Kwanini Watanzania wengi wanashindwa kutofautisha R na L kwenye kuandika Kiswahili na si Kiingereza?

Kwanini Watanzania wengi wanashindwa kutofautisha R na L kwenye kuandika Kiswahili na si Kiingereza?

ukifuatilia vizuri walio wengi ni vilaza hajaenda shule au kama amenda basi ameunga unga na akifuatilia kwa ukaribu maisha yake atakuwa ameishi uswahilini.

Msomi aliye elimika vizuri tungu mwanzo wa elimu kamwe hawezi kushindwa kutofautisha kati ya "R" na "L" chunguza utaona.

ni bora kuanzisha darasa rasmi la kuwafundisha hawa wasio jiweza kutofautisha kati ya " R" na "L"
tena kuwa na mtaala maalum.

hawa ndio wale tunashindwa kuwaelewa mfano;

Lais badala ya Rais
plesident badala ya Presedent.

sasa watu wa aina hiyo unaweza kusema wamesoma kweli?!
 
Ukiona umeshindwa kulitambua hilo jua ww nae pia unamapungufu kichwani.

Anavyo andika kitu tambua ndivyo anavyo kitamka hio utokana na mazingira aliyo kulia lugha mama ya ilo eneo imauwezo mkubwa wa kuathiri kiswahili chake.
Mfano. Sisi tuliokulia maeneo ya Mara si rahis kutumia "l" kwenye kiswahili chetu maana kwenye native language maneno yenye "l" nimachache ama hayapo kabsa kwaiyo wakati wa kujifunza lugha anajifunza kwa rafudhi ya lugha eneo husika
kiingreza pia unashindwa kutambua hizocherufi, mfano land unaweza andika rand, au portfolio uandike portforio
 
kiingreza pia unashindwa kutambua hizocherufi, mfano land unaweza andika rand, au portfolio uandike portforio
Kwenye kuandika atapatia ila amsikilize anapolitamka sasa
 
watu hapa wanaotoa sababu ya lugha ya mama naona hawajaelewa mada. sasa mbona watu hao hao kwenye kiingereza hakosei, mfano football labda aandike footbarr
 
Hamna sababu nyingine zaidi ya kutozingatia somo la Kiswahili..,

huwa namshusha sana hadhi mtu asietamka ama kuandika maneno ya Kiswahili kwa usahihi

kwa kiingereza naweza msamehe labda kasoma Kayumba
Ila Kiswahili no excuse..nakuweka kundi la mtu asie makini
 
ukifuatilia vizuri walio wengi ni vilaza hajaenda shule au kama amenda basi ameunga unga na akifuatilia kwa ukaribu maisha yake atakuwa ameishi uswahilini.

Msomi aliye elimika vizuri tungu mwanzo wa elimu kamwe hawezi kushindwa kutofautisha kati ya "R" na "L" chunguza utaona.
Ukweli mtupu

kuna kuelimika lakini pia exposure

ukiwa msoma vitabu kwa mfano utajua maneno mengi sana kwa usahihi
 
Hili tatizo lipo kwa waTanzania wengi sana hata graduates kwenye kuandika maneno ya kiswahili lakini si Kiingereza.

Mfano graduate hawezi kosea akaandika gladuate, lakini mtu huyo huyo ramli anaweza akaandika lamli, au ramri.

Hivi tatizo ni nini haswa. Hebu wadau nipeni majibu ya maana
kuendekeza uzembe, wengi tumezaliwa huku Kamachumu hata kiswahili shida ila tunaongea fasaha, sasa mulamula anaongea sijui kihaya, kiswahiliaama kingereza.
 
balozi mulamula ameishi Marekani New york miaka na miaka ila hapendi kubadilika kabisa.
Tangu kuteuliwa na CV yake nilikuwa very impressed.,
Ila juzi akisoma Bajeti ya Wizara yake nilikua very dissapointed..was like WTF is this.!!i was in shock kusikia ile Bajeti.,

Namba zinasumbua kusoma si useme Billion 3.567, kuna haja gani kupresent kwa umma vitu visivyoeleweka?

i hope atarekebisha.,haikuwa nzuri kwa kweli
 
Kama Professa aliyeishi Marekani anaongea vile, venacular sasa mimi na wewe tuliosoma chini ya mti na vyo vya kata tutaongeaje?

Just imagine BUNGE ZIMA walikuwa wanalilia kiswahili kitumike kila idara, na hata mahakama, nia si kupigia chapuo lugha ila ni WENGI WAO WANA VYETI ILA KUONGEA HAWAJU.
 
Ni msiba mkubwa kwa kweli.,
 
Hili tatizo lipo kwa Watanzania wengi sana hata graduates kwenye kuandika maneno ya kiswahili lakini si Kiingereza.

Mfano graduate hawezi kosea akaandika gladuate, lakini mtu huyo huyo ramli anaweza akaandika lamli, au ramri.

Hivi tatizo ni nini haswa. Hebu wadau nipeni majibu ya maana
Ukisiliza waimbaji wa kizazi kipya nao wanatatizo hili na pia hawajui thi, dhi, mfano urithi watasema urisi, ridhika watasema rizika n.k.
 
Back
Top Bottom