Kwanini Watawala huwa hawajifunzi kwamba haki ikikosekana kwa muda mrefu, madhara yake huwa ni Makubwa?

Kwanini Watawala huwa hawajifunzi kwamba haki ikikosekana kwa muda mrefu, madhara yake huwa ni Makubwa?

JET SALLI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
2,995
Reaction score
2,047
Ndugu zangu wanajamii Forums,

Mimi ninaamini kwamba hakuna mtu awaye yote asiyependa kutendewa HAKI katika mazingira ambayo anajua kwamba HAKI hiyo ni ya muhimu katika kipindi husika au kwa vipindi vyote kulingana umuhimu wa HAKI hiyo kwake yeye na kwa wengine pia,mm ninaiona kwamba viongozi wa Taifa letu bado wana nafasi ya kujifunza zaidi na kujua umuhimu wa haki.

Ni vizuri viongozi wakaona mbele zaidi na kujua umuhimu wa HAKI kama msingi thabiti wa AMANI.Si vzr Taifa kuwa na viongozi wasiojua kusoma alama za nyakati, maana viongozi wasiojua hayo daima hawayajui maumivu ya watu ktk maisha yao ya kila siku.NI HAKI TU NDIO INAWEZA KUINUA TAIFA NA SI VINGINEVYO.

Si vizuri viongozi kuwaonyesha wananchi kuwa ili wapate HAKI yao lzm waingie barabarani kudai HAKI hiyo. KUNA MSEMO WA KISWAHILI UNAOSEMA MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA. HAKI inapokosekana wananchi wanaona wala hakuna atakae waambia tazama. Kwa miaka mitano wananchi wameadhibiwa kwa makosa yasiyo yao na kwa maneno mengine tunaweza kusema Serikali ya CCM ndio kwa miaka yote imeleta shida kwa watanzania kama ni umaskini wa watanzania basi CCM inahusika moja kwa moja.

Tumefika mahala watu wakichagua viongozi jina lake linakatwa kwa maana hiyo HAKI haipo ktk kuchagua viongozi. CCM na serikali yake itambue kwamba WATU WATAKAPO CHOKA NA KUFIKA KWENYE UKOMO WA UVUMILIVU HATUTAKUWA NA TAIFA LENYE HESHIMA TENA DUNIANI NA KITAKACHOKUWA KIMESABABISHA NI KITENDO CHA KUJIVUA AKILI KWA MAKUSUDI NA KUDHANI KUWA HAKI HUKANYAGWA DAIMA NI WAKATI umefika sasa kujifunza kwa lazima hata kama hatutaki ili kulinusuru TAIFA letu. Ni wakati umefika kuwa na viongozi wanaoshaurika na wanaoweza kujua hatari inayolinyemelea TAIFA.

Tuko katija uchaguzi Ni vizuri Kutoa HAKI KWA WAGOMBEA WOTE. MUNGU ATAKAPO AMUA TUKUMBUKE HATUNA UWEZO WA KUZUIA MAAMUZI YAKE. HAKI, HAKI, HAKI, NDIO KWAYO TAIFA LITAINUKA ZAIDI NA ZAIDI NA KUHESHIMIKA.
 
CCM awamu hii imeliingiza taifa katika record ya hovyo kabisa ever..

Watu kupotea, watu kutekwa, viongozi wa umma kutukanwa live live na wanasiasa wa chama tawala....

Hii ni aibu kubwa..CCM has to go ..!!
 
Tatizo msaliti wa Nchi alikuja kwa pupa
Leo nilikuwa Kanisani. Padre wetu alisoma aya nyingi kutoka Biblia zibazohusu Haki. Alisema kwa mazingira ya sasa ukiisema haki sana unaonekana wewe ni chadema au act wazalendo. Ccm na serikali hawana ujasiri wa kubeba bango la haki.

Ccm haitaki haki, serikali iliyo madarakani haitaki haki kwa kuwa mpaka sasa wameshavunja haki na wanao mpango wa kuivunja katika uchaguzi huu. Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa waliivunja, na hata sasa wanajua fika ndiompango. Hii ni bahati mbaya sana kwa taifa letu.

Nilimpenda Padre wetu bure.
 
Tuna watawala wajinga sana Africa, ni hatari watu hawa na wengi ni mpaka wapigwe mawe ndio wanagutuka, huu ni wakati mzuri sana wa kuondokana nao.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Leo nilikuwa Kanisani. Padre wetu alisoma aya nyingi kutoka Biblia zibazohusu Haki. Alisema kwa mazingira ya sasa ukiisema haki sana unaonekana wewe ni chadema au act wazalendo...
Mkuu nitajie hilo kanisa nije niabudu hapo kisha nitoe zaka na sadaka ili kuunga mkono juhudi za huyo mtumishi wa kweli wa Mungu alie hai! maana siku za hivi karibuni tumekuwa na watumishi wa mungu na allah ambao ni walamba miguu ya watawala.

wako bize kusifia na kuombea watawala ili wajaze matumbo yao binafsi, wamefumbia macho kila aina ya uovu unaotendwa na watawala. Wamesahau majukumu yao ya msingi ya kuisemea HAKI kama tunda la amani ya nchi yetu.
 
Na inasikitisha tunapoona waziwazi viongozi wa dini wakiimba wimbo wa AMANI na wameziba midomo yao isitamke neno HAKI wasijue kwamba maneno ya kulishwa na wanasiasa hayatalisaidia chochote Taifa la Tanzania.

Ni vichekesho taifa lina viongozi wa dini wanafiki.Maandiko matakatifu hayasemi AMANI HUINUA TAIFA na badala yake yanasema HAKI PEKEE NDIO KWAYO TAIFA HUINULIWA.Viongozi wakiambiwa wajifunze pasipo kuleta machafuko hawataki ila wanasubiri wajifunze pakitokea machafuko na tabia hizi za hovyohovyo ziko AFRIKA pekee ambako viongozi wake wengi hawajitambui.

Na baba wa TAIFA aliwahi kusema tabia za kutojali watu zaidi ziko Africa ambako viongozi huonea watu hovyohovyo pasipo kujali HAKI ZAO.
 
Kama ukuwahi soma history mambo ya rise and fall of kingdoms utayajulia wapi haya.
 
Kenge huwa haamini kama kaumia mpaka atolea damu sikioni
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Leo nilikuwa Kanisani. Padre wetu alisoma aya nyingi kutoka Biblia zibazohusu Haki. Alisema kwa mazingira ya sasa ukiisema haki sana unaonekana wewe ni chadema au act wazalendo. Ccm na serikali hawana ujasiri wa kubeba bango la haki. Ccm haitaki haki, serikali iliyo madarakani haitaki haki kwa kuwa mpaka sasa wameshavunja haki na wanao mpango wa kuivunja katika uchaguzi huu. Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa waliivunja, na hata sasa wanajua fika ndiompango. Hii ni bahati mbaya sana kwa taifa letu.
Nilimpenda Padre wetu bure.
Huwezi kuwasikia hata mmoja wao akitaja neno Haki. 😅😅
 
Leo nilikuwa Kanisani. Padre wetu alisoma aya nyingi kutoka Biblia zibazohusu Haki. Alisema kwa mazingira ya sasa ukiisema haki sana unaonekana wewe ni chadema au act wazalendo. Ccm na serikali hawana ujasiri wa kubeba bango la haki. Ccm haitaki haki, serikali iliyo madarakani haitaki haki kwa kuwa mpaka sasa wameshavunja haki na wanao mpango wa kuivunja katika uchaguzi huu. Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa waliivunja, na hata sasa wanajua fika ndiompango. Hii ni bahati mbaya sana kwa taifa letu.
Nilimpenda Padre wetu bure.
There are some powerful people in our country trying to make it difficult for us to vote for Tundu Antipas Lissu. You know why? Because they know when we vote, things change.
 
Back
Top Bottom