Kwanini watu wanamuomba na kumshukuru Mungu? Wasipofanya hivyo matokeo yake ni nini?

Kwanini watu wanamuomba na kumshukuru Mungu? Wasipofanya hivyo matokeo yake ni nini?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kwa nini Mungu anataka binadamu wamuabudu, wamuombe, wamtolee sadaka na kumshukuru?

Kama unaamini Mungu yupo ni dhambi usipomuabudu, usipomuomba au usipomshukuru? Yani kama unakubali yupo lakini haufanyi ibada au shukrani yoyote kwake wewe unahesabika ni muovu? Atakufanikishia mambo yako?

Kwa nini wengine anawaambia wasali mara tano kila siku na sio mara kumi, mara moja, kila saa n.k?? Kwa nini wengine wanajiamulia kumuomba wakati wa kuamka, wakati wa kulala na wakati wa baadhi ya matukio tu kama kabla ya kula, kabla ya safari, kabla ya mechi n.k??
 
Kwa nini binadamu tumeletwa duniani?
Kumtumikia na kumwabudu lakini lengo kubwa zaidi ni kutawala viumbe wake wengine Mungu : kinyume na hapo wewe sio mfuasi maana tunaamini usipofanya hivyo lazima utakuwa upande wa shetani ambaye naye yupo anatafuta wafuasi wake
 
Kwa nini Mungu anataka binadamu wamuabudu, wamuombe, wamtolee sadaka na kumshukuru?

Kama unaamini Mungu yupo ni dhambi usipomuabudu, usipomuomba au usipomshukuru? Yani kama unakubali yupo lakini haufanyi ibada au shukrani yoyote kwake wewe unahesabika ni muovu? Atakufanikishia mambo yako?

Kwa nini wengine anawaambia wasali mara tano kila siku na sio mara kumi, mara moja, kila saa n.k?? Kwa nini wengine wanajiamulia kumuomba wakati wa kuamka, wakati wa kulala na wakati wa baadhi ya matukio tu kama kabla ya kula, kabla ya safari, kabla ya mechi n.k??

We hapo mwanao asipokuita baba utajiskia vp au mtoto wako anaamka kila siku bila kukupa salamu, na mda mwingine anaamua tu maamuzi yake
 
Kimsingi shukrani na tahania (gratefulness and appreciation) ni kwa ajili ya manufaa yako mwenyewe. Mtu akikosa shukrani kwa muda, hazipiti siku nyingi ataanza kujiona yeye ndiye kila kitu; amejitosheleza kila idara.

Na akiruhusiwa kuishi zaidi kidogo, atafikia hatua ya kujiona yeye ndiye mungu wake mwenyewe; amejiumba mwenyewe, anaishi kwa nguvu zake mwenyewe, na hivyo anawajibika kwa nafsi yake mwenyewe.

Na huo ndio mwanzo wa majigambo, mashaufu na mineng'eneko isiyo ya sayari hii. Utasikia akitokwa kauli mtambuka kama cogito ergo sum (naishi madhali nafikiri).

Kwa mantiki hiyo ni rahisi kumtofautisha tajiri asiye na shukrani na yule anayefahamu mipaka ya nafasi yake kama mwanadamu. Kukosa shukrani ni tawi mojawapo komavu la kiburi - ambacho mwisho wake ni fedheha.

^Appreciation is a wonderful thing. It makes what is excellent in others belong to us as well.^ ~Voltaire
 
Wewe umezaliwa family ya watu wenye Imani Kwa Mungu??? Ni nini kilikufanya ukaona hakuna MUNGU?? Ni elimu nzuri?? Experience ya maisha?? Au ni changamoto zilizotokea???
 
Kwa nini Mungu anataka binadamu wamuabudu, wamuombe, wamtolee sadaka na kumshukuru?

Kama unaamini Mungu yupo ni dhambi usipomuabudu, usipomuomba au usipomshukuru? Yani kama unakubali yupo lakini haufanyi ibada au shukrani yoyote kwake wewe unahesabika ni muovu? Atakufanikishia mambo yako?

Kwa nini wengine anawaambia wasali mara tano kila siku na sio mara kumi, mara moja, kila saa n.k?? Kwa nini wengine wanajiamulia kumuomba wakati wa kuamka, wakati wa kulala na wakati wa baadhi ya matukio tu kama kabla ya kula, kabla ya safari, kabla ya mechi n.k??

Psychological tu!
 
Kwanza jua kwa nini umeletwa duniani! Ukishalijua hili maswali yako yatakuwa ni mepesi sana kwako!
Sasa labda mama kahangaika sana kwa waganga wa ibilisi anataka mimba hapati, au kapata mimba bahati mbaya ukazaliwa.... Hapo malengo nini kuletwa duniani?
 
Binafsi sikuomba Mungu anilete duniani.
Alinileta kwa shida zake mwenyewe kwahiyo yeye ndiye anatakiwa anisujudie.
Acha kufuru wewe Mungu gani alikuleta duniani? Wewe ni Yesu?
Mungu alimtoa mwanae pekee ili kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele.
Wewe labda umezaliwa bahati nzuri tuu endelea kutafuta hela.
 
Sasa labda mama kahangaika sana kwa waganga wa ibilisi anataka mimba hapati, au kapata mimba bahati mbaya ukazaliwa.... Hapo malengo nini kuletwa duniani?
Mwanadamu amekuja ulimwenguni ki tawassuli!

Wale wazazi wetu ni tawassuli ya kuja ulimwenguni! Mungu alikuwa na uwezo wa kututeremsha tu bila ya baba na mama.

Tawassuli ni kupitia kwenye kitu fulani ili ufikie kwenye lengo!

Mifano uliyoitoa ni asbab ila ilishaandikwa wewe uwe ulimwenguni kama binadamu.

Kama Mungu asingelitaka uwepo hata zingelitumika hizo sababu ambayo ni mifano uliyoitoa, basi usingelikuwepo. Uwepo wako tayari alishaupanga uwepo na ndiyo maana upo!

Swali la msingi litakuja: aliyesababisha uwepo wangu uwepo ni nani? Na kama amenifanya niwepo anataka nini kwangu?
 
Kwa nini binadamu tumeletwa duniani?
Kwa malengo zofauti tofauti..
Warusi waliletwa duniani kupinga uonevu wa wamarekani na vibaraka wao.
Wachina waliletwa kwa ajili ya kuvumbua vitu mbalimbali vya kurahisisha maisha.
Waafrika tulikuja kuzaana ili tupewe msaada wa silaha tuuane wenyewe kwa wenyewe.
 
Back
Top Bottom