Kwanini Watanzania wengi sana wanachanganya L na R?

Kwanini Watanzania wengi sana wanachanganya L na R?

Unapataga?!! Na hili ni tatizo kubwa.
Unaendaga.
Unukujaga.
Unalalaga.
Unakulaga.
..........
............
Sioni kama zina tatizo izo -ga zinaonyesha kitendo kinachojirudia au endelevu
 
Pia kumbuka watanzania wapo wa jamii tofauti na utofauti wao huleta tofauti ya matamshi kwa jamii moja na nyingine mf WACHAGA,WABENA,WALUGURU hutumia sana R badala ya L na watu wa PWANI hutumia sana L badala ya R
Hio kutumia L badala ya R weka Wakurya wachaga hawana izo changamoto ndogo ndogo
 
Uzuri hakuna matatizo yoyote yanayojitokeza mtu akishindwa kutumia L,R,S,TH,DH,G,J kwenye mazungumzo pia hata uko ULAYA waliotuletea haya maandishi hukumbwa na tofauti hizo KIKUBWA TWAELEWANA 1000%
 
Tukumbuke pia 80% ya watanzania ni jamii tofauti pia kuna matamshi na maneno mengine yapo kwa matumizi ya KIMOMBO ingawaje utamkwaji ni sawa kwa waswahili( NA HUU NDIO UBANTU WENYEWE WALA KAKUNA SHIDA)
 
Pia kumbuka watanzania wapo wa jamii tofauti na utofauti wao huleta tofauti ya matamshi kwa jamii moja na nyingine mf WACHAGA,WABENA,WALUGURU hutumia sana R badala ya L na watu wa PWANI hutumia sana L badala ya R
Ujinga wa kujiendekeza tu.

Kuna jitu likiongea au kuandika unajua kabisa hili ni ZWAZWA.
 
Lugha yetu ya Kiswahili kwa asilimia kubwa ni ya Kibantu. Humu nchini tuna makabila zaidi ya 120 yenye lugha zao, herufi zao na jinsi wanavyo ongea hizo herufi tajwa. Cha msingi ni kuelewa maana ya ujumbe unaotolewa.
 
Hawa watu ndio waliopo kwenye taasisi za serikali na binafsi
Unamuandikia jina lako kamili anashindwa hata ku copy
Kuanzia passports, Nida, bima na hata vyeti vya ndoa na kwenye line za simu.
Unaanza kuhangaika tena kuomba warekebishe.
Hili ni tatizo kubwa kwenye elimu
 
Nilikuwa siamini ila sasa nimejionea mwenyewe. Wakenya walipokuwa wakituambia Watanzania kwamba hatujui Kiingereza, tulikuwa tukiwajibu wao kuwa hawajui Kiswahili. Lakini Wakenya nao wakawa wanatusema Watanzania pia hatujui Kiswahili kwa sababu tunachanganya sana L na R. Kiuhalisia nilikuwa siamini, ila tangu nianze kufuatilia comments za Watanzania nimegundua ni kweli. Watu wengi sana hawajui wapi watumie L na wapi watumie R

Leo nimekuta comment mtu anasema "Balabala yenyewe hamjapiga lami hata lobo"
Mtu anaandika Laisi, hajaludi, razima, rafudhi, rugha, talumbeta, kuhalibika, tayali, langi, balabala, lobo, rakini, harafu, lafiki nk
View attachment 3703193View attachment 3703194
Ukiwafuma wakate makofi.Huruma siyo malezi.
 
Tukumbuke pia 80% ya watanzania ni jamii tofauti pia kuna matamshi na maneno mengine yapo kwa matumizi ya KIMOMBO ingawaje utamkwaji ni sawa kwa waswahili( NA HUU NDIO UBANTU WENYEWE WALA KAKUNA SHIDA)
Usipende kuhalalisha ujinga, lugha lazima iandikwe na kutamkwa kwa usahihi. Ndio maana watu wanaenda shule.

Nakubali kuna accent tofauti, ila huwezi kusema mtu ashindwe kuandika kwa ufasaha kisa anaathiriwa na kabila lake.
 
Hili tatizo limeanzia miaka ya 1990 kuja juu nadhani kutokana na walimu wa UPE waliokuwa hawana weledi pamoja na elimu ya ufundishaji kuwa duni.

Zamani enzi zetu ilikuwa hauwezi kukuta mwanafunzi shuleni kwenye somo la kiswahili/kingereza akaweza kukojolea sarufi katika kutunga sentensi.

Maana mboko utakazolambwa kwa kosa hilo, huwezi kamwe kusahau na kurudia kosa.
Walimu wa UPE ndio walikuwa wanafundisha sasa sio hawa wa kizazi hiki
 
Acha kujifanya mjuaji hizo L na R ni kwaajiri ya kiingeleza tu
 
Je wewe kujua matumizi ya L,R na nyingine zimekupa mchongo au kukunyima nini kwenye jamii ya kitanzania au ww ni mzungu umekuta kiswahili ulichofundishwa uko ulaya ni tofauti na waswahili wenyewe wanavyokizungumza na kukiandika?
 
Nilikuwa siamini ila sasa nimejionea mwenyewe. Wakenya walipokuwa wakituambia Watanzania kwamba hatujui Kiingereza, tulikuwa tukiwajibu wao kuwa hawajui Kiswahili. Lakini Wakenya nao wakawa wanatusema Watanzania pia hatujui Kiswahili kwa sababu tunachanganya sana L na R. Kiuhalisia nilikuwa siamini, ila tangu nianze kufuatilia comments za Watanzania nimegundua ni kweli. Watu wengi sana hawajui wapi watumie L na wapi watumie R

Leo nimekuta comment mtu anasema "Balabala yenyewe hamjapiga lami hata lobo"
Mtu anaandika Laisi, hajaludi, razima, rafudhi, rugha, talumbeta, kuhalibika, tayali, langi, balabala, lobo, rakini, harafu, lafiki nk
View attachment 3703193View attachment 3703194
Ingia kwenye hii link 👉 Facebook
 
Back
Top Bottom