Kwanini watu huwa na tabia ya kuwapinga watu wenye IQ kubwa?

Kwanini watu huwa na tabia ya kuwapinga watu wenye IQ kubwa?

Kuna tabia hawa watu huwa wanakuwa nazo kwenye jamii zetu kwahiyo wengi hujulikana mfano ukitaka kujua mtoto mwenye IQ kubwa hupenda kuuliza maswali mengi sana, hupenda kujitenga pia wanapenda sana debate na kudadisi mambo
Humu nachukiwa sana hawanaga amani mpaka wanagroup lao lakuniteta , nje ya hapa nachukiwa sana sana .
WAnasema najiona sana najua sijui hili lile hata kazini nikamua kujiajiri sasa
 
Kama serikali ya mtaa wetu,mwenyekiti na viongozi wengine wanakula hela za michango mtaani lakini jifanye kuhoji kwenye mkutano kama utaungwa mkono na wanakijiji ambao wengi ni wajinga,kila mtu hataki kuonekana mbaya.
Aise lazima wakuandame na serekali zetu kwa bongo ndio zilivyo hawahitaji kuambiwa ukweli wajiboreshe
 
Nani mwenye IQ kubwa kapingwa? .

Swali limekaa kiufundi nataka nijue kama kweli unawajua watu wenye IQ kubwa
 
Nani mwenye IQ kubwa kapingwa? .

Swali limekaa kiufundi nataka nijue kama kweli unawajua watu wenye IQ kubwa
Philip Emeagwali (Nigeria) – Alisaidia katika kuunda technology ya supercomputers lakini mara nyingi mawazo yake yalipuuzwa mwanzoni na watu.
Njoo kwa Tshilidzi Marwala (South Africa) – Mtaalamu wa AI ambaye mara nyingi mawazo yake yalionekana kuwa ya ajabu kabla ya technology ya AI kuenea naye alipingwa sana.
Nikola Tesla mwenyewe concept zake zilipungwa na watu kama Thomas Edison na watu wengine wengi tu.

Ni viongozi wangapi wenye IQ na maono hupingwa ni wengi hasa hapa Africa
 
Achana na hao Investors, maana kwa sasa hamna anaewapinga, tutajie na hao baadhi ya viongozi wenye IQ kubwa hapa Africa wanaopingwa tuwajue
 
Achana na hao Investors, maana kwa sasa hamna anaewapinga, tutajie na hao baadhi ya viongozi wenye IQ kubwa hapa Africa wanaopingwa tuwajue
Tuanze na mugabe, lucha,mwalimu julius nyerere,sweety candy,nelson mandela,jomo kenyatta,mwinyi wa zamani,mkapa ,huyu kijana wa sasa anavaa kijeshi,kagame,museven,nawapigania uhuru wote .
 
Back
Top Bottom