Kwanini watanzania wanapuuza ndugu zao kwenye shida zinazowaua, lakini huwa na umoja misibani?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Inaweza kuwa mtu hana chakula, kaomba msaada wa chakula kwa kaka, dada au ndugu zake lakini bila bila, afe sasa !! hata kama msiba upo mtwara, ndugu waliopo kagera watafika na kuchangia .

Inaweza kuwa ni ugonjwa, mgonjwa kaomba msaada wa matibabu lakini anafungiwa vioo, ni mpaka afe ndio ndugu watakuja kuomboleza utadhani walikuwa wanamsaidia
 
Tukiwasaidia ktk shida zenu za kimasikini ugonjwa ada au kodi hamtutangazi mkaishia kusifia miungu yenu... Ila tukiwachangia hela ya jeneza na msiba mnatushukuru kwa wema wetu....
Kama hujanielewa subiri ukifa utanielewa
 
Watu wanapenda kujitoa kwenye matatizo ya mara moja limeisha. Matibabu, ada, chakula ni matatizo endelevu, wengi hawana moyo wa kuyabeba mpaka mwisho.

Ukibahatika kuwa na ndugu wanaoshikamana kwenye matatizo endelevu mshukuru Mungu.
 
Tukiwasaidia ktk shida zenu za kimasikini ugonjwa ada au kodi hamtutangazi mkaishia kusifia miungu yenu... Ila tukiwachangia hela ya jeneza na msiba mnatushukuru kwa wema wetu....
Kama hujanielewa subiri ukifa utanielewa
hahah... unapenda kutangazwa mkuu
 
Sijui zamani, ila kwa sasa ndugu wa familia au ukoo fulani hawaelewani kabisa na hawasaidiani. Hivyo huchangia misibani kuondoa aibu tu, wasionekane wabaya.

Pili, ndugu wengi wanawivu na ubinafsi, mtu anawaza nimchangieje ada mtoto wa mwenzangu wakati watoto wangu hawajafaulu kuendelea na masomo? n.k
 
Tanzania hali ngumu sanaa- ifahamike ivyo Mkuu

Hapo kwenye kutomsaidia mtu kwenye matatizo mtu anakuwa hana kitu mkuu, tuachane na wale wanacho alaf awataki kusaidia, wengi hali ngumu mkuu, sema ukitokea msiba mtu anakuwa hana budi atakopa ataiba ili afike msibani ila kiuhalisia hali mbaya sanaa tanzania kila mtu anajitosha mwenyewe

Familia za kipato cha chini ni nyingi sana, kulinganisha na kipato cha kati na cha juu
 
Inaweza kuwa mtu hana chakula, kaomba msaada wa chakula kwa kaka, dada au ndugu zake lakini bila bila, afe sasa !! hata kama msiba upo mtwara, ndugu waliopo kagera watafika na kuchangia .

Inaweza kuwa ni ugonjwa, mgonjwa kaomba msaada wa matibabu lakini anafungiwa vioo, ni mpaka afe ndio ndugu watakuja kuomboleza utadhani walikuwa wanamsaidia
Simple: Kwa sababu ukiumwa ni shida yako ila ukifa ni shida yetu.
 
Ukifa unakufa Mara moja imeisha.
Matibabu ni endelevu halafu hayana guarantee.
Hatuwez tupa pesa mingi AF usipopona huon ni loss .
Pesa tutajengea kaburi na chakula msibani
#TUSIOGOPEKUFA
 
Tukiwasaidia ktk shida zenu za kimasikini ugonjwa ada au kodi hamtutangazi mkaishia kusifia miungu yenu... Ila tukiwachangia hela ya jeneza na msiba mnatushukuru kwa wema wetu....
Kama hujanielewa subiri ukifa utanielewa
Unaookuwa huna la kuandika ni bora kukaa kimya!

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Shida apo ni upendo hakuna , kila mtu ni ndugu yako na ni wewe ukisaidia mwingne umejisaidia wewe , dini ya kwel ni upendo tu hakuna nyingne.
 
Nilipokuwa mdogo ilikuwa pale mtaani kila tajiri au mtu mwenye kazi nzuri hapatikani na ndugu zake na nilikuwa na mawazo kama ya kwako ila nilipokuja kupataka kazi ndio nimejua kwa nn ndugu wengi ambao wapo vizuri kiuchumi hawapatani na ndugu zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaweza kuwa mtu hana chakula, kaomba msaada wa chakula kwa kaka, dada au ndugu zake lakini bila bila, afe sasa !! hata kama msiba upo mtwara, ndugu waliopo kagera watafika na kuchangia .

Inaweza kuwa ni ugonjwa, mgonjwa kaomba msaada wa matibabu lakini anafungiwa vioo, ni mpaka afe ndio ndugu watakuja kuomboleza utadhani walikuwa wanamsaidia
Kusaidiana jambo jema sana,tatizo linaanzia pale unamasaidia mtu anakuja kukuharibia life lako Kwa njia zingine ndo lilishawafanya watu waacha kabisa kusaidia wengine yalishatutokea hayo,
 
Back
Top Bottom