate ktk idadi ya wanafunzi wanaokwenda shule za serikali za sekondari.

..quota system iliweka pass mark ya juu zaidi ktk mikoa kama Kilimanjaro na Kagera, huku mikoa ya pembezoni ikipewa pass mark ndogo.

..maelezo ya Mwalimu yalikuwa ni kuleta usawa ktk upatikanaji wa fursa za elimu kwa kila Mtanzania.

..kuna watoto toka Kagera na Kilimanjaro walilazimika kubadilisha majina na kwenda mikoa yenye pass mark ndogo kurudia mitihani ya darasa la 7. je, akitokea mwananchi wa Kagera au Kilimanjaro akamlaumu Mwalimu kwa kumnyima elimu akiwa kwao atakuwa amekosea?

..kulikuwa na ubaya gani kwa Mwalimu kuboresha mazingira ya upatikanaji elimu ktk mikoa ya 'pembezoni' bila kuwawekea kuwawekea 'spidi gavana' au quota system wanafunzi wa Kagera na Kilimanjaro?

..kuna wataalamu wanadai wanafunzi waliotoka mikoa ya pembezoni na kubebwa kwa quota-system hawakuwa wameandaliwa vizuri hivyo matokeo yake waliishia kufanya vibaya walipofika sekondari.

..je, mwananchi wa mikoa ya pembezoni ana haki ya kumlaumu Mwalimu Nyerere kwa kutoboresha mazingira ya upatikanaji elimu na badala yake kuwapatia quota system ambayo in a long run didnt help them that much?

Individually YES........as a NATION......hell NO

Joka Kuu
Unafahamu vizuri uongozi si kitu lelemama....na hasa unapokuwa na limited resources.........hekima/busara inahitajika sana....na wala si mambo vitabuni tena..............

ili upige hatua.........maamuzi mengine yanafanyika at expense of others or other things.............the issue now become.....the significancy i.e. by how much...and what are the margins.......ukisha-determine hivyo vitu....then compensation become one of options kwa wale/mazingira yalioathirika...........
 
Mkandara,

..Mwalimu alikuwa na idea yake nzuri tu equal access to education for all.

..sasa ikafika mahali ikaonekana kwamba kuna mikoa ina-dominate katika kupeleka wanafunzi shule za sekondari za serikali.

..kutokana na hali hiyo Mwalimu na washauri wake wa elimu wakabuni huu utaratibu wa quota-system ili kutoa nafasi zaidi kwa ile mikoa ya 'pembezoni.'

..iliwalazimu wazazi wenye mwamko wa elimu ktk mikoa kama Kagera[wakati huo ziwa magharibi], Kilimanjaro, kuwapeleka watoto kurudia mtihani wa std 7 ktk mikoa ya 'pembezoni' ili kupambana na quota-system. wako baadhi walibadili hata majina ili wasijulikane wanatokea Kagera, au Kilimanjaro.

..mimi nadhani Mwalimu angeelekeza nguvu zaidi ktk kuimarisha shule za mikoa ya pembezoni, bila kuwafunga 'spidi gavana' wanafunzi wa Kagera na Kilimanjaro.
 
Wakuu,

Mfumo wa elimu ulikuwa mbaya tangu wakati wa Mkoloni. Watu walikuwa wakisomeshwa ili wawe makarani na wasaidizi katika ofisi za Mkoloni. Hawakusomeshwa ili waelimike. Mwalimu JKN alikuwa na nia nzuri sana ya kutaka wananchi waelimike, lakini naye katika juhudi zake alifanya makosa kama binadanu mwingine yeyote.

Kosa kubwa sana ni lile la kuchukua watu walioshindwa na kuwafanya walimu wa UPE. Mtu, yeye mwenyewe yuko taabani, vipi umtegemee afundishe wengine wafanikiwe?
Kosa hili amelirudia tena Kikwete. Kujenga shule za sekondari kila kata bila ya kujuwa wapi walimu na vifaa vitapatikana.

Suluhisho ni cash-course za walimu. Walimu hao hawatakuwa na tofauti na walimu wa UPE.

Tatizo la wasomi wengi wa Tanzania, liko katika lugha. Hatujui Kiswahili wala Kiingereza na pengine hata lugha zetu za kikabila hatuzijui sawasawa. Unapokuwa hujui lugha basi hata kukieleza kile unachokijua inakuwa ni kazi kubwa. Na wakati mwingine hueleweki na kuonekana hujui kitu.
 
..watu wakizungumza bila data mnawalaumu. wakiamua kuleta data mnageuza kibao mnasema zimeandaliwa na 'haters' wa Mwalimu.

..tufike mahali tukubali ukweli kwamba mfumo wetu wa elimu tangu enzi za Mwalimu unapoteza wanafunzi wengi sana kabla hawajafika chuo kikuu.

..enrollment ktk primary schools ni nzuri, lakini tuna wanafunzi wachache sana ktk shule za sekondari, chuo kikuu, pamoja na vyuo vingine vya elimu ya juu.

FMES,

..Tanzania ilikatiwa misaada kwa mara ya kwanza wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

..baada ya kuingia Mzee Mwinyi na kukubaliana na masharti na maelekezo ya IMF na WB wahisani wakarudisha tena misaada.

..ikafika mahali Mzee Mwinyi akajisahau. yeye na serikali yake wakajitumbukiza kwenye ufisadi na uzembe wa kutokukusanya kodi. wahisani wakaamua kutukatia tena misaada wakimshinikiza Mzee Mwinyi amuondoe waziri wake wa fedha Prof.Malima.

..Mkapa ndiye aliyekuja kurudisha tena imani ya wahisani kwa serikali yetu kwa juhudi zake za kulipa madeni, kudhibiti mfumuko wa bei, na kuruhusu wawekezaji wa nje.

- Mkuu kaanglie tena facts, misaada ilikatwa under Mwinyi, sio Mwalimu.

Respect.

FMES
 
FMES said:
- Mkuu kaanglie tena facts, misaada ilikatwa under Mwinyi, sio Mwalimu.

Respect.

FMES,

..Mkuu, hilo halina hata mjadala. Mwalimu alikatiwa misaada ndiyo maana nchi ikapauka kiasi kile.
 
FMES,

..Mkuu, hilo halina hata mjadala. Mwalimu alikatiwa misaada ndiyo maana nchi ikapauka kiasi kile.
jokaKuu,
I hate to disappoint you. Mwalimu hakuwahi kukatiwa misaada. Kilichotokea nchi kupauka ni baada ya vita vya Uganda. Tanzania paid for every armament we bought from the Russians. Only Angola came to our rescue. Mwinyi ndiye aliyetishiwa kukatiwa misaada na sina hakika kama hatua hiyo ilichukuliwa.
 
FMES,

..Mkuu, hilo halina hata mjadala. Mwalimu alikatiwa misaada ndiyo maana nchi ikapauka kiasi kile.
Viulivyopausha nchi ni (i) Economic crisis ya mwaka late 1970s, (ii) High fuel crisis (iii) njaa ya kali miaka ya 70 (iv) vita ya Uganda (v0 uhujumu uchumi
 
niulize kukuza elimu ni kujua kusoma na kuandika au?

......kila nikiangalia cha nyerere kusifiwa kila wakati sioni.....apart from education ndio katufikisha hapa tulipo na umaskini huu.......
 
Siasa ya Mwalimu NyerereIlikuwa ni Siasia ya Ujamaa na Kutegemea.
Sasa kuna Siasa ya Ujamaa kwa wananchi na Ubepari kwa Viongozi wa juu Kisiasa na kujijazia fedha za ufisadi mifukoni.
Hata Kingunge aliyejifanya mkomunist wa kukata kwa shoka naye anatetea siasa hiyo.

Siasa ndiyo inayozaa mwelekeo wa kiuchumi, kisha uchumi ukikomaa unailazimisha siasa kuchukua mwelekeo unaofanana au kwenda sambamba na uchumi.

Vijijini watu wanachangishwa kwa nguvu wakati Viongozi wa juu wa CCM na serikali yake wamebariki wizi na wanaendelea kulinda wezi kwa nguvu zao zote hadi sasa.

Huu si undumila kuwili tu ni Undumila Kutatu.

Ujamaa, Ubepari na Udikiteta.
 
Wakuu,

Mfumo wa elimu ulikuwa mbaya tangu wakati wa Mkoloni. Watu walikuwa wakisomeshwa ili wawe makarani na wasaidizi katika ofisi za Mkoloni. Hawakusomeshwa ili waelimike. Mwalimu JKN alikuwa na nia nzuri sana ya kutaka wananchi waelimike, lakini naye katika juhudi zake alifanya makosa kama binadanu mwingine yeyote.

Kosa kubwa sana ni lile la kuchukua watu walioshindwa na kuwafanya walimu wa UPE. Mtu, yeye mwenyewe yuko taabani, vipi umtegemee afundishe wengine wafanikiwe?
Kosa hili amelirudia tena Kikwete. Kujenga shule za sekondari kila kata bila ya kujuwa wapi walimu na vifaa vitapatikana.

Suluhisho ni cash-course za walimu. Walimu hao hawatakuwa na tofauti na walimu wa UPE.

Tatizo la wasomi wengi wa Tanzania, liko katika lugha. Hatujui Kiswahili wala Kiingereza na pengine hata lugha zetu za kikabila hatuzijui sawasawa. Unapokuwa hujui lugha basi hata kukieleza kile unachokijua inakuwa ni kazi kubwa. Na wakati mwingine hueleweki na kuonekana hujui kitu.
 
Wa kwanza wanaostahiki kumlaumu Nyerere kwa kukoseshwa elimu kwa makusudi kabisa ni waIslam wa Tanzania. Intentionally and systematically Nyerere aliwakandamiza waislam kielimu.

For proof and statistics follow this link: http://www.igs.net/~kassim/nyaraka/Elimu2.html
 
Wa kwanza wanaostahiki kumlaumu Nyerere kwa kukoseshwa elimu kwa makusudi kabisa ni waIslam wa Tanzania. Intentionally and systematically Nyerere aliwakandamiza waislam kielimu.

For proof and statistics follow this link: Dear brothers and sisters in Islam,

naaam the real dar es salaaam.....now you talking

Yo Yo, huyo ndiye Dar Es Salaam, angalau sasa kila moja ataweza kumjua. Hiyo ya Elimu ni geresha tu - the shadow knows best !! Hongera Dar Es Salaam !!
 
Back
Top Bottom