Kwanini watu huwa na tabia ya kuwapinga watu wenye IQ kubwa?

Davidmmarista

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
1,367
Reaction score
2,451
Katika jamii, watu wenye IQ kubwa mara nyingi hukutana na upinzani kutoka kwa wengine. Je, hii inasababishwa na wivu, hofu, kutokueleweka kwa mawazo yao, au ni changamoto ya kijamii?

Je, tatizo liko kwa watu wenye IQ kubwa au kwa jamii inayo
wapinga? Karibu mdau wa JF Tupate maoni yako!
 
Tatizo ni wivu tu mkuu hakuna kingine
 
Watu wenye IQ kubwa wanatakiwa wapingwe kwa njia ya mdahalo, ambapo baada ya majadiliano yenye IQ kubwa kuwekwa mezani, ndipo mnapofikia muafaka na kufanya maamuzi.
Ukiona mtu anapinga tu bila kuwa na 'facts', juwa huyo hajaelimika.​
 
Nadhani ni mitazamo tu inakinzana; mtu typical mtaani kipaumbele chake kimawazo ni pesa, chakula, mavazi na mbususu wakati IQ kubwa inawaza extra mile; itahangaisha ubongo kujua mambo magumu magumu kama vile maana ya maisha yenyewe na sio kuishi tu na kadhalika na kadhalika
Hawa Watu wametwishwa mzigo wa mawazo ambayo sisi wengine hatuwazi lazima mkikutana utaanza kujihisi nyani na utamaindi
 
Hivi wewe una IQ kubwa au ndogo
 

Tupe mfano wa mtu mwenye IQ kubwa kwanza tujue umo au haumo?
 
Sometimes ni wapuuzi. Kama wale wa kusema Mungu hayupo tuwaangalie tu?
 
Kamwe usidharau nguvu ya watu wajinga wanapokuwa pamoja katika makundi makubwa ni hatari sana." — George Carlin
Kama serikali ya mtaa wetu,mwenyekiti na viongozi wengine wanakula hela za michango mtaani lakini jifanye kuhoji kwenye mkutano kama utaungwa mkono na wanakijiji ambao wengi ni wajinga,kila mtu hataki kuonekana mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…