Izack Mwanahapa
JF-Expert Member
- Apr 21, 2011
- 497
- 236
Jana Jaji Joseph Sinde Warioba amewasilisha Bungeni Rasimu ya pili ya katiba kwa muda wa masaa manne kwa ustadi na umahiri wa hali ya juu. Amejenga hoja zenye mashiko jajo si lazima kila mtu mtu azikubali kwani watu tunamitazamo tofauti.
Hakuna anayeweza kupinga ukweli kwamba Warioba ni mahiri wa uwasilishaji bila kujali kama unakubaliana au hukubaliani na alichokiwasilisha Bungeni jana. Lakini pia tukumbuke alichokiwasilisha si maoni yake binafsi bali ni ripoti iliyotokana na kazi iliyofanywa na Tume ya Mabadiliko ya katiba yeye aliwasilisha kama mwenyekiti tu na sio kama mmiliki au muandaaji pekee ripoti iliyowasilishwa.
Inashangaza kuona watu wa rika, nyadhifa na kada tofauti wakimshambulia Jaji Warioba kwa kumkejeli yeye binafsi badala ya kujenga hoja mbadala zinazoweza kufifisha hoja za Tume ya mabadiliko ya katiba zilizowasilishwa na Jaji Warioba. Wengine wanafika mbali zaidi na kuamua kumtukana Nguli huyu wa sheria ilhali kiumri watukanao wanaweza kuwa wajukuu wa mze huyu.
Hali hii inaonesha kuwa jamii yetu ina watu wengi waliofilisika sera kichwani ndio maana wanashindwa kupinga hoja kwa hoja badala yake wanaanza kumshambulia mtoa hoja kwa vijembe visivyo na tija. Mtu yeyote anayetaka kulazimisha kusikia anachotaka yeye kusikia ni --------.
Ripoti ya tume ya Warioba si msaafu kama watu wanahoja mbadala za kupinga hoja zilizowasilishwa wazieleze wazi badala ya kumvunjia heshima mzee huyu ambaye mara baada ya kuteuliwa kwenye kazi hii kila mtanzania alionesha kuwa na imani naye.
Tusiwe wavivu wa kufikiri kwa kudhani kuwa kumshambulia mtu kutabatilisha uzito wa hoja zake. Sisemi kwamba hoja zake zipo sahihi na hazitakiwi kupingwa, ni nachikisema ni kwamba anayejaribu kupinga hoja za Jaji Warioba basi apinge kwa hoja mbadala badala ya kuanza kumshambulia mtu binafsi (Warioba) kwasababu tu hukubaliani na hoja alizozijenga.
Kamwe huwezi kuzuwia hoja, Hoja inapingwa kwa hoja. Usikubali kubakwa na ushabiki wa vyama. Ripoti ya warioba haijaegemea kwenye chama chochote hata hao CHADEMA wanaunga mkono serikali tatu hoja yao imekuja baada ya Tume ya mabadiliko ya katiba kutoa rasimu ya kwanza ya katiba iliyopendekeza kuwepo kwa serikali tatu hivyo CHADEMA si waasisi au chanzo cha maoni haya wao wamedandia na kuunga mkono jambo hili baada ya kuibuliwa na tume ya mabadiliko ya katiba.
Tuonyeshe umahili wetu wa kukosoa mambo kwa kujenga HOJA mbadala si kuropoka ropoka kwa vijembe na mipasho ambayo haina tija kwa taifa letu. Tuheshimu wazee wetu kwa kutumia lugha za staha katika kuwakosoa.
"TAIFA KWANZA"