Kwanini Watoto wanaaminika 100% wakitoa Ushahidi wao Mahakamani tofauti na Sisi Vijeba / Wazee?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nahitaji sababu ya Kmantiki kabisa iliyoshiba Elimu Kubwa ya Kisaikolojia na Uhalisia wa Moyo, Roho na Akili ( IQ ) ya Mtoto.

Na mkinipa sababu iliyozoeleka na Wengi kuwa Watoto hawaongopi na ni wasema Kweli daima nitaikataa kwani kuna Mtoto leo Kanidanganya kuwa Baba yake ninayemdai hayupo na nikamuona Baba yake huyo Ananichungulia kupitia Dirishani katika Pazia na Macho yake makubwa kama Mapapai ya Tuangoma Bagamoyo.

Ambapo kwa Hasira sasa nimeondoka na Flat Screen yake ambapo nimempa Siku Tatu ( 3 ) tu asiponilipa naiuza ili Nijilipe Deni langu la muda mrefu.
 
Kwahio ulitazamia mtoto aseme "baba kaniambia niseme hayupo""!!!?
 
Niliwahi kushuhudia mtoto anafundishwa ya kusema wakifika polisi ili kuficha alichokifanya uncle wake,, kiukweli nilitamani Ile kesi nikashuhudie mwanzo mwisho ili nimuone malaika yule namna atakavyodanganya na kuaminika
 
Unaleseni ya kukopesha mkuu

Kama huna ,wewe mwenyewe unakesi ya kujibu

Haiwezekani mnaikosesha (TRA) ,serikali mapato kirahisi hivyo

Mkopaji na mkopesshaji wote mnamakosa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…