Kwanini watu wakiacha pesa zao benki kwa muda mrefu akiba yao ndiyo inakatwa badala ya wao kupata faida?

Ahsante sana Mkuu.
Nitakusumbua kidogo, naomba uniangalizie hiyo account ya pay as you go current account ya standard chartered, kwenye benki za NMB, CRDB, NBC na DTB kila moja wanaiitaje?
 
Ahsante sana Mkuu.
Nitakusumbua kidogo, naomba uniangalizie hiyo account ya pay as you go current account ya standard chartered, kwenye benki za NMB, CRDB, NBC na DTB kila moja wanaiitaje?

Nikazi kubwa sana mkuu, ila nnachojua ni kuwaambia tu nataka akaunt ambayo haina makato ya kila mwezi, sio kila benki wana hiyo akaunti, wengine hawana.

Kuna nyingine ni nzuri zaidi sema ina masharti kwenye kutoa, unatoa mara nne tu kwa mwaka, lakini unapewa asilimia ya riba kutokana na kiasi unachokua nacho benki. KCB anaiita Simba, hii benki nyingi wanazo ila ndio iwe ya kujiwekea akiba tu na sio ile ambayo utakua unatoa pesa mara kwa mara.
 
Hiyo elimu nani ataitoa sasa....vinginevyo mtu anafungua akaunt apewe elimu kwa style ya kupewa copy ya vigezo na masharti vya akaunti maana kwa wahenga ni kweli hizi akaunti za savings zilikuwa zinatoa riba kidogo hapo zamani za kale japo sio nyingi kama shukurani kwa mteja (nadhani mleta mada ameangalia kwa jicho hilo na yupo katika mtazamo ule wa kale)
 
Asiyeelewa haya maelezo atakuwa haelewi tena.
Nimekusoma Mkuu.
 

Tatizo enzi za wahenga zilivamiwa na wabepari japo hatukuwahi kuambiwa rasmi...mambo ndio yakawa kama yalivyo, unaweka pesa benki na unatozwa gharama za kupewa hiyo huduma. Hapo ndio mitandao ya simu inapokuja kuwa mcharo, ila na wenyewe gharama zao kwenye kutuma na kutoa pesa si haba!!!
 
Hapo sasa ndio kesi inapokua tata! Bado kuna benki zina akaunti rafiki sema ni kutokujua tu. Sasa hivi ushindani w kibiashara ni mkubwa mno, benki nyingi zinataka wateja wa kuweka pesa kwao.
Kuna watu huwa wapo comfortable hata bila akaunti na hela anaingiza hata kama sio nyingi, siku akitaka kupewa hundi ndo unaona anahangaika kufungua a/c
 
Hivi bado mnakomaa kutunza pesa benki, mi zangu nazipitisha hapo tu lakini sizihifadhi hapo, kwa faida gani kwa mfano
 
Hili Nalo La Kutotumia Account Yako Kwa Siku 90
Inafungiwa Yaani Pesa Zako Zinarudishwa Bot Bila Kujari Una Account Gani Iwe Personal Account, Junior Account, Fixed Account

Yaani Usipoweka /Kutoa Kwa Huo Muda Mambo Yanakuwa Magumu Sana Nimekuwa Nikipokea Ujumbe Toka Nmb
Sasa Wana Jamiiforums Ukiweka Bila Mfano Kwa Mwaka Labda Millions Moja Siku Unaihitaji Utaambiwa Na Bank Yako Nenda Bot
 
Benki ya posta ndo yenye gharama kubwa hasa kupitia maxmalipo, si chini ya 5500/= muamala
 
Bank sio mahali salama kwanza wezi watupu bora kuzipitisha tu na kuzitoa tit for tat sipendi umaskini mimi!
 
Uko sawa mkuu, sawa na paspot ya kusafiria, mtu hatafuti hadi siku kuna safari ndio anaanza kukimbizana na uhamiaji.
Alafu anasingizia wanapenda rushwa sana Uhamiaji wakati kama angekuwa anatafuta passport huku ame-relax anakuwa anawachora tu maana kama vielelezo havitoshelezi anafanya kuvitafuta mpaka vinatimia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…