Intersted Observer,
Bwana Mkandara,
Umesema Waislam walilazimishwa kubadili dini; are you sure? Mie kuna ndugu zangu zaidi ya watatu ambao ni Waislam na wanamajina ya ki-islam walisoma vizuri sana na kumaliza shule hizo hizo.
Mkuu nasema hivi kila Muislaam aliyesoma shule za Misheni aidha alibadilisha jina (nikiwa mmoja wao) au alibadilisha dini..Hii nazungumzia kabla ya mwaka 1967 waulize wazee wote waliosoma miaka ya 50 hadi 60 kuhusiana na ubaguzi elimu nchini..kuna mbinu tofauti zilitumiwa na Waislaam kusajili watoto wao, hivyo ni lazima uwe mmoja kati ya wazazi hao upate kuelewa.
Mkuu wangu, hizi habari za China zinakuja tu kwa sababu tulifuata siasa ya Kijamaa, leo hii Chevez anayafanya hayo hayo kabla ya hata ushurika wa China na Urusi ambao wote leo hii sio Wajamaa tena ni Mabepari..
Tatizo la sisi binadamu ni pale tunapotaka kutafsiri kila kitu kwa siasa... leo hii Obama anapo Bail out mashirika na kutangaza regulation wanasema ni Ujamaa wakati swala sii lazima iwe Ujamaa kuelewa kwamba regulations zinatakiwa kuwepo iwe ktk mfumo wowote ule wa Kisiasa...Nyerere kabla hata ya Ujamaa alitaifisha baadhi ya Hotel Dar -es Slaam kwa sababu walikataa kuwahudumia watu weusi tena nakumbuka kisa cha Meya wa kwanza Dar es Salaam..
Kashogi alipokwenda Kenya miaka ya 70, alinyimwa chumba hotel moja ya Kenya, kesho yake aliinunua Hotel nzima na kuwafukuza wafanyakazi waliomnyima chumba..Kitendo hiki hakimfanyi Kashogi kuwa Mjamaa binafsi!..
Kwa hiyo maamuzi haya hayana siasa isipokuwa ni kutazama haki. Trust me, hata kama mimi ningekuwa Bepari kiasi gani siwezi kukubali shule za Kikristu au za Kiislaam zisajili watu wenye imani zao tu wakati wanapotoa Elimu Dunia..Mkuu wangu wewe hukupitia haya na kwa bahati mbaya unasikiliza simulizi za watu ambao sifahamu wamesoma shule zipi..Na unaposema wamesoma vizuri tu ktk shuloe hizo hizo hufahamu mbinu zipi wazazi wao walitumia kuwasajili watoto hao..Acha wakati ule wa Mkoloni wewe unafahamu kwamba hata leo hii wapo watoto wanaobadilisha dini ili wapate ELIMU nzuri - Tanzania?.. Unajua kwamba wapo watoto wanaobadilisha dini ili wapate huduma za NGO's zilizoingia nchini kusaidia watoto Yatima na wale wa familia zisizojiweza..
Unajua kwamba kuna watu waliokufa, wameshindwa kuzikwa na ndugu zao kwa sababu tu wamebadilisha dini?...Huu upuuzi wa Elimu ya dini kutawala Elimu dunia na utu wetu unatoka wapi kama sio makombo ya fikra duni za kupandikizwa..Hivi kweli mnaona maisha ya leo yana unafuu wowote ktk jumuiya zetu wakati Watanzania tumepoteza kabisa values zetu leo hii tunaona Uzungu na Uarabu kuwa ndio deal..kiasi kwamba hata watoto wetu tunawakanya urafiki au ushirikiano na mtoto mwenye imani tofauti..
Mkuu wangu Tanzania inakoelekea ni Kubaya zaidi na sijui kama wewe umewahi kufikiria tanzania ya kesho itakuwa na picha gani..Sasa kama Nyerere alikuwa ameambukizwa na Wachina sijui mfumo huu mtasema tunaambukizwa na Utawala gani?..
Ohh by the way nimesema mfumo alioacha mwalimu hadi Mwinyi, nikiwa na maana mfumo wa ELIMU sio Mwinyi alichokifanya au utekelezaji wa utawala wa Mwinyi..
Hata leo hii ndani ya mfumo huu anaweza kuja kiongozi akaongoza vizuri, lakini haina maana mfumo mzima ni mzuri.. sikubaliani na Dini kuwa chanzo cha elimu dunia ya mwananchi..