Kwanini watanzania wanapenda ukuta na mageti?

Nchi za Ulaya wanajenga nyumba kwa kutumia mbao kutokana na mbao zinasaidia kukinga baridi isiweze kuingia ndani kipindi cha baridi kali tofauti na kujenga nyumba za matofali. Halafu kwao gharama za kujnga nyumba ya mbao ni rahisi kuliko kujenga nyumba ya matofali.

Na jambo lingine ulaya na Ameriak kila raia ana silaha bunduki na pistol ukijaribu kuingia katika eneo la nyumba yake anaweza kukupiga risasi ukafia mbali.tofauti na huku kwetu matajiri peke yao ndio wenye silaha waliobakia Raia wa kawaida hawana silaha. Kwa hiyo usifananishe nyumba za Ulaya na Amerika ukafananisha na nyumba za Afrika ni tofauti kabisa.
 
Hata viongozi wa majeshi wana walinzi na silaha lakini na wao wanaishi ndani ya geti😂😂
Wachungaji, mitume wa kibongo ,pamoja na upako wote walionao bado Wana lala ndani ya geti.


mashekh Wote Wana lala nda ya geti, japo wanajua kusoma albadili.

Tz kisiwa cha amani
 
Hata viongozi wa majeshi wana walinzi na silaha lakini na wao wanaishi ndani ya geti😂😂
Hata Rais anayesema Nchi ni kisiwa cha Amani, amezungukwa na manyamera wamebeba pipe ziko online
 
Wachungaji, mitume wa kibongo ,pamoja na upako wote walionao bado Wana lala ndani ya geti.


mashekh Wote Wana lala nda ya geti, japo wanajua kusoma albadili.

Tz kisiwa cha amani
Ni nje ya mada ila kwa kuwa umetaja ntahighlight, dua ya ahlul-badri ni ushirikina na hakuna mafunzo ya uislamu yanayoelekeza jambo hilo, ni vyema hao wenye kufanya hivyo ukawaita ni wavaa kanzu wanaosoma dua ya ahlul-badri, ila uislamu uko mbali kabisa na mambo hayo.
 

Binafsi ni usalama lakini naamini wapo ambao wanaona kama fashion au kasumba

Nchini kwetu usalama mdogo hatuna mifumo ya polisi mizuri, hata ukiibiwa umshike mwizi bado haikusaidiii imagine karne hii simu zinaibiwa na technologia ya kuzipata zipo lakini hamna anaeshughulikiwa! Kwetu ulinzi ni jukumu binafsi, Serikali haina msaada.
 
NI USHAMBA WA KUTUPWA KWA WATANGANYIKA, WALA SIO KUA NA HELA.
-yaani unakuta mtu amejenga ukuta mkubwa kama anazuia utoroshaji madini ya tanzanite
-yaani bank fensi zao fupi fupi no bwembwe, pita sasa nyumbani kwa mwalimu wa biology unajiuliza hawa watanganyika nani amewaroga
-ushamba ushamba ndani ya mageti ndiko wanakozalisha watoto mashoga tv mda wote ndani huko
-fenci jenga ndogo tu hata ue unawaona majirani sio fensi kubwa kama upo jela buana
-fensi sio ulinzi ni ubinafsi wa kishamba hio hela kamjengee hata ndugu yako banda la mifugo
-fensi kama la jela kwaajili ya kulaza IST,VITS premio,
-ushamba wa kusign nyumba hasa kushindwa kuzingatia maswala ya vyumba vya parking za magari majiko ya ndani nk.
-ukuta mkubwa hufugi hata kuku huna hata mbwa facken kabisa.
 
Hapo ukuta ukiwa mfupi,wewe hushindwi kuchomoka na tairi la ka IST kake. Huko ulaya na marekank nani ana shida hiyo? Afuge bata tu,anakesha mtaani kuwatafuta,kumbe mmeshawanyonyoa na manyoa mpaka mpande gari kuyatupa kwingine,isijulikane mliwaiba mkawala.🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ni matukio yanatufundisha tabia. Na wewe utajifunza tukio likikupata.
 

Ikulu ya USA unaweza kupiga picha leo pita Magogoni kapige picha ulete mrejesho.

Ustaarabu wetu uko tofauti sana, huku kwetu bila fence kuku wa jirani watakusumbua, mbuzi, mbwa, vibaka wa kubebe kandambili. Je hayo yapo huko Ulaya na Marekani?
 
Wewe hujakatazwa kuishi kama Ulaya, jenga nyumba yako ya mbao, Park gari zako tu hata mbili za kutembelea na zisiwe kuuubwa sana audi q7, na ki BMW x5.....na usiwe na wasiwasi
Wazee wa kazi wataiba mpaka injini kudadadeek!
 
Huko Marekani watu wanaiba hata taa za nyumbani?, taa za gari?,rediao, side mirror?, wanaiba tv kisogo na mparazo? Kuna panya road wanavamia nyumba na kulazimisha utoe Mpesa chini ya ubapa wa panga? Siyo hayo tu wanaiba mpaka makubasi na ndala? Wanachana nyavu za madirisha kuiba simu vitochi? Sasa huku Kwetu wako wengi sana, usipo kuwa na ukuta muda wote wewe lazima uwe na tahadhari. Ukuta unapunguza hadi 90% ya usumbufu wa Hawa vibaka wadogo.

Kwa Hali ya hewa Dar ni kweli kabisa kujenga ukuta ilitakiwa kupata kibari maalum lakini imebidi tuwe wabunufu kukabiriana na mazingira yetu utuelewe tu .
 
Wabongo ni wazee wakuiga mtu mmoja2 akifanya kitu kijiji kizima lazima kifanye🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…