youngkato
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 3,811
- 3,888
Wateja wanaingia dukani kwako kila siku, wanakuja dm whatsapp, wanauliza bei, lakini mwisho wa siku, hakuna mauzo yanayofanyika!
Kama wewe ni mfanyabiashara wa duka la nguo na unakutana na hali hii mara kwa mara, basi video hii ni kwa ajili yako. Leo nitakuonyesha sababu kubwa zinazowafanya wateja wasinunue hata baada ya kuonyesha nia, na muhimu zaidi nitakupa mbinu za kufanya biashara yako ivutie zaidi na ifunge mauzo kwa ufanisi.
Tumia mazingira uliyopo, rasilimali ulizonazo, na uanze kuongeza mauzo kila siku.
Tuanzie hapa.
Wateja wanakuja dukani… lakini hawanunui kwa nini?
Hali kama hii inakuacha bila sababu ya pekee ya wateja kuchagua biashara yako. Je, kwa nini mtu achague kununua kwako, ilhali kila kitu kinafanana na jirani yako?
Unaweza kutangaza hadi uchoke, ukatumia hela nyingi kwenye matangazo, lakini watu hawaji si kwa sababu bidhaa zako ni mbaya, bali kwa sababu hawakuamini.
Nikipingwa kuhusu bei, nitajibu nini?
Mteja akinieleza kuwa ana bei nafuu kwingine, nitajitetea vipi?
Akiniahirisha manunuzi, nitamrudishaje kwenye maamuzi?
👉 Kama unahitaji msaada wa kitaalamu kuongeza wateja na mauzo kwenye biashara yako, tuma neno “NAHITAJI KUONGEZA WATEJA” kwenye WhatsApp namba: +255693880325
Tutakusaidia kutengeneza mfumo wa tofauti, utakaoweka biashara yako mbele ya wateja sahihi, na kukuongoza kufunga mauzo bila kupoteza muda.
Kama wewe ni mfanyabiashara wa duka la nguo na unakutana na hali hii mara kwa mara, basi video hii ni kwa ajili yako. Leo nitakuonyesha sababu kubwa zinazowafanya wateja wasinunue hata baada ya kuonyesha nia, na muhimu zaidi nitakupa mbinu za kufanya biashara yako ivutie zaidi na ifunge mauzo kwa ufanisi.
Tumia mazingira uliyopo, rasilimali ulizonazo, na uanze kuongeza mauzo kila siku.
Tuanzie hapa.
Wateja wanakuja dukani… lakini hawanunui kwa nini?
USIIGE WAPINZANI WAKO (TENGENEZA NJIA YAKO MWENYEWE NA ONGEZA MAUZO)
Kuna tabia moja ambayo imezidi kuwaumiza wafanyabiashara wengi: “kuiga wapinzani wao.” Kila kinachofanywa na mwingine, naye anakopi tu. Matokeo yake? Soko linawaona wote kama watu wanaouza bidhaa zilezile, kwa njia ileile, kwa bei ileile.Hali kama hii inakuacha bila sababu ya pekee ya wateja kuchagua biashara yako. Je, kwa nini mtu achague kununua kwako, ilhali kila kitu kinafanana na jirani yako?
Watu Wameshachoka (Tofautisha Biashara Yako)
Watu wengi wamekumbana na matapeli. Wamewahi kuuziwa bidhaa feki. Wamewekeza pesa zao kwenye fursa zisizokuwa halali. Kwa sababu hiyo, wanakuwa waoga kurudia kosa. Hivyo basi, kama mfumo wa biashara yako unafanana na ule wa waliowatapeli, wanakuweka kwenye kundi hilo hilo.Unaweza kutangaza hadi uchoke, ukatumia hela nyingi kwenye matangazo, lakini watu hawaji si kwa sababu bidhaa zako ni mbaya, bali kwa sababu hawakuamini.
Kwa Nini Lazima Uwe Wa Tofauti
Fikiria Grace, aliyetapeliwa baada ya kuagiza viatu mtandaoni. Aliletewa “yebo” badala ya heels. Tangu siku hiyo, hataki kusikia mtu anayeuza mtandaoni. Sasa wewe unaweka post kama za yule aliyemtapeli. Je, unadhani Grace atakufuata? Bila utofauti, utapoteza mteja huyo kabla hata hajakujua vizuri. Jenga mfumo wa kipekee unaoonyesha thamani, usalama, na utofauti ndipo watu waone sababu ya kukupa nafasi.Jinsi ya Kufunga Mauzo (Sio Bahati, Ni Mbinu)
Kama umeshatangaza na watu wameanza kukuinbox, huo ni mwanzo tu. Kazi kubwa ni kuwageuza hawa watu kuwa wateja. Usiwategemee wao tu kuchukua hatua; jifunze namna ya kuwaelekeza kwa ufanisi hadi wafanye maamuzi ya kununua. Bila maarifa haya, utakuwa unapata DM nyingi lakini mauzo yako ni sifuri. Kumbuka: “When you don’t close, you lose.”Kujiandaa Kabla ya Kufunga Mauzo
Kama mtu anavyofanya research kabla ya interview, mfanyabiashara mwerevu hujiandaa kabla ya kuongea na mteja. Jiulize maswali kama:Nikipingwa kuhusu bei, nitajibu nini?
Mteja akinieleza kuwa ana bei nafuu kwingine, nitajitetea vipi?
Akiniahirisha manunuzi, nitamrudishaje kwenye maamuzi?
Udhibiti wa Mazungumzo
Epuka hasira. Sio kila mteja atakuwa mwepesi. Wapo watakaokuchelewesha, wengine watakukera. Lakini kazi yako ni kuwa mpole, kusikiliza, na kuongoza mazungumzo kwa busara. Hakikisha kila mazungumzo yanazunguka tatizo la mteja na suluhisho lako.Mbinu za Kumshawishi Mteja Kuchukua Hatua
Tengeneza Uharaka (Urgency)
Toa ofa ya muda mfupi. Mfano: “Bei ya leo ni 25,000/=, kesho inarudi 40,000/=.” Watu wengi huchelewa kununua kwa sababu huoni haraka yoyote.Tumia Hofu ya Kukosa (FOMO)
Mwambie, “Hii bidhaa imebaki 3 tu.” Mteja ataogopa kuikosa na kuchukua hatua haraka.Tumia Visual Content
Badala ya kuzungumza tu, onyesha picha, video, na shuhuda. Kama unauza sabuni, onyesha ngozi ilivyobadilika kwa mteja aliyeshatumia.Onyesha Kujali
Usimlazimishe mteja ambaye hana hela. Muelewe, mpe muda, na utajenga uaminifu. Atakurudia siku ya malipo.Milikisha (Ownership)
Mteja asikie kama tayari ni wake. Muulize, “Je, rangi ya nguounayopenda ni nyeusi au nyeupe?” Anapoanza kuchagua, tayari kachukua hatua ya kisaikolojia.Jibu Pingamizi kwa Pingamizi
Mteja akisema, “Je, bidhaa zako zitasaidia kupunguza kilo 5?” Usijibu “ndio” tu, bali muulize, “Kama bidhaa yangu itafanya hivyo ndani ya mwezi, uko tayari kuichukua leo?”Fanya Upimaji
Muulize, “Kwa skeli ya 1 hadi 10, unaonaje bidhaa yetu?” Akisema “8”, muulize “kwa nini sio 10?” Hapo utajua kipingamizi chake ni nini, na utashughulikia.Onyesha Behind the Scenes
Mteja akiona unavyoandaa bidhaa zako usafi, vifaa vya kisasa, ubora anaamini zaidi na haoni shida kulipa bei yoyote.Wape Uchaguzi
Badala ya kumuuliza “utanunua au la?”, muulize, “Tukuletee leo au kesho?” Uchaguzi hutoa mwelekeo wa hatua, sio shaka.Sikiliza Sana
Mteja anapenda kusikilizwa kuliko kuuzwa. Uliza maswali. Acha aseme. Acha ajieleze. Utajua anachotaka na namna bora ya kumsaidia.Wape Nafasi ya Kuonja / Kujaribu
Kama bidhaa yako inaruhusu, mpe sample au demo. Kama ni mfumo wa kidigitali, mpe kipindi cha majaribio. Hii huongeza uaminifu na ushawishi.👉 Kama unahitaji msaada wa kitaalamu kuongeza wateja na mauzo kwenye biashara yako, tuma neno “NAHITAJI KUONGEZA WATEJA” kwenye WhatsApp namba: +255693880325
Tutakusaidia kutengeneza mfumo wa tofauti, utakaoweka biashara yako mbele ya wateja sahihi, na kukuongoza kufunga mauzo bila kupoteza muda.