Kwanini watu wanamshambulia Jaji Warioba badala ya kupinga hoja zilizowasilishwa kwa hoja mbadala?

Kwanini watu wanamshambulia Jaji Warioba badala ya kupinga hoja zilizowasilishwa kwa hoja mbadala?

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2011
Posts
497
Reaction score
236
Jana Jaji Joseph Sinde Warioba amewasilisha Bungeni Rasimu ya pili ya katiba kwa muda wa masaa manne kwa ustadi na umahiri wa hali ya juu. Amejenga hoja zenye mashiko jajo si lazima kila mtu mtu azikubali kwani watu tunamitazamo tofauti.

Hakuna anayeweza kupinga ukweli kwamba Warioba ni mahiri wa uwasilishaji bila kujali kama unakubaliana au hukubaliani na alichokiwasilisha Bungeni jana. Lakini pia tukumbuke alichokiwasilisha si maoni yake binafsi bali ni ripoti iliyotokana na kazi iliyofanywa na Tume ya Mabadiliko ya katiba yeye aliwasilisha kama mwenyekiti tu na sio kama mmiliki au muandaaji pekee ripoti iliyowasilishwa.

Inashangaza kuona watu wa rika, nyadhifa na kada tofauti wakimshambulia Jaji Warioba kwa kumkejeli yeye binafsi badala ya kujenga hoja mbadala zinazoweza kufifisha hoja za Tume ya mabadiliko ya katiba zilizowasilishwa na Jaji Warioba. Wengine wanafika mbali zaidi na kuamua kumtukana Nguli huyu wa sheria ilhali kiumri watukanao wanaweza kuwa wajukuu wa mze huyu.

Hali hii inaonesha kuwa jamii yetu ina watu wengi waliofilisika sera kichwani ndio maana wanashindwa kupinga hoja kwa hoja badala yake wanaanza kumshambulia mtoa hoja kwa vijembe visivyo na tija. Mtu yeyote anayetaka kulazimisha kusikia anachotaka yeye kusikia ni --------.

Ripoti ya tume ya Warioba si msaafu kama watu wanahoja mbadala za kupinga hoja zilizowasilishwa wazieleze wazi badala ya kumvunjia heshima mzee huyu ambaye mara baada ya kuteuliwa kwenye kazi hii kila mtanzania alionesha kuwa na imani naye.

Tusiwe wavivu wa kufikiri kwa kudhani kuwa kumshambulia mtu kutabatilisha uzito wa hoja zake. Sisemi kwamba hoja zake zipo sahihi na hazitakiwi kupingwa, ni nachikisema ni kwamba anayejaribu kupinga hoja za Jaji Warioba basi apinge kwa hoja mbadala badala ya kuanza kumshambulia mtu binafsi (Warioba) kwasababu tu hukubaliani na hoja alizozijenga.

Kamwe huwezi kuzuwia hoja, Hoja inapingwa kwa hoja. Usikubali kubakwa na ushabiki wa vyama. Ripoti ya warioba haijaegemea kwenye chama chochote hata hao CHADEMA wanaunga mkono serikali tatu hoja yao imekuja baada ya Tume ya mabadiliko ya katiba kutoa rasimu ya kwanza ya katiba iliyopendekeza kuwepo kwa serikali tatu hivyo CHADEMA si waasisi au chanzo cha maoni haya wao wamedandia na kuunga mkono jambo hili baada ya kuibuliwa na tume ya mabadiliko ya katiba.

Tuonyeshe umahili wetu wa kukosoa mambo kwa kujenga HOJA mbadala si kuropoka ropoka kwa vijembe na mipasho ambayo haina tija kwa taifa letu. Tuheshimu wazee wetu kwa kutumia lugha za staha katika kuwakosoa.

"TAIFA KWANZA"

Jaji Warioba.jpg
 
Kama umewasikiliza akina Wasira na Kingunge wakiwa TBC1 wamempinga Warioba kwa hoja. Sema tu hupendi warioba akosolewe. Huwezi kutatua matatizo ya ndoa kwa kuongeza idadi ya wanawake
 
Suluhisho la matatizo haya ni kuwa na nchi moja, serikali zinaweza kuwa hata 10 na uraia uwe mmoja
 
Huo ni ukosefu wa fikra pevu. Jaji ameleta mawazo ya watanzania sasa hao wanaobisha bila sababu za msing wanataka nini? Na wanaomshambulia jaji ni viongoz wa chama fulan cha siasa!
 
Kama umewasikiliza akina Wasira na Kingunge wakiwa TBC1 wamempinga Warioba kwa hoja. Sema tu hupendi warioba akosolewe. Huwezi kutatua matatizo ya ndoa kwa kuongeza idadi ya wanawake

Kilichowasilishwa ni ripoti ya tume ya mabadiliko ya katiba au maoni ya warioba?, Unatakiwa kumpinga Warioba au kupinga hoja zilizowasilishwa na Warioba?
 
Hawana hizo hoja,wamebakia kutoa mifano ya mke. Mke na siasa wapi na wapi?. Siku zote walikua wanaenda kwa kufunikafunika mambo,sasa Ripoti ya Tume imepasua jipu.
 
Rasimu sio maoni ya Warioba bali ni maoni ya Watanzania. Kwani hao majuha Wasira na Kingunge ni kina nani hadi wapinge maoni na matakwa ya watanzania milioni 50???!!!!
 
Kama umewasikiliza akina Wasira na Kingunge wakiwa TBC1 wamempinga Warioba kwa hoja. Sema tu hupendi warioba akosolewe. Huwezi kutatua matatizo ya ndoa kwa kuongeza idadi ya wanawake

Kwanini CCM mnapenda kuulinganisha muungano na ndoa? Kwani kuna aliyetolewa posa?
 
Huwezi kutatua matatizo ya ndoa kwa kuongeza idadi ya wanawake

Huwezi kuendelea kuvumilia mangumi kila siku kwa kisingizio cha cha kulinda ndoa. Iko siku mwili utashindwa kustahamili mangumi ukapoteza roho.

Matatizo au kero Muungano zimedumu kwa miaka miaka 50 na hasa miaka hii 30. Kila mara kamati ambazo zimeundwa kuangalia namna ya kuondoa kero report zao zimepondwa. Na kila mara report hizo zinapotupwa Zanzibar hunyanyuka na kufanya mabadiliko kwenye katiba yao. Sasa hivi katiba ya Zanzibar inamfanya rais wa Muungano kuwz 'ceremonial figure' kule Zanzibar. Katiba ya Zanzibar pia inampa raia wa Tanzania bara hadhi sawa na raia wa Nigeria. Hana haki sawa na Mzanzibari.

Kinguge alikuwa wapi haya yote yakafanyika?
 
Hivi mh kingunge huwa anaongea manake kuanzia ninunue tv na kuangalia bunge huwa namwonaga amelala tu hivi vitu huwezi kuvikuta kwenye nchi za wenzetu ama kweli tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
 
Suluhisho la matatizo haya ni kuwa na nchi moja, serikali zinaweza kuwa hata 10 na uraia uwe mmoja

Hapa umejikanyaga na kuonyesha ushabiki wako wa kitoto. Ni wazi kuwa CCM wanapingana na wananchi waliowaweka madarakani....
 
Ni Tanzania pekee matakwa ya wananchi yanapopuuzwa mfululizo kwa miaka 30 for the expense of tabaka tawala.
 
Suluhisho la matatizo haya ni kuwa na nchi moja, serikali zinaweza kuwa hata 10 na uraia uwe mmoja
Je una uhakika kwamba mpaka sasa tuna nchi moja? (Rejea katiba ya Zanzibar kwa ufafanuzi zaidi)
 
Hoja zipi hizo ndugu yangu ? Hebu nitajie chache tu !

Nimemsikiliza Kingunge leo asubuhi TBC1, yaani anasikitisha kweli yaani niliona aibu kwa niaba yake ! Anapotosha vitu vya wazi as if ni yeye peke yake alimsikia Warioba halafu anatusimulia sisi ambao hatukuwepo !. Warioba ameweka wazi kwamba sasa hivi kikatiba kuna nchi mbili ambalo hata wewe huwezi kupinga !. Kingunge amebaki tu kumlaumu Warioba na kuongea vitu vya jumla jumla tu.....

Kwa sababu najua wewe ni either mwanachama au mshabiki wa CCM, hebu nikuulize swali moja....Hivi kweli mioyoni mwenu, mnafikiri kabisa mtafanikiwa katika kupitisha katiba yenye muundo wa serikali mbili ? Na ni kitu gani haswa kinachowapa kiburi kwamba mtafanikiwa wakati mnachokitaka ni kinyume na maoni ya wananchi ?!

Kama umewasikiliza akina Wasira na Kingunge wakiwa TBC1 wamempinga Warioba kwa hoja. Sema tu hupendi warioba akosolewe. Huwezi kutatua matatizo ya ndoa kwa kuongeza idadi ya wanawake
 
Ni Tanzania pekee matakwa ya wananchi yanapopuuzwa mfululizo kwa miaka 30 for the expense of tabaka tawala.

CCM walijaza wanachama wao kwenye mabaraza ya katiba na wengi wao wamependekeza serikali tatu. Taasis za serikali itokanayo na CCM ikiwemo ofisi ya Waziri mkuu wamependekeza serikali 3.

Kinachoendelea Dodoma ni muendelezo wa vigogo wa CCM kudharau wananchi pamoja na wana-ccm kwenye ngazi za chini.
 
Kama umewasikiliza akina Wasira na Kingunge wakiwa TBC1 wamempinga Warioba kwa hoja. Sema tu hupendi warioba akosolewe. Huwezi kutatua matatizo ya ndoa kwa kuongeza idadi ya wanawake

Chabruma we siasa zitakuweka sehemu mbaya, kwanini iwe kingunge na wasira ndio wampinge mzee Wirioba? Wanaogopa kitu gani? Mzee Warioba alichokiwakilisha jana ni mawazo ya watanzania walio wengi.
 
Kwanini serikali ya ccm inaogopa serikali 3? Kuna kitu gani kikicho nyuma ya pazia? Yaacheni mawazo ya walio wengi yachukue nafasi
 
Kama umewasikiliza akina Wasira na Kingunge wakiwa TBC1 wamempinga Warioba kwa hoja. Sema tu hupendi warioba akosolewe. Huwezi kutatua matatizo ya ndoa kwa kuongeza idadi ya wanawake

Kuongeza idadi ya wanakwake kwa mantiki ya hoja iliyopo mezani ni kuongeza nchi nyingine ya kuungana nayo ni ipi? Kwa maoni yaliyotolewa na wengi na kuingizwa kwenye rasimu , watu wanataka kurekebisha muundo wa muungano na ndoa inabaki vile vile!! Usipotoshe !
 
Kama umewasikiliza akina Wasira na Kingunge wakiwa TBC1 wamempinga Warioba kwa hoja. Sema tu hupendi warioba akosolewe. Huwezi kutatua matatizo ya ndoa kwa kuongeza idadi ya wanawake

Hoja mfu hii! Halafu hao TBC ni bure kabisa wako too biased, kama walitaka kubalance kwa nini wasingemwalika mmoja wa Wajumbe wa iliyokuwa tume ya Mabadiliko ya Katiba nae awape somo! Ni uandishi gani huu wa habari enyi TBC? Kwa nini mko biased kiasi hicho? Munataka kutuambia ni nyinyi tu TBC ndo wenye uchungu na nchi hii? Kwa nini mizania inawashinda, hamjifunz kwa wenzenu hata Kenya tu hapo KBC mbona wanajua kubalance? Tendeni haki bhana, kama maadili wote tumesoma masomo hayo hayo ambayo nyie mumesoma ebhoo!
 
Back
Top Bottom