GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Wachokoza Mada hasa za Kiserikali na Matukio Nyeti hasa yaliyobeba Hisia za Watu.
Watu ambao huwa hawakosekani Vijiweni 24/7 ila huwa wakimya tu na hawachangii lolote.
Watu ambao hupenda mno Kuchambua mambo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi Kiufasaha.
Watu ambao wakiondoka hapo Vijiweni huwa hawaagi na utashtukia tu hawapo Kitambo.
Watu ambao hupenda kuja Vijiweni mara kwa mara ila huwa hawapendi Kujulikana waishipo.
Watu ambao wakiwa Vijiweni hata ukiomba mbadilishane Namba watakataa au kukukwepa.
Watu ambao mkiwa mmekaa Kijiweni mnashtukia tu wamekuja na huwa hawaanzi Kusalimia.
Nawasilisha.