Kwanini watu hawataki kulipia huduma za kuzaa na kwanini Serikali inakubali huu ujinga?

Kwanini watu hawataki kulipia huduma za kuzaa na kwanini Serikali inakubali huu ujinga?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Kwa nini wanawake wanaozaa huwa hawataki kulipa huduma za hospitali za kuzalishwa?
Sababu hasa za watu kutaka huduma za kuzaa kuwa bure ni zipi?
Kwa nini utake watu wagharamikie kuzaa kwako?

Screenshot_20260708-213157~2.jpg
Screenshot_20260708-212956~2.png
 
Wanalalamika kwa Sababu Serikali ndio ilisema watu wa Umri Huo au Rika huko watibiwe Bure kama ujuavyo ahadi ni deni wananchi wanadai haki yao
 
Hakuna mtu aliyeomba kujifungua bure serikali ndio inajitapa kuwa huduma za mama wajawazito ni bure wakati kwa ground hali ni tofauti kabisa. Kama wewe mtoa mada mfano umembebesha mtu mimba ukasikia unadaiwa pesa ya kujifungua wakati kila siku unasikia huduma hiyo inatolewa bure utaelewa?
 
Kwa nini wanawake wanaozaa huwa hawataki kulipa huduma za hospitali za kuzalishwa?
Sababu hasa za watu kutaka huduma za kuzaa kuwa bure ni zipi?
Kwa nini utake watu wagharamikie kuzaa kwako?
View attachment 3625265View attachment 3625266
Iambie serikali yako isichukue kodi zao. Au hujui kazi ya kodi? Mshahara wa daktari na mkunga unatokama na kodi,dawa zinanunuliwa na kodi,zahanati inajengwa na kodi halafu unalazimisha walipie huduma basi usichukue kodi zao.
 
Nchi masikini bhana mawazo ya kimasikini tu aisee hapo kwa Wazulu na ujinga wao mtoto analipwa kwa umri wao wewe unapiga kelele gharama za uzazi Serikali kugharamia inakua tatizo.
 
Hakuna mtu aliyeomba kujifungua bure serikali ndio inajitapa kuwa huduma za mama wajawazito ni bure wakati kwa ground hali ni tofauti kabisa. Kama wewe mtoa mada mfano umembebesha mtu mimba ukasikia unadaiwa pesa ya kujifungua wakati kila siku unasikia huduma hiyo inatolewa bure utaelewa?
kwani nyinyi hamjui kuwa wanasiasa ni walaghai , kwanin mnaendelea kuamini matamko ya kisiasa ?
 
Tatizo ni serikali, inaleta siasa kwenye mambo yanayohitaji uhalisia. Wakienda kwa wananchi ili wanataka kufurahisha umma badala ya kuongea uhalisia. Walishajichanganya, sasa ikirokea mtu anataka kuwaambia wananchi ukweli lazina akutane na upinzani mkubwa, watu walishaaminishwa kujifungua ni bureee
 
ni sawa na kusema ulaya waache ujinga kulipa watu posho ambao hawana ajira
 
😀😄😄

Wewe unafikiri watu hawawezi kuzaa majumbani mwao?
Serikali ndio ilikataza watu kujifungulia majumbani kwa kile kiitwacho kupunguza hatari za vifo vya mama na watoto.

Lakini kuzaa wanawake wengi wanauwezo wa kuzaa nyumbani kwa kutumia wakunga wajadi ambao wengi wao huwa ni ndugu kama wamama, mashangazi na wabibi.

Ni sawa uulize, vijana waliosoma kwa nini wadai ajira kwa serikali.
Ni kwa sababu serikali ndio iliwaambia na kulazimisha elimu kwa watu huku ikitoa ahadi kuwa mtu akipata elimu atapata kazi nzuri na maisha mazuri.
 
Nadhani hujatembelea vijijini ukaona umaskini wa kutisha itoshe tu kusema ikiwa mleta mada una makebo makubwa ulombwe tu maana huna akili
 
Mtoa mada ana mental problem sio bure
 
Back
Top Bottom