Kwanini Watanzania wengi sana wanachanganya L na R?

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Nilikuwa siamini ila sasa nimejionea mwenyewe. Wakenya walipokuwa wakituambia Watanzania kwamba hatujui Kiingereza, tulikuwa tukiwajibu wao kuwa hawajui Kiswahili. Lakini Wakenya nao wakawa wanatusema Watanzania pia hatujui Kiswahili kwa sababu tunachanganya sana L na R. Kiuhalisia nilikuwa siamini, ila tangu nianze kufuatilia comments za Watanzania nimegundua ni kweli. Watu wengi sana hawajui wapi watumie L na wapi watumie R

Leo nimekuta comment mtu anasema "Balabala yenyewe hamjapiga lami hata lobo"
Mtu anaandika Laisi, hajaludi, razima, rafudhi, rugha, talumbeta, kuhalibika, tayali, langi, balabala, lobo, rakini, harafu, lafiki nk
 
Half education is more dangerous than no education.

Walielimishwa kidogo sana juu ya herufi R na L; S,TH na DH. Pia hawajihangaisha kujisomea habari, hadithi n.k ili kuelewa spelling za maneno yenye kutumia herufi hizo.

Kuna wengine kama Wasukuma, Wakurya, Wahaya, Waha, Wabena, Wanyakyusa n.k tuna matatizo yetu ya kiasili katika matamshi ya baadhi ya herufu na maneno.
Lobo (robo), Irara (Ilala), ine (nne), syuka (shuka), ngombe (ng'ombe).
 
Hili tatizo limeanzia miaka ya 1990 kuja juu nadhani kutokana na walimu wa UPE waliokuwa hawana weledi pamoja na elimu ya ufundishaji kuwa duni.

Zamani enzi zetu ilikuwa hauwezi kukuta mwanafunzi shuleni kwenye somo la kiswahili/kingereza akaweza kukojolea sarufi katika kutunga sentensi.

Maana mboko utakazolambwa kwa kosa hilo, huwezi kamwe kusahau na kurudia kosa.
 
Kuna watu wanaochanganya A na H pia, harufu, mtu anaandika arufu. Hapo ukikutana na mtu ambaye anachanganya vyote tu A na H pamoja na L na R, harufu inakuwa 'alufu'
 
Walimu wa sasahivi primary wafundishe watoto mapema wasichanganye hizo herufi ili ikifika miaka ijayo hili tatizo lipungue
 
Halafu na alafu
Upo na hupo
 
Tatizo la taifa ,hata A na H.
 
Watanzania wengi hawajui kusoma na kuandika.

Hata hapa JF utaona.

Takwimu za serikali, ambazo nazo pia zimechakachuliwa kuwa bora zaidi ya uhalisia, zinaonesha kuna mikoa asilimia ya watu wanaojua kusoma na kuandika, hususan wanawake, ipo around 75.

75% literacy, maana yake katika kila watu wanne, mmoja hajui kusoma na kuandika.

Na hapo tunaongelea kujua kusoma na kuandika kwa viwango, ukiongelea wanaojua kusoma na kuandika bila kufikisha viwango, utakuta wanaongezeka zaidi.

Unaweza kukuta pengine ni mtu mmoja katika wanne tu ndiye anajua kusoma kwa ufahamu (reading with comprehension) na kuandika kwa usahihi. I am not even going to get into abstract and logical thinking, that will be too much to ask for.

Ukienda kwenye numeracy huko sishangai ikiwa mmoja katika kumi ndiye yupo numerate.

Tatizo si Kiswahili, Watanzania wengi hawajui kusoma na kuandika katika lugha yoyote.

Na ukiangalia takwimu, miaka ya nyuma tulijitahidi kidogo. Enzi za Nyerere, hususan kwenye elimu ya watu wazima, Tanzania ilikaribia 100% literacy. Mpaka bibi wazee walifundishwa kusoma na kuandika wakaweza.

Maana yake tunavyozidi kuzaliana kwa style ya "nchi kubwa hii, bado ina mapori mengi, tuzaliane tulime" tunazidi kuzalisha masikini wajinga, na wao watazaa wajinga zaidi, tatizo linazidi.
 

Mi nikikuta mtu anaandika hivyo automatikale napata hamu ya kumbloku fasta.
Nikadhani unapataga hamu ya hisia mkuu!
Maana kuna watu huhemkwa wakikutana na wadhaifu, wao huita 'mnyonge wangu'πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ˜„.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…