Kwanini watu wakiacha pesa zao benki kwa muda mrefu akiba yao ndiyo inakatwa badala ya wao kupata faida?

nyundo2017

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2017
Posts
1,439
Reaction score
861
Habarini,

Hiki kitendo cha watu kuweka hela zao benki pasipo kuzitoa kwa muda mrefu halafu benki wanakuwa wanazikata kwa kasi ya 4G wakati benki wanazikopesha kwa watu wenginebkwa riba siyo sawa kabisa ni wizi.

Benki wakate pale tu mtu anapotoa pesa zake lakini mtu asipotoa pesa benki zikakaa kwa muda mrefu basi watoe faida kwa hiyo hela siyo mtu anaweka hela bila kuzitoa benki wanakopesha hizo kwa riba harafu mwenye hela tena yeye ndiyo akatwe.

Benki zinajigamba zinapata faida sana sio kweli zinaibia watu sana hadi watu sasa wanafirisika, hivyo hili liangaliwe upya ikiwezekana kusiwe na makato yoyote kwa hela kukaa benki tu, wao wapate za riba wanazokopesha watu na za mtu anapotoa hela benki na faida itokanayo na riba wagawane benki na mwenye hela.
 
Kuna haja ya elimu ya huduma za kibenki kama sio mambo ya fedha kutiliwa msisitizo kwa watu.
Unapoenda benki, kuna aina tofauti tofauti za akaunt, kila aina ina dhumuni lake na masharti tofauti, mathalan kuna akaunt za kuweka pesa kwa wakati maalum bila kuzitoa, hizo unapata riba baada ya muda mliokubaliana kuwadia. Kuna akaunt za akiba, unaweka pesa kadri unavyopata na kuzitoa wakati wowote unapohitaji, benki nyingi hutoza huduma hii kwa mwezi, kila mwezi utakatwa pesa kwa ajili ya wao kukutunzia pesa zako. Zipo akaunt za aina hii ambazo wewe unawekewa kiasi cha faida kutokana na kiasi cha pesa unachokuwa nacho kwenye akaunt yako.

Endapo utaweka pesa kwa muda mrefu bila kuitoa na akaunt yako ipo kwenye hilo kundi la kukatwa kila mwezi, pesa yako itaendelea kupungua badala ya kuongezeka kadri siku zinavyoenda.

Ni muhimu sana kuelewa aina tofautitofauti za akaunt upate kujua aina gani ya akaunti itakufaa kwa mahitaji yako.
 
Hki ni moja ya sababu kuu inayo avoid financial inclusion Tanzania kwa mabenki yetu.. Most of financial services za benki zetu hazipo affordable kwa raia weng wa chini kiasi kwamba mtu ukianza fikiria garama za kuendesha akaunti ya benk unapata shida... Ebu fikiria mkulima mim nimehangaika nkapata elfu 30, then nkaweka benk kwa ajili ya kunisaidia, mara baada ya miezi mitano kuja kuchukua pesa nakuta salio ni eflu10, hvi kweli kesho utanishawish niendelee kua mteja wako? Hapana kwakwel.... Na hapa ndo maana mitandao ya simu inapiga bao kwakua wao japo wanakua ghali wakati wa kutoa pesa but atleast pesa yako utaikuta ipo palepale.. Mabenki ya Tanzania yajifunze... Ndo maana huwa nasema equity bank wakikaza buti itakuja kua benki kubwa sana mbeleni kwakua services zao zipo cheap sana and reliable...
 
Mwaka jana kuna mtu alipitishia hela yake ktk acc yangu. Wakati tunaenda kuzitoa, tukaelezwa mlolongo mwingi wa makato tukakubaliana na matakwa yao. Baadae mwenyewe nilipiga mahesabu nikaona ktk mil 42 wamekata karibu sh laki mbili kasoro hivi.... Dawa pekee ya hela ni kwenda kuizalisha na sio kuhifadhi benki. Km utaamua kuweka hela bas ni ktk acc za biashara zao
 
Kuna haja ya elimu ya huduma za kibenki kama sio mambo ya fedha kutiliwa msisitizo kwa watu.
Unapoenda benki, kuna aina tofauti tofauti za akaunt, kila aina ina dhumuni lake na masharti tofauti, mathalan kuna akaunt za kuweka pesa kwa wakati maalum bila kuzitoa, hizo unapata riba baada ya muda mliokubaliana kuwadia. Kuna akaunt za akiba, unaweka pesa kadri unavyopata na kuzitoa wakati wowote unapohitaji, benki nyingi hutoza huduma hii kwa mwezi, kila mwezi utakatwa pesa kwa ajili ya wao kukutunzia pesa zako. Zipo akaunt za aina hii ambazo wewe unawekewa kiasi cha faida kutokana na kiasi cha pesa unachokuwa nacho kwenye akaunt yako.

Endapo utaweka pesa kwa muda mrefu bila kuitoa na akaunt yako ipo kwenye hilo kundi la kukatwa kila mwezi, pesa yako itaendelea kupungua badala ya kuongezeka kadri siku zinavyoenda.

Ni muhimu sana kuelewa aina tofautitofauti za akaunt kabla ya kuamua unataka kufungua akaunt ya aina gani.
Kwahiyo wewe unaoona huo utaratibu wa kukata hela kweye akiba ya mtu ambaye kaziacha tu ni sawa?

Siyo kila utaratibu uliowekwa na haya mabenki uko sawa,moja wapo ni huu uondolewe
 
Mtu anayeweka akiba kwaajili ya kudunduliza au kuweka tu asikatwe chochote bwana hao wanaokopa ndiyo wafidieh izo gharama huu ni wizi,hivi ni lini masikini atapata hela za kuweka fixed akaunti ndiyo apate faida wakati hata hela ya kula hana?
 
Sina hela benk Mimi benk yangu ni kibubu. Inategemea account uliyonayo. Hakuna tozo kwenye saving account lakini ukiwa na current account unabidi ilipie huduma kila mwezi.

Wale wa fixed deposit ndiyo wanadnjoy faida ya bank. Uwe na milioni zako mbili ambazo huzhihitaji unatoa cha kwa miaka miwili unakuta ina faida.
 
Ni njia mojawapo ya kuiwezesha bank kujiendesha.
Kama NMB wanakata 1900 kila mwezi kwa personal account.

Unapotaka kuichimbia pesa mwaka mzima kule piga na mahesabu ya makato yao kabisa.

Pia nikukumbushe tu kutoa pesa dirishani ni 4000/= makato ila kwny ATM ni 900/=

Pia kutuma fedha kwa NMB mobile ni gharama zaidi kuliko kuitoa na kuituma kwa njia tofauti na hiyo.

Wengi wetu tunafanya miamala bila kufahamu tozo.
 
Kwahiyo wewe unaoona huo utaratibu wa kukata hela kweye akiba ya mtu ambaye kaziacha tu ni sawa?

Siyo kila utaratibu uliowekwa na haya mabenki uko sawa,moja wapo ni huu uondolewe

Mkuu, sijasema ni sawa, lakini wao wanakutoza pesa kwa ajili ya kukupa huduma ya kukutunzia pesa zako.
Mimi akaunti yangu nakatwa pale nnapoenda kutoa pesa tu, mambo ya makato ya mwisho wa mwezi hayapo.
Ndio maana nikasisitiza kuelewa aina tofautitofauti za akaunti za uendeshaji wake. Nafikiri tumeelewana
 
Hiyo akaunti yako inaendandana na kipato chako,je nani wa hali ya chini anaweza kuweza kuifungua?
 
Sina hela benk Mimi benk yangu ni kibubu. Inategemea account uliyonayo. Hakuna tozo kwenye saving account lakini ukiwa na current account unabidi ilipie huduma kila mwezi.

Wale wa fixed deposit ndiyo wanadnjoy faida ya bank. Uwe na milioni zako mbili ambazo huzhihitaji unatoa cha kwa miaka miwili unakuta ina faida.
Siyo kweli kama una mtu aliye na saving account kaprint bank statement uone makato yaliyomo
 
Hiyo akaunti yako inaendandana na kipato chako,je nani wa hali ya chini anaweza kuweza kuifungua?

Mkuu mbona kama hatuelewani? Nimesema kwa kuwa naelewa akaunti zinavyoendeshwa, akaunti yangu sikatwi makato ya kila mwezi. Nikiweka elfu kumi 10,000 leo, ntaikuta hivyohivyo hata baada ya miaka mitano, ila nikitoa ndio nakatwa gharama za kutoa.

Kuna benki nyingin siku hizi zimekuja na hizo akaunti, sema kwa watu wengi kutokuelewa, wanafungua akaunti zenye gharama kubwa kuziendesha, sio rafiki kabisa kwa mwananchi wa kawaida.
 
Maandazi na chapati tayari nije kuchukua nifungue kinywa?

Kibubu kizuri sema sasa huku kwa mtogole vibaka hawakawii kuondoka nacho.
Una kuweka kwenye jumu ndani ya gunia juu unaweka mkaa kidogo. Wanaweza kuwaza mama mchafu Huyu analala na mkaa chumbani kumbe akili mu-kichwa.
 
Sina hela benk Mimi benk yangu ni kibubu. Inategemea account uliyonayo. Hakuna tozo kwenye saving account lakini ukiwa na current account unabidi ilipie huduma kila mwezi.

Wale wa fixed deposit ndiyo wanadnjoy faida ya bank. Uwe na milioni zako mbili ambazo huzhihitaji unatoa cha kwa miaka miwili unakuta ina faida.
hata saving account hupata faida pia
 
Kuna haja ya elimu ya huduma za kibenki kama sio mambo ya fedha kutiliwa msisitizo kwa watu.
Unapoenda benki, kuna aina tofauti tofauti za akaunt, kila aina ina dhumuni lake na masharti tofauti, mathalan kuna akaunt za kuweka pesa kwa wakati maalum bila kuzitoa, hizo unapata riba baada ya muda mliokubaliana kuwadia. Kuna akaunt za akiba, unaweka pesa kadri unavyopata na kuzitoa wakati wowote unapohitaji, benki nyingi hutoza huduma hii kwa mwezi, kila mwezi utakatwa pesa kwa ajili ya wao kukutunzia pesa zako. Zipo akaunt za aina hii ambazo wewe unawekewa kiasi cha faida kutokana na kiasi cha pesa unachokuwa nacho kwenye akaunt yako.

Endapo utaweka pesa kwa muda mrefu bila kuitoa na akaunt yako ipo kwenye hilo kundi la kukatwa kila mwezi, pesa yako itaendelea kupungua badala ya kuongezeka kadri siku zinavyoenda.

Ni muhimu sana kuelewa aina tofautitofauti za akaunt kabla ya kuamua unataka kufungua akaunt ya aina gani.
Mkuu, sijasema ni sawa, lakini wao wanakutoza pesa kwa ajili ya kukupa huduma ya kukutunzia pesa zako.
Mimi akaunti yangu nakatwa pale nnapoenda kutoa pesa tu, mambo ya makato ya mwisho wa mwezi hayapo.
Ndio maana nikasisitiza kuelewa aina tofautitofauti za akaunti za uendeshaji wake. Nafikiri tumeelewana
Mkuu mbona kama hatuelewani? Nimesema kwa kuwa naelewa akaunti zinavyoendeshwa, akaunti yangu sikatwi makato ya kila mwezi. Nikiweka elfu kumi 10,000 leo, ntaikuta hivyohivyo hata baada ya miaka mitano, ila nikitoa ndio nakatwa gharama za kutoa.

Kuna benki nyingin siku hizi zimekuja na hizo akaunti, sema kwa watu wengi kutokuelewa, wanafungua akaunti zenye gharama kubwa kuziendesha, sio rafiki kabisa kwa mwananchi wa kawaida.
Hiyo akaunti inaitwaje Mkuu?
 
Hiyo akaunti inaitwaje Mkuu?

Kila benki wana majina yao ila kwa hiyo niliyonayo wanaiita Pay as you go current account (Standard Chartered Bank), unapewa cheque book, unaweza aacha salio hadi TZS 0, makato ni pale unapotoa kwa ATM au kutoa dirishani. Benki nyingi sasa hivi wanakuja na hiyo aina ya akaunt, mfano mwingine ni Equity Bank, wanayo japo wao hawakupi cheque book, na niliwapenda kwenye USD account, ina uendeshaji mdogo sana kwa gharama.
 
Back
Top Bottom