Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,584
- 6,136
Kelly, Kisukuma rahisi sana. Unahitaji tu kukumbuka kuongeza mwisho wa sentesi --MO, au --GA. Hii ni kwa sababu, kwa mfano ukiuliza kama kwenye mtungi kuna maji, Msukuma anakujibu kwa Kisukuma ".. gatimo-MO..". Hivyo kwa Kiswahili kumbuka ili uanze kujifunza, inabidi uwe unasema/andika "...maji hayamo-MO, basi limekuja tumetumbukia-MO". Yeye anakuja-GA, anakwenda-GA.... Ukiweza hayo basi itakuwa mwanzo mzuri.