#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

 

Attachments

  • VID-20210326-WA0012.mp4
    6 MB
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19.
Tuwekee pia nakala ya utafiti ulioufanya.
 
 
Hii kauli ya madaktari kujua inatumika kizushi tu kwa sababu huko hospitali kungekuwa na tahadhari ya hali ya juu kwa sababu wanajua uhalisia ila ndio kwanza wamelegeza masharti, mwanzo ilikuwa huingii bila barakoa ila sasa sio lazima tena halafu ndio useme wansjua kuwa kuna corona? Hata ile kamati basi ingetuambia vitu kama hivyo ila wapi.
 
Mie sijawahi kuzungumza hivyo vitu, halafu cha ajabu bongo huku huwa mnasema corona ni ugonjwa wa kuja na kuondoka ndio sababu sasa bongo inaonekana hakuna corona ila huko vaccine ndio mnaisimia kuondoa maambukizi.
Hujaelewa..... Chanjo sio mpaka ugonjwa uwepo ila unajihami kabla ya mlipuko kufika.

Ila ningeomba maoni yako juu ya ugonjwa kupungua nchi kma UK na Israel baada ya chanjo kuzagaa zaidi ya 60% ya population.
 
Hujaelewa..... Chanjo sio mpaka ugonjwa uwepo ila unajihami kabla ya mlipuko kufika.

Ila ningeomba maoni yako juu ya ugonjwa kupungua nchi kma UK na Israel baada ya chanjo kuzagaa zaidi ya 60% ya population.
Sasa si ndio nimekwambia Tanzania tukisema mbona tunakusanyana tu na hatuoni kinachotokea huwa mnajibu kuwa corona ni ugonjwa wa kuja na kuondoka kwa maana sasa umepungua na bila ya chanjo, ila huko kwa wenzetu mnatuambia chanjo ndio zimepunguza maambukizi na si kwamba corona ni ugonjwa wa kuja na kuondoka.
 
Nimemsikia dakatari kutoka MAT(Mwenyekiti wao) alikuwa anahojiwa na Azam alikiri kabisa kwamba wana wagonjwa wa corona.....Swala la kujilinda ni jikumu la mtu mwenyewe ,kila siku wanatoa matangazo jinsi ya kujikinga na malaria lakini kuna watu bado wanalala bila net ,kulala bila net hakumaanishi kwamba hakuna malaria.
 
Huu ujinga kauleta jiwe
 
Nionavyo mimi, wanaokataa chanjo hawana sababu zozote za msingi, isipokuwa waliaminishwa kwamba chanjo zinatulenga sisi kwenye vita ya kiuchumi na ndiyo maana baadhi ya watu wakaanza kuwa na mtazamo hasi na kuamini kuwa waliogundua chanjo hawana nia njema nasi. Lakini ukimuuliza mtu yeyote anayekataa chanjo kama ana ushahidi wowote wa kisayansi (na siyo ramli) hakuna mwenye huo ushahidi kwamba chanjo wanayoikataa ina madhara gani kwao. Baadhi wanapinga kutokana tu na 'ignorance' na hasa kwa sababu ya kudanganywa na wao kudanganyika kwa sababu mpaka leo hii watoto wao bado wanapata chanjo ambazo hazikugunduliwa hapa nchini, lakini hakuna aliyewahi kupinga chanjo ya surua, porlio, tetekuwanga nk. Jambo la kuzingatia ni kwamba tunaposhauriwa na wataalamu wa afya tuwe na 'trust' kwa mambo ambayo yako juu ya uwezo wetu na kama tukikataa jambo angalau tuwe na sababu za msingi za kufanya hivyo na siyo tu kufuata mkumbo wa watu wenye mtazamo hasi kuhusu utafiti ambao umefanywa na wataalamu kama wa Shirika la Afya Duniani. Tujifunze kufanya mambo kisayansi na tutafika mbali kuliko kukalia kupiga ramli.
 
Hili la chanjo ni jambo tata kidogo, limekaa ktk sura ya hiari ila ndani yake kuna ulazima flani kwa wenye mataifa yao.
Tunaweza kuamua kama nchi tukakataa huo ulazima na ikabaki katika uhiari kwa mwenye kutaka, ila kama jambo hili ni mkakati wa wenye mataifa yao tusitegemee kupata viza bila chanjo, na hapo ndipo ulazima wa wenye jambo lao unapo chukuwa nafasi.
 
Nazungumzia huko hospitali ambako kulikuwa na masharti ya kutokuingia bila barakoa na kunawa mikono kwa sababu ya corona ila sasa hakuna hayo masharti.
 
Nazungumzia huko hospitali ambako kulikuwa na masharti ya kutokuingia bila barakoa na kunawa mikono kwa sababu ya corona ila sasa hakuna hayo masharti.

Kwahiyo kama hakuna masharti ina maana ndio ugonjwa hakuna? Mwenyekiti wa Madaktari Tanzania amesema bado kuna wagonjwa wa korona hospital mim na wewe ambao ni mangubaru inakuwaje tubishe?
 
Kwahiyo kama hakuna masharti ina maana ndio ugonjwa hakuna? Mwenyekiti wa Madaktari Tanzania amesema bado kuna wagonjwa wa korona hospital mim na wewe ambao ni mangubaru inakuwaje tubishe?
Hoja ni kwamba huko hospitali ndio wanajua uhalisia wa corona ndio nimeuliza mbona huko hakuna masharti kama zamani na wakati huko ndio kwenye wagonjwa wa corona?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…