Kwanini watanzania wanapenda ukuta na mageti?

Kwanini watanzania wanapenda ukuta na mageti?

Wakati nimehamia kwenye kibanda changu nilikuwa sijaweka fence, hakukutokea tukio lolote la kihalifu ila watu walikuwa wanapita hadi karibu na madirisha, yaani eneo lote ni njia.
Nikaweka fence na ndio nikaibiwa! How? Long story.
Kuna rafiki yangu alijenga kwenye hii miji mipya. Akaleta uzungu nyumba yake ramani haina fence inatakiwa ibaki wazi,madirisha hayana grill kabisa. Bonge ya nyumba kila anaepita lazima ageuze shingo.
Siku aliojikuta yeye,mkewe na mtoto wa mwaka mmoja wamelala chini saa tano asubuhi ndio anaamka alihama kesho yake.
Kwahio mtoa mada wote tunapenda nyumba zenye kioo from floor to ceiling bila grill,nyumba iwe na very short hedge fence au isiwe na fence kabisa lakini mazingira hayaruhusu.
 
Ni ubinafsi tu wa mafanikio na kutaka watu wasije Kuelezea shida zao kwako kiurahisi kama tunaamini fence vipi kuhusu camera kazi yake nini na vipi kuhusu walinzi magetini mpaka na mbwa ndani mara nyingi fence inatumika kujificha usionekane kiurahisi ndani mwako.
 
Africa tuna changamoto ya ustaarabu. Kama Huna fensi utapata vituko vingi sana. Eneo lako linaweza kugeuka njia, wizi wa vitu vidogo vidogo maana umasikini ni mkubwa Africa unaweza ukaibiwa hata jungu la ubwabwa kama jiko liko nje.

Pia usalama ni mdogo Africa yani mwenye nyumba silaha kubwa ni ukuta kujilinda na watu wengine.
Pia kuna changamoto ya migogoro ya ardhi kwa kiwango kikubwa. Hata kama eneo limepimwa unaweza kukuta jirani kamega eneo lako ndio mana matajiri wengi wanaanza kujenga kwanza fensi alafu nyumba inafata lengo ni kukwepa migogoro ya ardhi.



Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Siku ukipata hela utajikuta tu umeshajenga ukuta.
Privacy ni muhimu lakini pia unapunguza vibaka na wadokozi wale wanaookota hadi kandambili za mgeni mlangoni
Niliwahi kuibiwa gun boots za mtoto wangu ambazo house girl aliweka kwenye baraza ya nyuma ili adeki pale zilikokuwa zimehifadhiwa saa kumi na moja asubuhi, ghafla akaona kijana mdogo miaka kumi hivi (nyoka) akitambaa kuzifuata na kabla house girl hajaweza hata kupiga kelele nyoka alizinyakua na kukimbia nazo. Baada ya hapo nilijenga ukuta!
 
Niliwahi kuibiwa gun boots za mtoto wangu ambazo house girl aliweka kwenye baraza ya nyuma ili adeki pale zilikokuwa zimehifadhiwa saa kumi na moja asubuhi, ghafla akaona kijana mdogo miaka kumi hivi (nyoka) akitambaa kuzifuata na kabla house girl hajaweza hata kupiga kelele nyoka alizinyakua na kukimbia nazo. Baada ya hapo nilijenga ukuta!
Hili ni mojawapo ya matukio mengi
 
Ukienda nchi za Ulaya na Marekani, nyumba zimepangwa eneo la wazi na hakuna uzio wa ukuta wala machuma.

Nyumba zenyewe za mbao, wanaishi kirahisi sana.

Ukija Tanganyika, nyumba zimejengwa kwa uzio wa zege na machuma, ati ndio maisha ya kisasa!

Kila mwenye hela lazima ajenge liukuta refu na mazege juu. Na siku hizi wamejikita kujenga MISAUZI basi unakuta jumba refuu lina manondo kama yote.

Mwanzoni nilijua ni swala la kiusalama kumbe la hasha. Ukienda Ulaya na Marekani kuna matishio makubwa zaidi tena ya silaha za moto.

Tanganyika wala hakuna tishio lolote zaidi ya vipanya vichache ambavyo vinashughulikiwa kikamilifu.

Sasa yale makuta marefu na mageti ya chuma huko Tanganyika ni USHAMBA au hofu ya kisichojulikana?
Broo Tanganyika Nchi Gani huyo[emoji1787][emoji1787]
 
Nazidi kupata mlari! Leo vibaka wamepita na kuku zangu tatu.

Nikizipata noti nitafunga mipaka na majirani
 
Trespass kwa America ni Criminal Case kubwa ukipita nyumba ya mtu unaweza kupigwa risasi.
Tanzania hatuna utaratibu huo ndo maana watu wanajenga fensi
Hata huko pia kuna gate community ingia YouTube utaona.

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
Unapo andk " Trespass" unamaansh nn
 
Ninacho hisi risk ya Nyumba ya Fensi mnaweza kutekwa wote Kimyah Kimyah na majiran wakaja kujua after wiki
 
Ukija Tanganyika, nyumba zimejengwa kwa uzio wa zege na machuma, ati ndio maisha ya kisasa!
😂😂😂 Utakua haujawahi kupigwa tukio la Mwaka wewe sio uzio tu na machumachuma na Mlinzi juu anawekwa yaan pamoja na uzio, machuma geti kubwa, CCTV camera, fences za waya wa umeme, na Mlinzi anawekwa getini ndio utaelewa wanamaanisha nini, mtu analala ndani na million 900 unataka afanyaje akae kizembe afundishwe adabu mjini?
 
Ninacho hisi risk ya Nyumba ya Fensi mnaweza kutekwa wote Kimyah Kimyah na majiran wakaja kujua after wiki
Hakuna kitu km hicho kuna nyumba zina zaidi ya Ulinzi sio ukuta tu na geti kubwa technology imekua sana tembea uone, usione tu zimekaa kizembe zingine zimefungwa mpaka IoT (Internet of Things) na haujui kwa hio jichanganye usimuliwe kumbe unaonwa tu yaan usije ukahisi hivyo hata kidogo
 
Kibongo bongo, ukuta na mageti ni muhimu..
Kwanza kuna udokozi wa kijinga mnoo.
 
Back
Top Bottom