R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,178
Nami wala nisiwe mnafki sitaki nijifiche kwamba ni mwema kwamba niwakemee wengine
Watu wengi tumepata bahati ya kuweza kuja hapa duniani tukiwa na bahati kubwa sana ya kupata malezi ya kulishwa, kuvishwa, kuishi nyumbani na kulelewa na wazazi ama ndugu walioweza kujitwika hayo majukumu.
kuna hawa wenzetu ambao hawakuipata hio bahati, aidha wazazi walifariki bila kuwajua ndugu, waliishi na wazazi / ndugu wanaowatesa wakaamua kutoroka, kupotea mitaani wakiwa watoto, kutekelezwa mitaani, n.k.
Sasa unakuta sisi ambao tuliweza walau kupata hizo bahati za kipekee huwa hatujiongezi, tunakutana na hawa wattoto ila tunawapuuza na hata tukifatwa mtu anaweza jifanya yupo bize kumbe anakwepa maksudi kwa kuona ni kero, wengine hudiriki kuwafukuza kabisa.
Binafsi nimewahi kusaidia saidia hawa watoto ila misaada yote jumla ni kama elf 40 tu, nafsi inanisuta kamba sijawahi hata hii misaada haifikii hata asilimia 0.01 ya bahati niliyopata ya kuwakuta wazazi wangu walionilea na kunipa mahitaji kadri ya uwezo wao,
nimejikuta najiona nina ubinafsi mkubwa sana, pengine hii ndio mitihani tunayopewa pindi tukizaliwa, haijalisgi hata uende kanisani / msikitini bila kuwazingatia wenzako wa kundi hili, bado huwezi kupata idhini yale Muumba.