Kwanini watu wakitekwa au kupotea viongozi wa CCM hawakemei au kulaani kwa wakati?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Nadhani viongozi wa CCM wanapaswa kubadili msimamo wao. Kila ikitokea taarifa ya kutekwa au kuuwawa kwa asiye mwana CCM wao ukaa kimya. Kwa kuzingatia umuhimu wa haki ya kuishi niwaombe wabadili response strategy zao na wajitokeze mapema kulaani na kukemea.

Ukimya wa CCM umepelekea hata vyombo vya habari vya serikali na binafsi navyo kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa wakati. Ni kama vile vyombo vya habari vinasuburi kuambiwa nini wafanye.

Tusifungamano na vyama tukapoteza utu; tusikubali kufundishwa roho mbali na ukatili; viongozi wenye roho mbaya wasiwe misingi yetu ya maisha. Tujitenge na wale wanaotumiamisha kwamba wao ndio wenye kujua nani aishi nani afe.
 
Unataka anayewateka nae aje kulalamika? Kweli?
 
Siyo wanakaa kimya tu bali wanafurahia kwani mauaji hayobyanafanywa kwa faida ya CCM
 
HUYU NI MWANA CCM damu damu, lakini amekuwa na MTAZAMO HUU baada ya UCHAGUZI WA 27/11
👇🏽

Ningeingizwa kwenye kamati za CCM ningewashauri,... ni bora wapeleke Proposal kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini taifa lirudi kwenye mfumo wa chama kimoja ili itambulike kimataifa kuliko kuendelea kuamini katika Demokrasia katili inayozidi kuhatarisha maisha na mstakabari wa vizazi vyetu.

Kuuishi unafiki inahitaji kipaji cha asili, japo usalama unabakia kuwa suala la MUHIMU.

Je kama taifa tunaendelea kushuhudia changamoto za mauaji kiasi hiki tena kwa uchaguzi wa serikali za Mitaa tu nchini, uchaguzi ambao hauna mshahara ambao posho ya mwezi ni Tsh 5,000/=, Je udiwani, ubunge na Urais Wana CCM tutegemee kuendelea kuwazika ndugu zetu wa upinzani zaidi au nini tutegemee.

Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa mwaka kesho huenda taswira kamili ikaonekana.

Ila ningewaomba viongozi wa Chama katika Kila nafasi wajitafakari.

Huko CHADEMA kuna dada zetu, Kuna kaka zetu wa heshima, Kuna wajomba zetu yaani kiufupi Kuna Ndugu zetu.

Hii hali itakapokithiri watanzania wakachoka, ipo siku wenye nchi wataiogopa Mitaa na Mitaa itawaadhibu wenyenchi na wananchi watakuwa watawala kisha damu itakuwa ndo jasho la wadai haki... siku yaja, just Mark my Words.

CCM TUJISAHIHISHE
 
Back
Top Bottom