Kwanini watoto wengi wanapenda wali-maharage?

Kiporo cha wali maharage ni hatari sana..hasa ukipige na chai ya rangi!
 

Sato ni gharama wee tunajua ni tamu sanaa ila maharage chakula cha taifa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi napenda ubwabwa arage mpaka leo na ndevu zangu izi,na my wife anajua kabisa ili nirudi nyumbani mapema bila kupitia ulabu ananitaarifu kabisa Leo wali ndondo...
 
Mie maharage kwa kweli hapana, tangu utoto yalishanishinda, labda niweke nyama na mchuzi wa maharage kidunchu, au samaki na mchuzi wa maharage kidunchu. Ukiona nakula wali maharagwe wenyewe wenyewe jua kabisa sina option ya maisha siku hiyo.

Ndio maana boarding nilikuwa mkondefu wa kuwaza jinsi ya kula mandondo, Shuleni ikitokea kuna muuza mbogamboga za majani ilikuwa lazima niwe mteja wa kudumu. Bora wale ndugu zake maharage akina mbaazi, njegere, dengu, choroko na kunde lakini maharage kwangu big no!
 
Vipi una Ulcers ama hupendi tu maharage?, mimi mbaazi,dengu,choroko duh sitaki bora ndondo tu
 
Naona mnatetea gesi zenu😂
Kitu sato ndani ya sahani na kachumvi kapilipili na limao pembeni 😋😋
Hamjawayi kujua tu

kwangu mimi vyakula bora ni samaki,kuku,mayai,maziwa,maharage,wali
 
Acha kutunyanyapaa wakubwa
 

Kipato cha Mtanzania ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya maharage kutumika kwenye nyumba nyingi. Shuleni huwezi kuwa na bajeti ya nyama kila siku au kila mara kwani uwezo huo haukuwepo, vivyo hivyo kwenye ngazi ya familia, miaka ya nyuma ikipikwa nyama nyumbani ni sherehe ata kwenye familia za wafugaji. Kwa hiyo mimi naweza kusema pamoja na umuhimu wa maharage na vitamin zake kwa ujumla, suala la watoto kupenda maharage ni kwa sababu yapo kila siku ndani, sasa hivi hali hiyo haipo tena kwa kuwa chips , mihogo ya kukaanga,soda, juice, pilau, samaki, vimetamalaki. KWA HIYO UMASIKINI NDIYO ILIKUWA SABABU, UMESAHAU ENZI YA VILAKA KWENYE UNIFORM ZA SHULE NA NGUO ZA NYUMBANI? KUTEMBEA BILA VIATU LILIKUWA JAMBO LA KAWAIDA,PIGA PICHA YA MIAKA YA SABINI UTAKUBALIANA NA MIMI KAMA ULIKUWA UMEKWISHA ZALIWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…