Kwanini Watu wema wanateseka?

Kwanini Watu wema wanateseka?

joex

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2011
Posts
1,598
Reaction score
1,294
Labda wewe ni miongoni mwa watu ambao wanajitahidi sana kufanya yaliyo mema machoni pa Mungu na kusaidia jamii.

Hata hivyo pale unapopata mateso maishani labda kwanini ninateseka hata ingawa nimejitahidi kufanya yote yaliyomema!

Endapo umefikia hatua hiyo na kujiuliza maswali hayo, nakutia moyo kuwa hauko pekeyako. Na kwakweli kwa silika ya mwanadamu ya kupenda haki, kuona wanadamu wema wanateseka ni lazima kutatokea maswali kama hayo na hata zaidi labda ukatilia shaka kusudi la Mungu kutuumba au hata kuwepo kwake.

Fuatilia nami kwenye Kiambatishi
 
Attachments

Kwanini watu wema wanateseka-2.jpg
 
Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na Mateso?

Badala yake Dunia ya mateso ipo, Watu wanateseka?

Huyo Mungu yupo kweli?

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Alafu yeye pia kuna watu aliwatesa na kuwaua kabisa wengine aliwabadilisha wakawa Jiwe la chumvi kisa tu kutofautiana mitazamo. Noma
 
Aisee na Mungu anaangalia tu mnateseka. Poleni ndugu zetu
Vita vyetu sio vya damu na nyama ni vya kiroho...

Mungu wetu ametupa uwezo ambao ni nguvu za Rohoni za kupiga falme zote za wakuu wa giza...
 
Duuh nilitegemea Mungu asingewaweka kwenye vita
Si hivi ulivyofikiria vita wanayopigwa watu wa mungu ni kule kuwa kwao kinyume na waovu hakuna mtu wa mungu atakayeshabikia pombe, kamari, uzinzi, wizi, kula kisicho halali yake na mengineyo mf wa haya na dunia tuliyonayo haya yamekuwa ni vitu vya kawaida sana
 
Labda wewe ni miongoni mwa watu ambao wanajitahidi sana kufanya yaliyo mema machoni pa Mungu na kusaidia jamii.

Hata hivyo pale unapopata mateso maishani labda kwanini ninateseka hata ingawa nimejitahidi kufanya yote yaliyomema!

Endapo umefikia hatua hiyo na kujiuliza maswali hayo, nakutia moyo kuwa hauko pekeyako. Na kwakweli kwa silika ya mwanadamu ya kupenda haki, kuona wanadamu wema wanateseka ni lazima kutatokea maswali kama hayo na hata zaidi labda ukatilia shaka kusudi la Mungu kutuumba au hata kuwepo kwake.

Fuatilia nami kwenye Kiambatishi

Kwa sababu wengi ni wajinga/maamuma.
Wakati waovu wengi wapo smart.
 
Si hivi ulivyofikiria vita wanayopigwa watu wa mungu ni kule kuwa kwao kinyume na waovu hakuna mtu wa mungu atakayeshabikia pombe, kamari, uzinzi, wizi, kula kisicho halali yake na mengineyo mf wa haya na dunia tuliyonayo haya yamekuwa ni vitu vya kawaida sana
Hivyo vimekuwepo tangu kabla hata yesu hajazaliwa mkuu, kumbuka pia muujiza wa kwanza wa Yesu ni kubadili maji kuwa divai/mvinyo. Watu wa mungu tumeambiwa tunywe kwa kiasi
 
Unaweza kutenda mema ukamuudhi Mungu nikupe mfano. Kuna gari lilidumbukia kwenye maji pale kamanga mwanza. Vijana waliojitolea kwenda kuokoa walipokuja maaskari waliwatoa kwa virungu na fimbo eneo la tukio kwa maana ya kuingilia majukumu yao mamlaka ya uokozi. Yaani wao mamlaka ndo wanajua mfumo na mipango ya uokozi inavyokwenda. Tunaenda sasa kwenye maada.

Mungu ndiyo hupanga kila kitu. Hata mateso kwa watu unaowahurumia wewe anakuwa kayapanga yeye. Huenda hao watu kuteseka kwao ni adhabu ya Mungu kwa mkosa yao ya nyuma ama wazazi wao
Sasa we unapowasaidia utakuwa umepinga hukumu ya haki ya Mungu juu ya waharifu. Kwa kifupi umetorosha wafungwa wa Mungu katika gereza la Mungu na bado unataka Mungu akuongezee baraka. Hapo anachokifanya ni kukuweka na wewe gerezani kwa kosa la kutaka kutorosha wafungwa wake. Tena ikibidi wewe adhabu yako yaweza kuwa kubwa kuliko hata hao.

Hapo ndo watu wema yanapowakuta mambo mabaya. Ushauri

Acheni kutorosha wafungwa wa Mungu kwa kujifanya munahuruma sana
 
Back
Top Bottom