Kwanini watia nia nafasi ya Urais wanaruhusiwa kuonyesha nia zao mapema lakini wagombea ubunge na udiwani wanaonekana kama wanatenda jinai ?

Kwanini watia nia nafasi ya Urais wanaruhusiwa kuonyesha nia zao mapema lakini wagombea ubunge na udiwani wanaonekana kama wanatenda jinai ?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kwanini wagombea urais wanapenda sana wafahamike kwa wananchi mapema zaidi hata mwaka kabla ya uchaguzi lakini ni marufuku kwa watia nia ubunge na udiwani kuonyesha nia zao?

Hali hii ipo kwenye vyama vyote vya siasa nchini na ukanda wa Afrika. Mfano kwa sasa mgombea Urais au mtia nia ACT anafahamika, CCM anafahamika, Chadema wanafahamika pamoja na vyama vingine.

Lakini inapokuja suala la kujitokeza kuonyesha nia kwenye ubunge au udiwani inaonekana ni kigezo cha kukatwa jina. Hii mila na desturi ipo kisheria au ni takwa la viongozi waliopo juu?

Kwa maoni yangu nilitamani watia nia waonyeshe nia angalau mwaka mmoja kabla kuvisaidia vyama kufanya tathmini ya nani anakubalika zaidi na kumpa kipaombele muda wakuteua wagombea unapofika. Naamini kinachotakiwa kupigwa vita siyo kuonyesha nia bali viashiria vya rushwa ndivyo vyakuangaliwa mapema. Na ili kudhibiti watoa rushwa tulipaswa kuwabaini kabla hata ya uteuzi.
 
Back
Top Bottom