Kwanini watu hupendelea kuuliza hili swali kwa watoto?

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
284
Reaction score
912
Mara nyingi mtoto akitoka kwenda kucheza kwa jirani huuliza swali "mmekula nini kwenu? ".

Tabia hii nimeiona mara nyingi kwa wanawake pia imeshamiri sana maeneo ya uswazi na wengine huenda mbali kumuuliza mtoto kwa kumpamba ili awambie ukweli " leo mmekula nini kwenu, mtoto mzuri?

Ni Kwanini watu hupendelea kuuliza hili swali na siyo maswali mengine?
 
Wazazi wa uswazi huwa na tabia ya kutambiana huko kwenye vijiwe vyao. Wengi hujifanya mambo safi ama kuwasifia waume zao kuwa kila siku wakirudi wamebeba vinono. Sasa watoto ndio wajumbe wa haki wasioongopa huongea ukweli bila kujua

Jibu la mtoto ndio humaliza kelele ama ndio huwa mwanzo wa vijembe kejeli na mipasho
Jr[emoji769]
 
[emoji106] [emoji106]
 
Ndio stori za kupiga na mtoto. Mfano naongea na bi mkubwa akasema ongea na huyu aunt yako....aunt mwenyewe ana miaka mitatu nitaongea nae nini?
Ni njia mojawapo ya ku-"break the ice" na mtoto kwa kumuuliza vitu/mada rahisi; umekula?, unaangalia tv?, unacheza?. Mtoto ukianza kumuuliza kuhusu hali ya hewa, siasa na mambo kama hayo siyo rahisi kwake kukujibu.
 
Ni njia mojawapo ya ku-"break the ice" na mtoto kwa kumuuliza vitu/mada rahisi; umekula?, unaangalia tv?, unacheza?. Mtoto ukianza kumuuliza kuhusu hali ya hewa, siasa na mambo kama hayo siyo rahisi kwake kukujibu.
Anataka uanze kumuuliza mtoto vipi hali ya corona huko kwenu? Unamuuliza maswali rahisi umekula nini? Amekupikia nani? Umesoma nini leo? N.k
 
Hata kwenye sim tu, mtu akipewa aongee na mtoto lazima amuulize mtoto swali hilo.
"Sasa watoto ndio wajumbe wa haki wasioongopa huongea ukweli bila kujua
Jibu la mtoto ndio humaliza kelele ama ndio huwa mwanzo wa vijembe kejeli na mipasho"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…