Kwanini watu huwa na tabia ya kuwapinga watu wenye IQ kubwa?

Maumivu ya kutumia akili katika ulimwengu wa wajinga ni makali sana mkuu.
Basi utumie akili kwenye mambo yako unajua Kuna watu huwa wanalaumu wengine Kwa kufeli kwao kama mtu anajiona ana akili anafeli analaumu watu waliomzunguka
 
Mkuu usikimbilie kuwa wa kwanza kujibu, soma elewa Kisha jibu kwa usahihi.

Hapo umeingizia feelings zako na sio ajabu hata haujaelewa nimeandika nini.

Sijui nimemlaumu nani hapa kwa mambo yangu! 🤔
 
Hapana wapi nmesema umemlaumu mtu au wewe ndo mwenye IQ kubwa.
Ila nilichomaanisha kama wewe una IQ kubwa ya kufanya mambo yako kwanini upate maumivu Kwa sababu ya wajinga wengine badala ya kuchukua hatua Kwa yanayowezekana?
 
Lazima tuweze kutofautisha baina ya IQ na EGO. Mjuvi wa mambo ni mjuvi tu. Na utambaini katika nyanja kuu tatu, ambazo ni:-
1. Namna anavyo wasilisha mawazo yake juu ya jambo flani katika jamii inayomzunguka.
2. Namna anavyo toa msaada(wa mawazo, pesa au nguvu kazi) katika jamii
3. Na namna anavyojiweka katika jamii(staili ya maisha yake), wenye IQ kubwa dhamira/msukumo wao mkubwa ni kuisaidia/kuikwamua jamii kutoka katika mkwamo wa kiuchumi, kijamii na kisiasa.
 
Watu wenye IQ kubwa mara nyingi huwa hawayumbishwi, pili wana misimamo na siyo waoga hivyo hupelekea kuchukiwa.
 
Watu wenyewe IQ kubwa hukutana na upinzani kwasababu wao nanajiona hawana cha kupoteza kwani hujiona wamekamilika kila eneo nahujihisi sio binadamu wa kawaida hvo lazima wakutane na upinzani mfano wewe hapo mtoa mada..pili, watu wenye IQ kubwa hupenda kujichanganya na wenye IQ ndogo hvo lazima wakutane na upinzani kwani mitazamo yao ni tofauti..mfano wewe hapo mtoa mada...nimechoka kubonyeza ngoja niishie hapa japo sababu ni nyingi.
 
Katika jamii, watu wenye IQ kubwa mara nyingi hukutana na upinzani kutoka kwa wengine. Je, hii inasababishwa na wivu, hofu, kutokueleweka kwa mawazo yao, au ni changamoto ya kijamii?

Je, tatizo liko kwa watu wenye IQ kubwa au kwa jamii inayo
wapinga? Karibu mdau wa JF Tupate maoni yako!
I.Q kubwa wengi wao ni introverts. Kuna classmate wangu wa A level yupo hivyo..
 
Kama serikali ya mtaa wetu,mwenyekiti na viongozi wengine wanakula hela za michango mtaani lakini jifanye kuhoji kwenye mkutano kama utaungwa mkono na wanakijiji ambao wengi ni wajinga,kila mtu hataki kuonekana mbaya.
Tena wanaweza kusema kuwa unamuonea wivu ndugu Mwenyekiti. Hovyo sana hao watu.
 
Katika jamii, watu wenye IQ kubwa mara nyingi hukutana na upinzani kutoka kwa wengine. Je, hii inasababishwa na wivu, hofu, kutokueleweka kwa mawazo yao, au ni changamoto ya kijamii?

Je, tatizo liko kwa watu wenye IQ kubwa au kwa jamii inayo
wapinga? Karibu mdau wa JF Tupate maoni yako!
Inferiority Complex leading to Extremely Feeling Jealous !
 
Back
Top Bottom