Kwanini watu wakiacha pesa zao benki kwa muda mrefu akiba yao ndiyo inakatwa badala ya wao kupata faida?

Kwanini watu wakiacha pesa zao benki kwa muda mrefu akiba yao ndiyo inakatwa badala ya wao kupata faida?

Kila benki wana majina yao ila kwa hiyo niliyonayo wanaiita Pay as you go current account (Standard Chartered Bank), unapewa cheque book, unaweza aacha salio hadi TZS 0, makato ni pale unapotoa kwa ATM au kutoa dirishani. Benki nyingi sasa hivi wanakuja na hiyo aina ya akaunt, mfano mwingine ni Equity Bank, wanayo japo wao hawakupi cheque book, na niliwapenda kwenye USD account, ina uendeshaji mdogo sana kwa gharama.
Ahsante sana Mkuu.
Nitakusumbua kidogo, naomba uniangalizie hiyo account ya pay as you go current account ya standard chartered, kwenye benki za NMB, CRDB, NBC na DTB kila moja wanaiitaje?
 
Ahsante sana Mkuu.
Nitakusumbua kidogo, naomba uniangalizie hiyo account ya pay as you go current account ya standard chartered, kwenye benki za NMB, CRDB, NBC na DTB kila moja wanaiitaje?

Nikazi kubwa sana mkuu, ila nnachojua ni kuwaambia tu nataka akaunt ambayo haina makato ya kila mwezi, sio kila benki wana hiyo akaunti, wengine hawana.

Kuna nyingine ni nzuri zaidi sema ina masharti kwenye kutoa, unatoa mara nne tu kwa mwaka, lakini unapewa asilimia ya riba kutokana na kiasi unachokua nacho benki. KCB anaiita Simba, hii benki nyingi wanazo ila ndio iwe ya kujiwekea akiba tu na sio ile ambayo utakua unatoa pesa mara kwa mara.
 
Kuna haja ya elimu ya huduma za kibenki kama sio mambo ya fedha kutiliwa msisitizo kwa watu.
Unapoenda benki, kuna aina tofauti tofauti za akaunt, kila aina ina dhumuni lake na masharti tofauti, mathalan kuna akaunt za kuweka pesa kwa wakati maalum bila kuzitoa, hizo unapata riba baada ya muda mliokubaliana kuwadia. Kuna akaunt za akiba, unaweka pesa kadri unavyopata na kuzitoa wakati wowote unapohitaji, benki nyingi hutoza huduma hii kwa mwezi, kila mwezi utakatwa pesa kwa ajili ya wao kukutunzia pesa zako. Zipo akaunt za aina hii ambazo wewe unawekewa kiasi cha faida kutokana na kiasi cha pesa unachokuwa nacho kwenye akaunt yako.

Endapo utaweka pesa kwa muda mrefu bila kuitoa na akaunt yako ipo kwenye hilo kundi la kukatwa kila mwezi, pesa yako itaendelea kupungua badala ya kuongezeka kadri siku zinavyoenda.

Ni muhimu sana kuelewa aina tofautitofauti za akaunt kabla ya kuamua unataka kufungua akaunt ya aina gani.
Hiyo elimu nani ataitoa sasa....vinginevyo mtu anafungua akaunt apewe elimu kwa style ya kupewa copy ya vigezo na masharti vya akaunti maana kwa wahenga ni kweli hizi akaunti za savings zilikuwa zinatoa riba kidogo hapo zamani za kale japo sio nyingi kama shukurani kwa mteja (nadhani mleta mada ameangalia kwa jicho hilo na yupo katika mtazamo ule wa kale)
 
Nikazi kubwa sana mkuu, ila nnachojua ni kuwaambia tu nataka akaunt ambayo haina makato ya kila mwezi, sio kila benki wana hiyo akaunti, wengine hawana.

Kuna nyingine ni nzuri zaidi sema ina masharti kwenye kutoa, unatoa mara nne tu kwa mwaka, lakini unapewa asilimia ya riba kutokana na kiasi unachokua nacho benki. KCB anaiita Simba, hii benki nyingi wanazo ila ndio iwe ya kujiwekea akiba tu na sio ile ambayo utakua unatoa pesa mara kwa mara.
Asiyeelewa haya maelezo atakuwa haelewi tena.
Nimekusoma Mkuu.
 
Hiyo elimu nani ataitoa sasa....vinginevyo mtu anafungua akaunt apewe elimu kwa style ya kupewa copy ya vigezo na masharti vya akaunti maana kwa wahenga ni kweli hizi akaunti za savings zilikuwa zinatoa riba kidogo hapo zamani za kale japo sio nyingi kama shukurani kwa mteja (nadhani mleta mada ameangalia kwa jicho hilo na yupo katika mtazamo ule wa kale)

Tatizo enzi za wahenga zilivamiwa na wabepari japo hatukuwahi kuambiwa rasmi...mambo ndio yakawa kama yalivyo, unaweka pesa benki na unatozwa gharama za kupewa hiyo huduma. Hapo ndio mitandao ya simu inapokuja kuwa mcharo, ila na wenyewe gharama zao kwenye kutuma na kutoa pesa si haba!!!
 
Hapo sasa ndio kesi inapokua tata! Bado kuna benki zina akaunti rafiki sema ni kutokujua tu. Sasa hivi ushindani w kibiashara ni mkubwa mno, benki nyingi zinataka wateja wa kuweka pesa kwao.
Kuna watu huwa wapo comfortable hata bila akaunti na hela anaingiza hata kama sio nyingi, siku akitaka kupewa hundi ndo unaona anahangaika kufungua a/c
 
Habarini,

Hiki kitendo cha watu kuweka hela zao benki pasipo kuzitoa kwa muda mrefu halafu benki wanakuwa wanazikata kwa kasi ya 4G wakati benki wanazikopesha kwa watu wenginebkwa riba siyo sawa kabisa ni wizi.

Benki wakate pale tu mtu anapotoa pesa zake lakini mtu asipotoa pesa benki zikakaa kwa muda mrefu basi watoe faida kwa hiyo hela siyo mtu anaweka hela bila kuzitoa benki wanakopesha hizo kwa riba harafu mwenye hela tena yeye ndiyo akatwe.

Benki zinajigamba zinapata faida sana sio kweli zinaibia watu sana hadi watu sasa wanafirisika, hivyo hili liangaliwe upya ikiwezekana kusiwe na makato yoyote kwa hela kukaa benki tu, wao wapate za riba wanazokopesha watu na za mtu anapotoa hela benki na faida itokanayo na riba wagawane benki na mwenye hela.
Hivi bado mnakomaa kutunza pesa benki, mi zangu nazipitisha hapo tu lakini sizihifadhi hapo, kwa faida gani kwa mfano
 
Hili Nalo La Kutotumia Account Yako Kwa Siku 90
Inafungiwa Yaani Pesa Zako Zinarudishwa Bot Bila Kujari Una Account Gani Iwe Personal Account, Junior Account, Fixed Account

Yaani Usipoweka /Kutoa Kwa Huo Muda Mambo Yanakuwa Magumu Sana Nimekuwa Nikipokea Ujumbe Toka Nmb
Sasa Wana Jamiiforums Ukiweka Bila Mfano Kwa Mwaka Labda Millions Moja Siku Unaihitaji Utaambiwa Na Bank Yako Nenda Bot
 
Ni njia mojawapo ya kuiwezesha bank kujiendesha.
Kama NMB wanakata 1900 kila mwezi kwa personal account.

Unapotaka kuichimbia pesa mwaka mzima kule piga na mahesabu ya makato yao kabisa.

Pia nikukumbushe tu kutoa pesa dirishani ni 4000/= makato ila kwny ATM ni 900/=

Pia kutuma fedha kwa NMB mobile ni gharama zaidi kuliko kuitoa na kuituma kwa njia tofauti na hiyo.

Wengi wetu tunafanya miamala bila kufahamu tozo.
Benki ya posta ndo yenye gharama kubwa hasa kupitia maxmalipo, si chini ya 5500/= muamala
 
Bank sio mahali salama kwanza wezi watupu bora kuzipitisha tu na kuzitoa tit for tat sipendi umaskini mimi!
 
Uko sawa mkuu, sawa na paspot ya kusafiria, mtu hatafuti hadi siku kuna safari ndio anaanza kukimbizana na uhamiaji.
Alafu anasingizia wanapenda rushwa sana Uhamiaji wakati kama angekuwa anatafuta passport huku ame-relax anakuwa anawachora tu maana kama vielelezo havitoshelezi anafanya kuvitafuta mpaka vinatimia
 
Back
Top Bottom