Kwanini watu wanaendelea kuchukua Mikopo Kausha Damu wakati wengine Wanafilisiwa?

Kwanini watu wanaendelea kuchukua Mikopo Kausha Damu wakati wengine Wanafilisiwa?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Wakuu,

Mikopo kausha damu inapigiwa sana kelele, na tuomeona watu kadhaa wakiathirika na mikopo hiyo, lakini mbali na hayo yote kutokea na kupigiwa kelele kuwa haifai bado watu wanaendelea kukopa na wahanga wanaongezeka!

Kwanini watu wanaendelea kuchukua mikopo hii mbali na athari wanazopata kutokana nayo?
 
Wengine wanasukumwa na tamaa ya kunia makubwa kuliko uwezo wao.
 
Kujilinganisha maisha na wengine ni tatizo kubwa sana.

Ndiyo hupelekea yote hayo kutafuta ku maintain status fulani ya maisha ambayo iko juu ya uwezo wa mtu.
 
Ni changamoto tu za kimaisha ndizo zinazowasukuma watu kuchukua hiyo mikopo.
 
Huu mkopo umekuwepo kwa muda sana Ila naona kwa sasa ndio umegeuka content kwenye media kutokana na visa vyake..
Kiufupi inakuzwa kuliko uhalisia
 
Wakuu,

Mikopo kausha damu inapigiwa sana kelele, na tuomeona watu kadhaa wakiathirika na mikopo hiyo, lakini mbali na hayo yote kutokea na kupigiwa kelele kuwa haifai bado watu wanaendelea kukopa na wahanga wanaongezeka!

Kwanini watu wanaendelea kuchukua mikopo hii mbali na athari wanazopata kutokana nayo?
Wengi hawajisumbui kusoma na kuelewa masharti husika kwa undani kabla ya kukopa, hivyo hawawezi kujua kama huo mkopo ni kausha damu.

Pale mkopo unapoongezeka kadiri unavyorejesha ndo unagundua ushaingia cha kike
 
Watu wengi hususani kina mama hawana vigezo vya kukopesheka kwenye taasisi rasmi za fedha kama mabenki.

Kule kunahitajika aidha ajira rasmi, biashara iliyosimama tayari, dhamana za Mali zisizohamishika pamoja na wadhamini wa kueleweka.

Unakosa vigezo hivyo wakati una shida halafu unasikia kuna kikundi kikijiridhisha na TV iliyopo geto kwako tu wanakupa mkwanja utalipa kidogo kodogo kila wiki unategemea nn? Kwaio hao wanafata mikopo kausha damu ni vile hawana option tu
 
Back
Top Bottom